Miss Natafuta
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 26,953
- 49,705
Kijana upo 35 hadi 40 una watoto 3 au 2, mama tofauti bado unatafuta mke wa kuoa, halafu kwenye thread za kuponda masingle maza wewe upo, hutaki single maza, hao wadada wa watu uliowazalisha unataka nani awaoe unavyohamasisha wenzio wasiwaoe? Ila jua hata kama ukioa bikra aliezaliwa leo dhambi ya kuzalisha wengine itakutesa mpaka ukome.
Halafu wanawake inabidi tuamke, mwanaume akikuzalisha hata kama una uwezo usikubali kulea mwenyewe hata kama hutaki mawasiliano nae nenda polisi ustawi wa jamii wapo anapewa kiwango cha kupeleka kila mwezi wewe unafata tu pale wala huna haja ya kuonana nae. Hichi kiburi cha kuwaacha wasitoe hela kisa tunawachukia ndo kinawafanya waendelee kutuzalisha hovyo.