Hivi huu wote ni uongo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huu wote ni uongo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlachake, Apr 9, 2011.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Na Mwandishi Wetu, Loliondo
  Tiba ya kikombe inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa KKKT, Ambilikile Masapile ‘Babu’ imeendelea kubeba maajabu kila kukicha.
  Risasi Jumamosi kupitia uchunguzi wake, limebaini matukio 10 ya miujiza ambayo yametokea Loliondo tangu Babu alivyoanza kutoa tiba hiyo.

  Tathmini ya gazeti hili, inaweka matukio hayo kwa mtiririko wa namba kulingana na ukubwa wake kama ifuatavyo;
  1. MGONJWA KUTAPIKA NYOKA
  Tukio la mgonjwa aliyetapika nyoka, limeweka rekodi ya aina yake, hivyo kuongoza miujiza hiyo.

  Wiki iliyopita, gazeti hili liliripoti tukio la mgonjwa aliyefika kwa Babu kwa lengo la kutibiwa lakini akatapika nyoka baada ya kupata kikombe.

  Ilielezwa kuwa, nyoka huyo aliwekwa tumboni mwa mgonjwa huyo kwa njia za kishirikina.

  2. KUZAA NYAMA
  Tukio la pili ambalo linabeba miujiza kwa Babu ni lile la mgonjwa aliyekwenda kwa matatizo ya uzazi, matokeo yake akajifungua kipande cha nyama baada ya kupata kikombe.

  Ilielezwa kuwa, mwanamke huyo (jina lake halikufahamika) baada ya kupata kikombe, alihisi tumbo kuvimba, baadaye kushikwa uchungu wa uzazi, akajifungua kipande hicho cha nyama chenye uzani wa kilo mbili.

  Taarifa iliyotolewa baadaye ni kuwa mwanamke huyo alikuwa amefungwa uzazi kwa njia za kishirikina.
  3. KIZAAZAA CHA POCHI
  Pochi ya Mkenya iliyoibwa Loliondo ikiwa na hati ya kusafiria na fedha za Kenya Shilingi 20,000 (zaidi ya shilingi 356,000) iliibua kizaazaa na kuwa moja kati ya maajabu 10 ya Babu.

  Ilielezwa kuwa, baada ya Mkenya huyo kuibiwa na taarifa kuenea, Babu alitoa agizo kwa aliyeiba kurejesha pochi hiyo, vinginevyo angechapwa na Mungu.

  Baada ya agizo hilo, mhusika aligoma kurudisha pochi lakini dakika kadhaa zilizofuata, kijana mmoja alianza kulalamika anachapwa fimbo na mtu asiyejulikana, huku akijitaja kwamba yeye ndiye aliyeiba.

  4. WALIOUA NYOKA WAKIONA
  Tukio lingine la maajabu lilitokana na mtu aliyetapika nyoka.
  Habari zinasema kuwa baada ya mtu huyo kutapika nyoka, Babu aliagiza ‘mdudu’ huyo asifanywe chochote mpaka aondoke mwenyewe.
  Hata hivyo, baadhi ya watu walikosa uvumilivu, kwa hiyo walimpiga nyoka huyo mpaka akafa.

  Saa chache baada ya nyoka kuuawa, wauaji walianza kuugua, huku wakilalamika kuchomwa chomwa mwilini na vitu visivyoonekana.
  Watu hao, baadaye walipelekwa kwa Babu ambaye aliwaombea wakapona lakini aliwapa sharti la kuzingatia anachoagiza.

  5. MZIMU KWENYE DAWA
  Tukio lingine la ajabu kwenye himaya ya Babu ni lile la mzimu ulioonekana kwenye foleni.

  Mwanamuziki zao la Bongo Star Search (BSS), Baby Madaha ambaye alikwenda Loliondo kupata kikombe alisema kuwa, aliishuhudia mzimu wakati akisubiri zamu yake.

  Baby alisema kuwa, awali alidhani mzimu huo ni mtu wa kawaida, lakini watu wakamwambia siyo na kufumba na kufumbua ulitoweka.
  Baadaye alielezwa kuwa ule ni mzimu na kufafanuliwa kwamba kwenye himaya ya Babu Ambi kuna miujiza mingi.

  6. KUPONA KABLA YA KIKOMBE
  Kuwepo kwa watu ambao wametoa ushuhuda wa kupona kabla ya kupata kikombe ni maajabu mengine ya Babu.

  Imeelezwa kuwa, watu hao ambao hutoka nyumbani kwao wakiwa wagonjwa, hupona wakiwa kwenye foleni, hivyo hunywa kikombe ili kukamilisha safari yao ya tiba.

  Janette Ismida wa Morogoro alilithibitishia gazeti hili wiki iliyopita kwamba, alipona kwenye foleni, alisema: “Nafikiri imani ndiyo inaponya. Mimi nilikuwa na kiharusi, mdomo wangu ulikuwa umepinda.

  “Nikiwa kwenye foleni nilishangaa nashikwa na baridi kali, nikaona maruweruwe. Kikafuata kigiza fulani hivi wakati ni mchana. Baada ya hapo nikapona, nikawa naweza kuongea, kwa hiyo nilikunywa kikombe kukamilisha tu.”

  7. MAPEPO YALIPUKA
  Tukio lingine la ajabu ni lile la wanawake mbalimbali kulipuka mapepo wakiwa hatua chache kumfikia Babu, wakiwepo walokole.
  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, huwa haipiti siku bila wanawake wasiopungua 10 kulipuka mapepo na kuzungumza vitu vya ajabu kwa lugha mbalimbali duniani.

  8. VIBWEKA VYA WACHAWI
  Gazeti hili lilielezwa na mmoja wa wasaidizi wa Babu kuwa, wachawi wamekuwa wakifika Loliondo kufanya vitendo vya kumjaribu mchungaji huyo lakini siku zote wameshindwa.

  “Wachawi wanamfikia sana Babu, lengo lao ni kuona nguvu zake lakini kwa taarifa ni kuwa hawamuwezi, ” alisema mmoja wa wasaidizi wa Babu aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini.
  9. WANAOMUIGA WAKOSA MVUTO

  Tangu Babu Ambi aibuke Loliondo, watu mbalimbali wamekuwa wakitoa ushuhuda wa kufunuliwa kwenye ndoto utabibu wa njia ya kikombe.

  Hata hivyo, kwa kile kinachoonekana ni nguvu ya Babu, wote waliojitangaza wamekosa mvuto, hivyo Loliondo imebaki kuwa kimbilio kuu la wagonjwa wenye maradhi sugu.

  Watu ambao wamejitangaza kutoa tiba hiyo mpaka sasa ni Fatma Said Sengo ‘Bibi’ wa Morogoro, Margaret Mutalemwa ‘Dada’ wa Tabora wakati Mbeya kuna kijana, Jafar Welino ‘Kaka’.

  10. KICHAA CHA BIBI KIZEE
  Tukio la 10 la ajabu ambalo lilichukua nafasi Loliondo ni la bibi kizee (jina tunalo) ambaye alipelekwa kupata tiba ya kikombe.
  Bibi huyo baada ya kunywa dawa, alipona ghafla wakati kwa miaka mingi alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kurukwa akili.

  Kwa mujibu wa ndugu aliyeongozana naye, bibi huyo alirukwa akili kwa zaidi ya miaka 30, hivyo walimpeleka kwa Babu Ambi kama kubahatisha.

  “Mungu mkubwa sana, hatukutegemea. Alipokunywa tu kikombe alishangaa amefikaje pale, halafu akaomba apewe maji aoge kwa sababu alikuwa mchafu,” alisema ndugu huyo (jina tunalo).
   
 2. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  The devil at throne in Samunge. Be warned everyone. Open your eyes and see.

  More tomorrow. God bless you all.
   
 3. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu, naona umeamua kutoka kiudaku zaidi...................
   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hata CCM nao wanaweza kuandika maajabu ya utawala wa Kikwete.
  1. Kafanikiwa kujenga umoja Zenji
  2. Kafanikiwa kujenga UDOM
  3. Kafanikiwa kuongeza shule za kata na walimu nk.
  Kwahiyo katika perspective zote mazuri huwa yapo hata kama mabaya ni mengi zaidi.
  Mfano;
  1. Wagonjwa wengi wamepoteza maisha.
  2. Wengi hawajapona maradhi yao.
  3. hakuna utafiti unaonyesha dawa yake inatibu. hii nayo ni miujiza nk.
   
 5. C

  Clego Member

  #5
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alioteshwa atatibu magonjwa mangapi?
   
 6. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,060
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Whether that's real or not, my fellow members here, let's repent and accept Jesus as our Lord and savior. Let's allow him to guide our day to day life. I can testify to everyone here it is good to be in Jesus and you don't need babu's vision or whatever he calls it. Jesus can heal your pain all you need is to believe in him and allow him to be your King.
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna jukwaa la dini kule
   
 8. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  1. Kutapika nyoka si jambo la ajabu katika uganga wa jadi. Ndio maana tunasema shetani anaweza kuweka ugonjwa halafu akauondoa ili kukufunga kwake. Ndio wanayofanya akina manyaunyau kila siku. Ndivyo hivyo hata kuzaa nyama.

  2. Mungu kuchapa mwizi. Hakika inashangaza sana juu ya utendaji wa Mungu wa Samunge. Mungu anayetajwa kwenye biblia hushughulika na mwili lakini zaidi na roho ya mtu. Sasa baada ya kutembeza bakora yule jamaa akaapa kutorudia kuiba hapo Samunge, imemfaidia nini kiroho? Mungu huyu anayejali miili tu anafanana na utendaji wa majini ambao hutumwa kichawi kuwaadhibu watu. Ama hujapata kusikia watu waliopoteza mali wakaenda kwa mafundi kusomewa aya? Ndivyo hivyo hata kwa wale walioua nyoka. Mungu wa kuchoma watu misumari? Kisha walipoombewa wakapona kwa sharti la kuzingatia maagizo ya babu. Sasa hapa mbona babu ndio anasimama kama Mungu? Masharti yapi tena zaidi ya neno? Give me a break!

  3. Inaonekana Samunge ni eneo maalum kwa ajili ya mapepo. Kwamba pale mizimu na majini huonekana mara kwa mara ni uthibitisho tosha wa kazi za babu. Na huyu Madaha aliyeona mtu mwenzake kwenye foleni kisha wengine wakamwambia sio, hao walijuaje kwamba huyo si binadamu? Yaani mgonjwa anaona mzimu kwenye foleni na anatulia tu? Napata wasiwasi juu ya jamii inayokwenda Samunge. Hayo mapepo yanahusiana na baadhi ya wagonjwa huku wengi wakienda bila kujua kinachoendelea pale. Kwa Yesu mapepo hupiga magoti na kukiri ukuu wake, na si kufanya mizaha ya kuonekana na kutoweka mbele za watu. Halafu watu wakachukulia matukio hayo ni uwezo wa Mungu.

  4. Kupona kabla ya kikombe yaweza kuwa ndio kazi ya hiyo mizimu kwenye foleni. Kiharusi na mdomo kupinda ni kifungo cha mapepo hicho. Hivyo yanapofika Samunge yanamwachia mgonjwa kwa vile tayari anakwenda kugongwa muhuri. Kisha yanatembea tembea kwenye foleni kuwazingua akina bebi madaha kisha hutoweka kwenda mawindoni kusaka wengine.

  5. Tukio la mapepo kulipuka wakiwemo walokole!? Nani kakuambia Samunge kuna walokole? Mtu anachukua hatua kwenda Samunge tayari anaukana wokovu wa Kristu Yesu. Na hilo la mapepo kulipuka si ajabu, shetani ni bingwa wa kuigiza. Sasa hapo samunge anawafunga wanawake, na kuwagaragaza chini ili "wafuasi wa babu" wazidi kuiamini nguvu hiyo ya upotevu.

  6. Wachawi kufika mara kwa mara kumjaribu babu. Yeye anasema "hawamwezi." Hatujaona hata mchawi mmoja aliyejisalimisha kwa nguvu ya Mungu mkuu (kwa jina la Yesu). Badala yake twashuhudia mapambano ya kuzidiana tunguli tu. Huyu si Yesu nimjuaye mimi. Mkasa huu unanikumbusha nguvu kubwa sana aliyopewa Iyke Uzorma wakati akitumikia ulimwengu wa giza. Someni kitabu kiitwacho "MKUU WA WACHAWI SASA AMPOKEA KRISTO, kimeandikwa na Iyke Nathan Uzorma."

  7. Kukosa mvuto kwa wanaomwiga si kweli. Sababu kubwa inayofanya wasisikike ni media kumfanya babu celebrity wa waganga wa kienyeji. Serikali nayo imechukua uwakala wa kumtangaza babu. Yaani mpaka anapewa hati miliki ya mti wa Mugariga. Hebu watangazwe na wengine uone idadi ya watu wanavyojaa huku ndipo utakapo tambua nguvu ya upotevu inavyotenda kazi.

  8. Kicha ndio hukohuko kutokwa na mapepo baada ya kufika kwa mkuu wao aliyepo Samunge. Ushahidi uko wazi zaidi. Alipona bila ya IMANI. Imekuwa ikiimbwa kila siku hapa kwamba imani ndio msingi mkuu wa uponyaji Samunge. Lakini kwa bibi huyu hata ndugu zake walikuwa wakibahatisha tu. Mnataka msikie nini ndio muamini kwamba babu anatenda kwa nguvu tofauti na Mungu aliye juu?Watu wanafunguliwa kimwili halafu milango inaachwa wazi bila kufungwa. Bila kumpa Yesu maisha yote hayo yanayotendeka Samunge ni bure kabisa. Mungu hushughulika na roho za watu ndio maana Kristu alikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele. Mwenye masikio na asikie.

  Mungu Awabariki nyote. Nawasalimu katika jina la Yesu, Amina.
   
 9. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Wheather dawa ya babu inaponya au haiponi, thats non of my concern, kama unaumwa na una imani unawezapona na kikombe cha babu, chapa mwendo loliondo.
   
Loading...