hivi huu sio ubinafsi wa wanafunzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hivi huu sio ubinafsi wa wanafunzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ms Judith, Feb 5, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  siku hizi huwezi kusikia wanafunzi wa hapa kwetu wakiandamana kupinga mambo ya kitaifa kama malipo wa dowans nk. utawasikia tu baadhi ya waalimu wao kama Prof Baregu, Prof Shivji nk wakizungumza na wanhabari, ila likija suala la mikopo inayotumbukia mifukoni mwao wako tayari hata kufa! nasikia wengine mimba zinaharibika wakipigania kuongezwa viwango vya hiyo mikopo.

  mi naamini baadhi ya harakati zikifanywa vizuri na wanafunzi zinaweza kuwa na tija kubwa sana kwa taifa. mfano wanafunzi wa UDOM na vyo vingine vya dodoma wanaweza hata kwenda kuzingira ukumbi wa bunge linapojadiliwa suala muhimu la kitaifa kama dowans ili kushinikiza bunge kuwajibika kwa wananchi badala ya kuwafurahisha wakubwa wa serikali

  sasa maswali yangu ni haya:
  1.
  tabia kama hii haiwezi kuwa ni kielelzo cha aubinafsi wa hao wadogo zetu?
  2.
  lini wataanza kugoma na kuandamana kushinikiza masuala muhimu ya kitaifa kupewa uzito wake na wakubwa?
   
 2. B

  B4U Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yes you are very right Juddy, ni leo tu nimetoka kuwa andikia barua kupitia gazeti la Mwanahalisi, ni kionmba barua hile itoke hili iwafikie wengi maana Mwna halisi nao ni wachaguzi wa barua, barua hiyo ililenga kuwaonya juu ya maandamano yasiyo na tija kwa taifa wakati Taifa lipo katika wakati mgumu tangu kuzaliwa sijaona, tuliwahi kuwa na baa la njaa hapo nyuma lakini ukiangalia kwa makini hili la sasa ni zaidi ya baa la njaa, maana ikiwa tunaita hakuna njaa chakula kipo lakini hakinunuliki hii utaita nini? alafu hawa wa andamana kutaka waongezewe 5000/- wana akili sawa sawa hawa! hivi utathubutu kumuita mtu msomi katika mantiki hii kweli? au usomi wa magazeti ya Udaku, let say ombi lao limekubaliwa tena badala ya kupewa 5000/- wakapewa 10,000/- alafu kesho kina kuwa nini? hivi wana akili sawa sawa hawa? walau wangetumia hata elimu yao kidogo kwa kufikiri, nina mashaka hata madarasani hawa ambulii kitu, au wanasoma kujibu mitihani tu! this is crazy!!!!!!!!!!!!!!!!! ok wao wamepewa nyongeza ya boom!! wazazi wao huku majumbani anawapa nani boom!!! badala ya kuandama uongozi utafute mbinu mbadala ya kukwamua taifa na umaskini na mfumuko wa bei, ambao hata wangepewa 50,000/- bado isingetosha hapo siku za usoni, heti ni wasomi wana andamana natamani hata kuwatukana.......!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  maslahi binafsi!
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mimi sipingi wao kuandaman ila nauliza kwa nini hawaandamani kwa maslahi ya taifa bali wanaandaman pale wanapodai maslahi yao tu? na lini wataitisha maandamano yanayolenga kushiniiza maslahi ya taifa zima kama wafanyavyo mfano TGNP na wadau wengine mara kwa mara?
   
 5. M

  Matarese JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Zimeharibika mimba za wangapi? taarifa za jana ni mmoja tu ndie aliharibikiwa mimba, generalization yako inapoteza mantiki nzuri ya ├║lichokiandika na kuingiza uswahili!
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  samahni naomba kujua kuwa kwa standard zako mimba zapaswa kuharibika ngapi ili ziwe worth of being mentioned here?

  back to the point, issue sio mimba kuharibika au wanafunzi kuandamana. issue bi kwa nini kila mara wanashinikiza mambo yao na hawajitokezi kushinikiza masuala mengine ya taifa zima kama wanaharakati wengine wa makundi mbalimbali?
   
 7. peck

  peck JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  judy inawezekana huwa unachagua habari za kusikiliza! suala la migomo sio mikopo tu japo kuwa pesa ndo kila kitu katika maisha ya shule.
  Naomba nikumbushe baadhi ya migomo ambayo haihusu MIKOPO.
  1. CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII- IRINGA, Walikuwa wanadai maji safi kwani wanatumia maji ya mtoni yanayowasababishia magonjwa.
  2. TAASISI YA USTAWI WA JAMII- DAR, Walikuwa wanadai bodi ya chuo, udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza etc
  3. CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI, Wanadai jenereta kuweza kuendana na muhula wa masomo kwani tatizo la umeme naamini hata wewe walifahamu.
  4. CHUO KIKUU CHA TUMAINI DAR, Wanadai punguzo la ADA kwani ada wanayolipa ni kubwa sana (Milioni mbili na nusu) na HAWALI, HAWALALI wala HAWATOLEWI FOTOKOPI na chuo.
  LET THEM FIGHT FOR WHAT THEY FEEL IT IS RIGHT FOR THEM
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  katika hayo, ishu ya kitaifa ni ipi?

  nijuavyo mimi hakuna taasisi ambayo imekamilika kwa kila kitu na internal adjustments kwa lengo la kujiimarisha ni natural process of every open system. kudai maboresho ya ndani ni mambo amabyo hata majumbani tunakoishi yapo. tusikatae ukweli kuwa hawa wadogo zetu wanaweza kuishia kuonekama wabinafsi mbele ya watanzana kama hawatkuwa wakijishughulisha pia ma mashinikizo ya mambo ya kitaifa kwani ni a very sensitive social group. wanaweza kujifunza hata kutoka kwa wanafunzi wenzao wa nchi nyingine
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hawa wanafunzi wanachekesaha sana,:twitch:
   
Loading...