Hivi huku sio kubaka kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huku sio kubaka kweli?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Felixonfellix, Oct 14, 2011.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [h=3][/h] [​IMG]

  Kama kubaka ni hali ya mwanaume au mwanamke kulazimisha kufanya tendo la ndoa bila hiyari ya mwingine, basi wanawake wengi sana walioko kwenye ndoa hubakwa na waume zao kila siku.  Kubakwa huku kunatokana na ukweli kwamba wanawake wengi hulazimika kukubali kufanya tendo la ndoa na waume zao kutokana na mazingira mbalimbali yaliyo nje ya upendo.


  Kuna ndoa nyingi ambazo zimekufa, ingawa wanandoa wanaishi pamoja. Zimekufa kwa sababu hazina mawasiliano kabisa. Lakini cha ajabu ni kwamba, watu hawa wanakutana kimwili na pengine kuzaa watoto. Kwa sehemu kubwa kwenye ndoa za aina hii, wanawake huwa hawako kwenye ukamilifu wao kimawazo.


  Mara nyingi athari huwa ni kwa wanawake kwa sababu wao kimaumbile huishi kihisia. Kutokana na kuathirika kimawazo hamu yao ya kushiriki tendo la ndoa nayo hupotea.


  Kwa kuwa hawana hamu ya kushiriki tendo la ndoa, waume zao wanapowaambia, ‘geuka huku’ (hawaongei zaidi ya hapo kwa sababu hakuna mawasiliano), hufanya hivyo. Na hufanya hivyo huku wakiwa hawataki.


  Sio wengi wanaoweza kukataa kwa sababu hawakulelewa katika mazingira yanayoweza kuwafanya wakatae. Wamelelewa kwenye mazingira ambayo yamewaambia, miili yao hawana haki nayo mbele ya utashi wa waume zao!


  Ukiacha mawasiliano kuna ndoa ambazo wanaume ni Malaya sana, walevi, au wapigaji. Kwenye ndoa za aina hii unaweza kukuta mwanamke bado anaendelea kuwepo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ya utegemezi au watoto. Pamoja na kuendelea kwao kuwepo, hamu ya tendo la ndoa na waume zao nayo inakuwa haipo  Lakini mwanaume hatakiwi kunyimwa mwili wake anapouhitaji. Kwa hiyo, kinachotokea ni mwanamke kufanya mapenzi kwa kujilazimisha au kulazimishwa..
  Kuna kesi nyingi ambapo tumesikia juu ya wanaume kuwauwa wake zao kutokana na kuwakatalia unyumba au wakiwa wanapigana baada ya mwanamke kukataa kushiriki tendo la ndoa.

  Kwenye ndoa nyingi wanawake hubakwa, yaani hushiriki tendo la ndoa bila hiyari zao. Hulazimishwa au hujilazimisha kutokana na nafasi ambayo jamii imewapa.


  Ni kwa nini basi tunapozungumzia kubaka tusiwaambie wanawake na kuwashauri wawe macho na ubakaji huu ambao
  una athari kubwa kwao na kwa jamii wakiwemo watoto wanaozaliwa kwenye ndoa hizi za kibabe?


  Source: kaluse.blogspot.com
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  mi bado kuvunja sinia, msiniharibu
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kwa wazungu haya
  kwa waafrika inafahamika ukikubali kuolewa unakubali yote....
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  mimi nadhani mtu akishaanza kutoa 'ushirikiano' kunako 6x6 suala la kubakwa linapotea hapo hata kama alilazimishwa
   
 5. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  -kuna maandiko katika biblia yanasema mume ana haki juu ya mwili wa mkewe alikadhalika mke juu ya mwili wa mumewe.....
  -sheria ya ndoa ya tz (LMA 1971) mume habaki mkewe ispokuwa kama wawili hawa wapo under separation hapa talaka inakuwa bado kutolewa....
  -hivyo kwa mujibu wa dini na sheria mume na mke wanaolala chumba kimoja hawabakani hata kama mmmoja hajaridhia tendo...-

  -my take; its not health for spouses to have sex before resolving their conflicts or when one has not given his/her consent
  -wanaoathirika zaidi ni wanawake kwa sababu kwao tendo la ndoa huusisha hisia zaidi its more than physical need , kwa hiyo kama hajaridhia ni rahisi kuadhirika kisakolojia.
  -sex isitumike kama silaha ya kunyimana haki yenu ya ndoa.
   
 6. Bambanza jr.

  Bambanza jr. JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huku sio kwao binti nenda majukwaa mengine usije ukadumaaa!
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  dah nazjaz kumbe zile post zako haziendani na umri wako ?
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Nimefarijika matron!
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mama usingizi haukuji nimejikuta na msongo wa mawazo ikabidi nipige chabo JF ,bestlady ngoja nilale nisije kukulilia kesho
  take care
   
 10. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sina la kuongeza ime2lia had raha
   
 11. bht

  bht JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Relax..... (usiuruhusu)
  Kimbia haraka kitandani!

  Nailyne......asante kwa maelezo !
   
 12. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kama sio kweli. Hata wanaume wa kiafrika wanafaham kuna wakati hutakiwi ku-insist kama mwenzio amekataa. Ila kwa upande mngine ni kweli, kubakwa kuna definitions nyingi na sio lazima tukubaliane na definition ya wazungu.
  Mi nadhani kama mtu anatoa shingo upande (angependa asitoe ila anajilazimisha kutoa) sio kubaka. Kubaka ni wakati hataki kabisa kutoa na ANALAZIMISHWA kutoa kwa kutishiwa physicaly au mentaly (atapigwa, watoto watapigwa, hata hudumiwa, atashtakiwa kwa wazazi etc).
  Sijui wengine mnasemaje hapa?
   
 13. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #13
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nyie ndo mnaosema hivi alafu siku ukifunuliwa kunakuwa wazi, unaanza kudanganya nilikuwa naumwa Dr akaniingizia vyuma...
   
Loading...