Hivi hili ni kosa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi hili ni kosa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by demokrasia, Jun 8, 2012.

 1. d

  demokrasia Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mwanaume. Nina mpenzi wangu ambaye bado yupo chuo anasoma. Nimekuwa nikijitahidi kumsaidia mambo mengi sana pale hali yangu ya uchumi inaporuhusu. Hivi majuzi ilitokea huyu binti alipata tatizo la kutaka kuzuiwa kufanya mitihani kwa sababu alikuwa hajamaliza kulipa ada, hivyo akaniomba nimsaidie. Kutokana na majukumu mengi niliyokuwa nayo wakati huo, kiasi cha pesa alichokuwa anahitaji ndicho kilichokuwa nimebaki nacho kwenye akaunti yangu. Nilimweleza hali halisi, lakini yeye akaniambia kuwa nimpatie tu hiyo hiyo kwa sababu anategemea kupewa hela hiyo na mzazi wake wiki inayofuata halafu atairejesha. Kutokana na uzito wa jambo hilo, nilikubali kukausha akaunti yangu nikampatia pesa hiyo. Baada ya kumaliza mitihani, nilimwambia kuwa baba yake akimpatia hiyo pesa, asinirudishie yote bali aigawe, nusu anirudishie na nusu abaki nayo ili imsaidie kwenye matumizi yake binafsi. Cha kusikitisha huyu binti alianza kunirushia maneno ya kashfa kuwa mimi ni mshamba, maskini, limbukeni, kwa sababu eti kuna wanaume wanahonga magari lakini hawadai. Pia alifikia hatua ya kunikatia simu pamoja na ku-block namba yangu.Wana JF hayo maneno yaliniuma sana kwa sababu ni mambo mengi sana nimemsaidia siku za nyuma na sijawahi kumdai anirudishie. Sema tu this time ilitokea hivyo kwa sababu uchumi wangu ulikuwa umebana. Kutokana na jinsi ambavyo nilichukia kwa maneno yake ya kashfa aliyonitolea, niliamua kuwaeleza wazazi wake kuhusu anayoyafanya binti yao. Wazazi walinishukuru sana kwa kuwapa hizo taarifa na walisikitika sana na kuahidi kuchukua hatua ya kumuonya binti yao. Sasa kwa upande wa huyo mpenzi wangu, ananilalamikia kuwa nimefanya kitendo ambacho sio cha kistaarabu na nimemdharau. Wana JF naomba mawazo yenu, je hapo nimekosea kuwaeleza wazazi wake?
   
 2. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  mfadhili mbuzi si mwanadamu mkuu...tupa kule anza maisha mapya pesa zinatafutwa tu mkuu...
   
 3. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Piga chini kimeo hicho
   
 4. LD

  LD JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Acheni hao wanafunzi wasome jamani....mnawaweka kwenyematatizo sana hamjui tu ninyi vijana. Tamaa ya pesa inazidi kumuingia mapema. We fikiria una kibinti cha mwaka wa kwanza chuo, unakipa mihela/hela yani kinawaona hadi wenzie takataka kwa kuwa kinaishi maishi tofauti na wao.

  Unadhani unamjenga huyu binti kiakili na kimaisha......ahii mi sijui vizuri lakini kwa kweli uhusiano wa mkaka anayefanya kazi zake huko mtaani na mabinti wa chuo mi siuungi mkono. Mbaya sasa na ninyi kaka zetu ndio mwawekeza humo. Mi sijui.....
   
 5. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu hata mimi nakuunga mkono, kuwekeza kwenye vibinti vya chuo noma. Kwa mtoa mada aelewe kwamba hako kabinti bado hakajakomaa kiakili hivo na kufikiria kiutu uzima na kwa busara kama mdada ambaye ameexperience maisha ya utafutaji na jinsi pesa ilivo ngumu. Yeye anafikiria kiutuuzima wakati kabinti kanawaza kivingine, hamtoendana. Kitakachofuata ni kuumia kwani kitamtafuta pedejee jingine. Mbona wadada wengi tu na wazuri wa umri wako na kazi zao wapo. Hata huku wanajitangaza. Tukua hatua.
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Huyo binti inawezekana hajitambui! Inawezekana vipi mtu unasaidiwa kiasi hiki halafu unamlipa aliyekusaidia matusi, dharau, kejeli na kashfa? Na wasiwasi na msimamo wa huyo binti. Inawezekana rafiki zake hao anaowasimulia huwa wanahongwa hivyo vitu anavyovisema (magari, pesa nk) na mapedeshee wa hapa mjini na kufanyiwa mambo machafu na pengine hata kupewa magonjwa na kujikuta na yeye pia anafikiria ktk level hiyo ya kuhongwa!

  Kitu anachotakiwa kukitambua ni kuwa yeye ni mkeo mtarajiwa na si mpenzi tu wa kupita wa kuishi maisha ya kuhongana bali mtu ambaye mna future naye. Kwa mtu na mchumba wake huwa hakuna kuhongana bali kushirikiana na kusaidiana kwa ajili ya kuboresha maisha yenu ya mbeleni.

  Cha msingi muonye na hilo lililojitokeza na ni vzr kumonitor tabia zake pamoja na hao marafiki zake wa karibu. Ukiona hazibadiliki bado anaendeleza tamaa na dharau achana naye kabla huja-invest sana kwake utapata mwingine. Akibadilika msamehe na kusahau na kuanzisha maisha mapya.

  Pole mkuu. :twitch:
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  mshukuru Muumba wako umegundua tabia yake mapema...
  hao wanaume wanaohonga magari hakuwaona? mbona hawakumpa hiyo ada?

  kak, hilo jini mla fedha achana nae...atakusumbua baadae, mwache akatafute wenye fedha wamuhonge....
  :angry:
   
 8. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kaka achana na hiyo kitu itakupa presha bure inaonekana iko kimaterial zaidi kuliko upendo wa dhati....achana naye fasta, tena ukizingatia si wa posa wala barua, piga chini ndugu.
   
 9. LD

  LD JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mi kwa mtazamo wangu hapa huyu kaka ndio hajajua vizuri aina ya mtu aliyenaye.....yeye anawaza kilometer 7000 mwenzie anawaza mwisho hapo kwenye pua yake...unategemea nini? WE unambebesha akili ambayo hana.....unamtwisha mzigo wa kuanza kufikiria ukosefu wako wa pesa wakati yeye hayuko hivo. Unamkomaza tu wewe.
   
 10. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  hivi mnaosema wanaofanya kazi wawaache wanafunzi hao mnamaana gan? Kwan mtoa mada si kasema huyo ni mwanafunzi wa chuo? Mmeulza umri wa huyo mwanafunzi? hivi chuo hamna wenye ndoa zao?
   
 11. Optic Density

  Optic Density Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Keshapata msomi mwenzake wa kumuoa huyo. Wewe amekugeuza ATM kaka. Kama ulishajitambulisha kwa wazazi wake, unaweza ukawaheshimu wazazi wake kwa kuwapa taarifa za kuachana nae. Pia huyo demu piga chini mapema, akufai, waachie wenye magari wachukue mzigo.
   
 12. d

  demokrasia Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka hata mimi ni msomi, sio kwamba nilikuwa na demu ambaye amenizidi elimu.
   
 13. d

  demokrasia Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka hata mimi ni msomi, sio kwamba nilikuwa na demu ambaye ananizidi elimu.
   
 14. LD

  LD JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Akili yake haiendani na umri ake hata kama ana umri mkubwa wa mika 35. We umeona hayo majibu ni majibu ya kumjibu mtu mwenye malengo na wewe? Khaa yani kabisaaaaaa!!!!
   
 15. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Usiwe kama ile NEC ya CCM na Magamba. Fanya maamuzi mgumu dogo. Piga chini.
   
 16. Optic Density

  Optic Density Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuwa na mpenzi anayesoma chuo yahitaji uvumilivu, Mimi nakumbuka nilipokuwa chuo kulikuwa na wasichana kama 8 ambao walikuwa wanasomeshwa na waume zao wa ndoa. Lakini ni dada mmoja tu mwenye asili ya kiarabu ndiye aliyekuwa mwaminifu. Wengine wote watu walikuwa wanajisevia, ilikuwa tukimaliza group discussion unachukua kipoozeo. Pia ukiwa vizuri kifedha ndio kabisaa unachukua mzigo kilaini. Kuhusu suala lako huyo dada anaonyesha dhahiri anakupenda wewe kwa ajili ya fedha zako, ndio maana hata ukivunja account yako kwa ajili yake yeye hajali. Anaposhindwa kukusaidia wewe unapokwama ndio anapotoa taswira yake halisi kuwa hakufai.
   
 17. S

  Sumu JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 6,225
  Likes Received: 3,204
  Trophy Points: 280
  Kaka pole sana kwa jambo lililokutokea halinatofaiti nalangu..,inaonyesha unampenda sana huyo mpenzi wako na hilo jambo analijua na limefanya akupelekeshe ushauri wangu...
  1.achana naye najua itakuwa ngumu lakini usibishane na ukweli
  2.hakupendi kwasababu hana huruma nawe umemwambia huna umebaki na hela anayoihitaji anakuambia umpe hiyo hiyo alijua utaishije nawe unafanya kazi utakulanini,nauli utapata wapi?huyo ataukifukuzwa kazi hata jisikia vibaya yeye anajiangalia yeye tu!
  3.mtu aliyekupenda kweli hawezi kukuomba hela hata kama anashida sana atakuambia kimafumbo naweutajua kakuomba na hakulazimishi
  4.anamtu anayempenda zaidi yako na hela unayompa naye anaenda kumwonga ampendaye
  5.usijidanganye kuwa ni utoto angekuwa mtoto wazazi wasingekubali jambo hilo litendeke anamaamuzi yake..
   
 18. Nemo

  Nemo JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 661
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 80
  Demokrasia

  Ni kweli unamakosa, you had NO right to go and tell her parents what transpired between you two. If you were legally bound kweli, Kwani ni mkeo huyo? This is nothing but the case of "Cant stand the heat, dont be in the kitchen" :angry:!!!!! So what if umpempa blah blah blah , na kutoa msaada including zeroing your acc?Kama despite all that anakudharau and shouldnt the obvious action be leaving her!?? Unang'ang'anie mwenyewe while huwezi kummudu kifedha, kiushauri wala tabia halafu you want to play the victim,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,urgh~!!!!!!!!!!!!!?
   
 19. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #19
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ni kinyaa kuongelea mee la mtu..

  kweli wewe ni mshamba.. chuo kuna kitu yaitwa three digits.. ushamba wako ndio unaokuzuzua..mbali na mapokezi mtu apatayo chuoni lakini pia aingiapo bwenini hupewa DARSA la three digit..

  1. mwanaume kwa ajili ya kupiga chabo kwenye paper ili ufaulu, lazima awe kipanga flan hivi..
  2. mwanaume ATM, sanasana huyu ni wa mtaani ambapo ukipungukiwa salio unalialia kwake anatapika pesa, maarufu kama mee..
  3. Yule Laazizi hasa..

  sasa weye ni mee wa mtu.. ha ha haaa... pole we!
   
 20. seg

  seg Member

  #20
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana kaka!...mabinti ndivyo walivyo wanajali zaid feeling zao kuliko kingine chochote,..so si ajabu ukamfanyia kila jema malipo yake kutukanywa...unatakiwa kuishi nao kwa akili sana...be tolerant God will pave the way!...:mwaaah::mwaaah::mwaaah:
   
Loading...