:Hivi hili la tigo pesa, airtel money, m-pesa na mengineyo serkali haioni {inflation}? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

:Hivi hili la tigo pesa, airtel money, m-pesa na mengineyo serkali haioni {inflation}?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by commonmwananchi, May 7, 2012.

 1. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,143
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  kuna tatizo la mfumko wa bei sasa hivi nchini kote,tena kwa kiwango cha juu sana.kwa mwananchi wa kawaida kila kukicha ni aheri ya jana.tunalo bunge kubwa kuliko nchi za kenya,uganda,na hata rwanda na zambia ambao kitakwimu wanafanya vizuri kuliko sisi.

  Humo ndani ya bunge tukisomewa majina tuna kila aina ya wasomi,ma-DK,PROF,ENG nk.sasa basi tultegemea kipindi hiki cha anguko la uchumi nchini.mbali na wao kukaa pale kugawana posho na kufukuzana uwaziri ili na wengine wakalie unono, lakini pia wale ambao ni wasomi wazuri na wachache. Nawashauri kama ifuatavyo ili watusaidie kupitia bunge letu ambalo linamermeta pale dodoma,wakati raia tumepauka huku site wafanye hili.

  *Kuna fedha nyingi sana kwa sasa ambayo iko nje ya mzunguko wa mabenki yetu nchini kwa sasa,jambo ambalo linaifanya hata benki kuu ishindwe kudhibiti mzunguko wa fedha nchini.na hili ni jambo ambalo halihitaji ubishi kuliona na kulielewa

  Sasa wakati hali ikiwa hivyo hawa wabunge wetu hakuna anayekuna kichwa ili walau kuja na hoja binafsi bungeni ili serikali ichukuwe hatua ya kudhibiti huu mzunguko usio rasmi kupitia kampuni za simu ambazo kwa sasa zimegeuka kufanya kazi za kibenki bila mfumo rasmi wa udhibiti ili kuhakikisha wanailipa serikali kodi stahiki na kuliongezea taifa kipato kwa faida ya wananchi pia.

  Ni ukweli usiopingika kuwa huduma hizi zimetusaidia sana wananchi wa tanzania ukizingatia kwamba mabenki yetu yamejaa ukiritimba uliokithiri katika utoaji huduma zake na kugeuka kuwa kero kwa wananchi hasa pale unapokuwa na shida muhimu na za haraka kwa watu wa vijijini hii imekuwa kama mkombozi wetu namba moja.

  Lakini nikiwa nimezingatia hilo basi ni vema sasa serikali ingeanza rasmi kama si kufungua kitengo rasmi pale TRA ambacho kitashughulika na hizi kampuni za simu nchini ili kuhakikisha kila promoshheni ambayo inahusika na ukusanyaji pesa kama bahati nasibu za kushindania magari,internet packages na zinginezo zinalipiwa kodi husika ili kuongeza wigo wa kodi nchini na tusikae kulilia nadini tu wakati na hii nayo inazidi madini kwa sababu ni mzunguko wa ndani na ni rahisi kuudhibiti,

  Nina uhakika kuna matokeo chanya yatakayotokea na tusikae tu bungeni kusema michakato inaendelea.....nk,
   
 2. c

  collezione JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  You are a great thinker. Safi
   
 3. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Watanzania bwana hivi hamjui hao ma prof,dr,eng,mr and mrs wamefuata nini?huoni mbatia amemshukuru JK kwa kupewa ulaji bungeni?pambana ki mpango wako nchi imeshauzwa zamani sana!
   
 4. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  ni kweli BOT wanapaswa kuongeza uthibiti kwenye hizi biashara za fedha. Haiwezekani mtu anaweka kiti na meza moja stand ya daladala alafu anafanya transaction za fedha
   
 5. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,143
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Thank you sir!
   
 6. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,143
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Dalili ya nchi yoyote kufilisika huanzia na hatua yaa fedha kuzagaa kwenye sekta isiyo rasmi na mwishowe tunakuwa kama congo DRC na Somalia yaani tunaelekea kuibadilisha sarafu kwa mara ya tatu.na tutafikia mahali tunanua kilo ya nyama kwa fedha ya kujaa rambo plastic bag
   
 7. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,143
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Na huu ndio mpango wangu wa mapambano kwani walau great thinkers tunaweza kuja na kitu cha kuanzia kupata ufumbuzi.hata unapotaka mkopo lazima kwanza uwe na bussines plan yako,.

  Isitoshe ndio maana nimesema tuna bunge kubwa ambalo halitusaidii,na nikasema walau hao wachache wenye kuthubutu na waanzie hapo basi!

  Kuhusu Mbatia ni mtu anayependa labda kukumbatiwa kama jina lake lilivyo na hivyo anapopewa gamba na akakubali kulivaa nafikiri picha yote itakuwa clear muda si mrefu humohumo bungeni na tutaijua nini plan 'C' ya ccm baada ya ile plan 'B'ya CUF kufanya kazi sasa wameanza project vuruga upinzani ndani ya bunge,nafikiri wanaona kama vile wabunge wa NCCR mageuzi wanafanya kazi ya CDM zaidi bungeni,kwahiyo kocha kamuingiza substitute mbatia kutokea benchi, aingie uwanjani akiwa na maelekezo rasmi toka kwa kocha kiranja kwamba nenda kamkabe ZITTO kabla hajatufunga goli la Tatu!

  Alamsik.........
   
 8. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,143
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Yaani utafikiri tuko somaliland vile!
   
Loading...