ELIAS MICHAEL MORRIS
JF-Expert Member
- Sep 26, 2016
- 385
- 298
Habari zenu wanajamvi,
Kuna ndg yangu mmoja (RIP) alipata ajali ya pikipiki mwezi June mwaka jana, aliumia sana kichwani, akapelekwa muhimbil akatibiwa na akaruhusiwa (mwaka jana huo huo) na akashauriwa asitumie vilevi na hata kukaa kwenye vurugu vurugu.
Alikua anafanya shughuli zake kama kawaida ila wiki iliyopita tarehe 5 akazidiwa na tukampeleka Muhimbili tena. Alipofika kule hali ikazid kuwa mbaya tukaambiwa inatakiwa afanyiwe scan. Tukalipia na akafanyiwa, majibu yakaonyesha kuwa ubongo wake umevimba sababu ya ile ajali hivyo mwili hauna mawasiliano kabisa na ubongo na hakuna njia ya kutatua hilo (na kipind hiko alkuwa haongei wala hajitikisi).
Akapelekwa ICU na akawekewa mashine ya kumsaidia kupumua hadi siku Mungu atakayoamua kumchukua. Majuzi tarehe 11 akafariki, sasa tatizo limekuja baada ya kufariki.
Juzi tumeenda muhimbili kufatilia taratibu ya maiti wanatuambia maiti inadaiwa tsh mil 1.5. Sasa sisi tunajiuliza iyo milioni 1 na laki 5 inatoka wapi wakati scan na vipimo vingine vyote tulilipia. Kuna vidawa kidogo navyo tulilipia. Je kulala ICU pekee na ile mashine ya Oxygen pekee kwa siku 5 ndo mil 1.5? Maana huko ICU hakuwekewa hata dripu au dawa yeyote zaid ya hiyo oxygen pekee.
Hadi sasa maiti bado haijachukuliwa sababu ya ukubwa wa hizo gharama. Je wanajamvi wenzangu hii ni sawa? Je muhimbili imebinafsiswa?,
Asanteni na nawasilisha.