Hivi hii tabia wanawake wote mnazo msaada jamani

Pure Scientific

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
716
643
Wakuu habari zenu....
Naombeni msaada kwa hili wakuu hivi inakuaje upo kwenye mahusino na huyo mwanamke uliye naye ana kuwa mtu wa lawama kwako mda wote na pia wewe unaonekana mkosefu kwa kila jambo liwe dogo au kubwa.

Mfano muda wote ana hitaji muwasiliane na usipo onyesha ushirikiano linakuwa kosa kwako na pia yeye kila muda ni lawama tu hata muda mwingine unajiona hauna kosa lolote

wakuu wanawake kwa wanaume ni msaada hii inakuaje
 
Kampe neno!

10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.
11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.
12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
13 Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
14 Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
15 Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
16 Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao.
17 Wala njia ya amani hawakuijua.
18 Kumcha Mungu hakupo machoni pao.
 
Sio wote.. Hiyo shida inakuja kutokana na uwekezaji wa Penzi na Moyo kwa mtu unaempenda kuliko yeye.. Mfano Ktk kisa Chenu yeye kakupenda zaidi.. Mfano Kama Ni ingekua Ni hisa basi yeye kaweka 70% wewe Ni 30%.
 
Tena wanawake wenye gubu/lawama ktkt karne hii ndio wanaongezeka kwa kasi ajabu kama ya mh padlock beer...sio wote baadhi tuu BT asilimia kubwa.
 
Kampe neno!

10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.
11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.
12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
13 Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
14 Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
15 Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
16 Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao.
17 Wala njia ya amani hawakuijua.
18 Kumcha Mungu hakupo machoni pao.

Kwa hii mistari mama mchungaji Evelyn Salt anasubiri.
 
Mkuu ushauri..
Wanawake wapo wengi na kila mmja anamzuri na mapungufu yake..
Lamsingi wewe tafuta yule ambae utaweza kuvumilia vimbwanga vyake, Lakini kila mwanamke anavimbwanga vyake..tena havina Kikomo..
 
Huyo mwanamke aanze kumcha mungu, hilo ni tatizo la kisaikolojia la kushindwa kuappreciate vtu vizuri anavyofanyiwa na kuona vitu hasi. Angekuwa mcha mungu angekuwa anaona mazuri unayomfanyia na maisha yangekuwa mazuri.
 
Ana tatizo la kucomplicate vitu huyo, ana matarajio makubwa mno ambayo baadae atakuja kugundua kuwa ni ndoto tu, mwelimishe polepole atabadilika na mtasonga mbele
 
Mwambie apunguze kuangalia sinema za Mexico - Telemundo and the likes - na kudhani ndio hali halisi ya maisha. Yale ni maigizo tu.
 
Back
Top Bottom