Hivi hii system haiwezi kutumika na Makonda na wengineo?

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Hello JF..

Merry Christmas Everyone.

Wazungu walituwahi wakaweka miundo mbinu mizuri huko chini kwa chini kwa ajili ya choo na floods.

Sasa,hatuwezi kuanza kubomoa na kuanza kujenga hio miundo mbinu na sisi (ingawa inawezakana in the future)

But nimeona kuna hii system sio mpya..ila inaonekana ina trend mitandaoni.

Ni kuchimba mashimo ya choo yasiyojaa

Hivi si neema kwetu watu wa Africa?

Kumbe hatuna haja ya kubomoa miji.

Sasa kama hayajai.

Si Makonda na wengine wangei adopt hizi system kwa kujenga Public Toilets?

Miji gani haina Public Toilets?

Hii topic ningependa kusikia kwenu but more important kutoka kwa ma engineer, is this the way forward?

===
Tsh 2,500,000

Mashimo ya choo yasiyojaa (Bio digester septic system)

Location: Ilala, Kinyerezi Dar Es Salaam

Details
Price negotiable Yes

Condition New

Description
Eco septic Tanzania ni wajenzi wa mashimo ys choo yasiyojaa, yasiyonyonywa, yanayochukua nafasi kidogo, yasiyochagua udongo, yasiyoogopa chemchem wala high water table, yenye garantii ya miaka mitano.

8629DA7C-8988-407B-927B-ECE45CD5EFAE.jpeg
83442504-D659-4ACB-B349-0E764780338F.jpeg
2861AF6F-837F-4137-A780-9A2BA6F529AA.jpeg
BFFC8A7A-F1A7-42D0-9305-60201CB7582F.jpeg

Chanzo: Zoom Tanzania
 
Suluhisho ni kubomoa baadhi ya nyumba ili barabara na mifumo mingine Kama ya maji taka na maji safi ipite bila usumbufu.Hizo aina za vyoo visivojaa haviwezi tatua tatizo. Unafikiri hao wazungu walivoamua jenga miji kimpangilio walifanya hivyo kwasababu ya vyoo tuu?
Fikiria kuhusu ajali za moto, zimamoto zitafikaje eneo lisilo na barabara au hawajui nyumba ilipo? Ukiwa na mgonjwa hasa usiku utawezaje kupata msaada wa ambulance?
Kwahio solution in kubomoa baadhi ya nyumba ili upitishe njia za barabara na mitandao ya maji na pia upate address ya nyumba ili kukiwa na dharura msaada uje kwa haraka
 
Mkuu kama ni address,fire na mambo mengine..sidhani km utahitaji kubomoa 'baadhi' ya nyumba tu..jiji lote limejengwa kiholela...and it is costly kufumua lote na kuanza kujenga upya..labda wafikirie haya yote wanapojenga miji mipya...
sijajua hao wazungu system yao but I think principle ni moja..nayo ni kutojaa ..kufurika..ingependeza kama wanaosoma engineering wangekuja na solution...ya nini tufanye kwa mazingira yaliyopo...
 
Back
Top Bottom