Hivi hii Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na mkuu wa mkoa, hawaoni kweli watu wanavyoteseka na mradi wa mwendokasi wa hovyo kabisa?

Tunzo

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
4,021
2,296
Au ndoo hivyo! Alieshiba hamjui mwenye njaa? Kisa wao wako kwenye viyoyozi na magari yetu, kwa kodi zetu wanapita tu na kutucheka?

Huu mradi umekua wa hovyo kabisa, si siku za kawaida! Kimbembe kukunyesha mvua!
Leo kuna watu wamelipa nauli maeneo ya Fire, kkoo, posta nk kuanzia mchana wamelundikana tu vituoni magari hayapiti

Wamechukua nauli za watu na kuwajaza watu kuanzia mchana namagri hayapiti, mpaka watu wanamua kutoka kwenye vituo na kuacha nauli zao kwenda kutafuta usafiri mwingine!

Kimbembe kama ulikua na 650 tu leo watakesha kwenye vituo, mana magari hakuna.. Thuluma ilioje hii, nahisi huko maofisini wanajichekea tu kua wamelamba mia sita sita za watu na hawaleti magari, na ukitoka kituoni hawakurudishii kajifie mbele.

Wenye ndoa wasameheni wake zenu nanwaume zenu walioko huko mjini mana huko hali ni tete, magari hakuna na watu wengine wameamua kutoka kutafuta magari ya makumbusho kuzunguki kule!

Nyie mwendo kasi endeleni na uhuni wenu tu wa kupokea naili za watu na kutoleta magari, kwanini kama mnaona hamtaleta magari msiwaambie watu, nyie mnapokea tu pesa zao kuanzia mchana mpaka inaelekea saa moja jioni hakina magari.

Watanzania ni wapole ila kuna siku watachoka! Ingekua ni sehemu kadhaa huko nchi za wenzetu wasingekubali huu upuuzi.. mgekuta vibanda vyenu na wahudumu wamebebwa juu juu.

Wito kama serekali ya mkoa imeshindwa kutatua ishu ya mwendo kasi tafadhali Raisi wetu mependwa tatua hili tatizo, wananchi wako wanateseka na mwendo kasi, ndoa zinaharibika huko mitaani, mtu anatoka saa 11 jioni anafika home saa tatu usiku,

Kama Raisi imeweza mandege huko, mareli na mamiradi makubwa sembuse mwendo kasi? Si unatamka tu...

Basi hebu tamka kitu tuone kweli ni wa wanyonge! Achana na hao wanaokula viyoyozi kwenye magari yetu.
 
Waone nini wakati wao kutwa wanapigwa vipupwe
Na kama Kuna foleni wanapita kwenda Barabara ya mwendolasi
Aliyeshiba hawezi muona mwenye njaaaa
Acha tuendeleee kutaabika tu na mradi huu

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakweli kwa sasa DART imechoka na wafanyakazi wamechoka. Wampe mchina aendeshe huo mradi sisi tubaki kupiga kelele tu. Project Management Skills hatuna kabisa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Dr mmoja pale udsm alinifundisha topic moja ya" public policy" nakumbuka siku moja pale class alichambua vizuri sana namna ya kutatua shida ya usafiri hapa daslam. Leo hii ana mwaka wa 3 ameteuliwa kuwa katibu mkuu kwenye wizara fulani yupo kimyaa .sasa najiuliza kwenye hiyo steering committee ya Baraza la mawaziri anafanya kazi gazi kutatua tatizo la usafiri hapa dar
 
Ni yule koti la mkumbo nini?
 
Kanyamazishwa
 
Au ndoo hivyo! Alieshiba hamjui mwenye njaa? Kisa wao wako kwenye viyoyozi na magari yetu, kwa kodi zetu wanapita tu na kutucheka?

Huu mradi umekua wa hovyo kabisa, si siku za kawaida! Kimbembe kukunyesha mvua!
Leo kuna watu wamelipa nauli maeneo ya Fire, kkoo, posta nk kuanzia mchana wamelundikana tu vituoni magari hayapiti
Kwa kweli huu mradi umegeuka kuwa kero tofauti namatarajio yetu wasaka tonge wengi. Kuna siku unakaa hata saa moja na nusu ndio unapata gari kitu ambacho ni ujinga kwa sababu unapoteza muda. Inafika wakati tunatamani hata wangeruhusu daladala. Wanaudhi kweli hawa UDART. Kama vipi wapewe private sector waendeshe tu serikali ipate kodi na wananchi wapate ajira maisha yaendelee
 
Kuna Dr mmoja pale udsm alinifundisha topic moja ya" public policy" nakumbuka siku moja pale class alichambua vizuri sana namna ya kutatua shida ya usafiri hapa daslam. Leo hii ana mwaka wa 3 ameteuliwa kuwa katibu mkuu kwenye wizara fulani yupo kimyaa .sasa najiuliza kwenye hiyo steering committee ya Baraza la mawaziri anafanya kazi gazi kutatua tatizo la usafiri hapa dar
hahahahahahaaa . . . . kama namuona vile huyo Dkt. Ukiitafakari sana hii kero ya usafiri Dar es Salaam utasikitika tu kwa jinsi tunavyominyana kwenye magari na mwendokasi. Inauma sana kuona mtu kama huyo tena kasoma kwa kiwango cha juu kakaa kimya na solution anayo tena pengine ndiyo njia muafaka
 
Wakishapata vyeo wanajisahau. Dr.ndumbaro huyo nasikia ni katibu wa wizara ya utumishi wa umma.
 
Usiombe uwe umetoka mkoani, ukajisahau kufanya shoping, uende huko kariakoo siku moja kabla ya sherehe yoyote kubwa, mfano mwaka mpya, utajuta.
 
Tatizo hapo ni monopoly right waliyonayo ndio inayowalevya. Wangeruhusu mfanyabiashara binafsi aka-operate mabasi yake 50 kama hayo ya mwendokasi katika njia hizo hizo hapo ndio wangejifunza jambo.
Dala dala zilipoanza miaka hiyo iliwafanya UDA wafunge virago na hawa wakati wao wa kufunga virago umefika.
We have to send them parking otherwise it will be the same story over and over again.
 
Back
Top Bottom