The Hidden
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 246
- 101
Nimepata ramani ya nyumba ya kuishi, yenye vyumba 4( kimoja kati ya hivyo ni self contained), sitting room, dinning room, jiko,choo na bafu(public) ukubwa wa nyumba ni 107.5 sq m lakini naangalia humu jf mijadala mingi kuhusu ujenzi inaonesha kama sq meter za hii ramani yangu ni ndogo sana kulinganisha na idadi ya vyumba.Wakuu, kwa aliye na utaalamu juu ya ujenzi, naomba nifahamisheni kama inawezekana kwa huo ukubwa wa nyumba ikawa na sq m 108 au mchoraji wangu wa ramani kanidanganya?