Jana Ulirudi Usiku
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 2,362
- 2,261
Ninatafakari sana.
Pombe ni dhambi na kulewa ni dhambi, leo makanisa ya kiroho yanapiga vita unywaji wa pombe wakisema ni dhambi, wakitoa maandiko ya kukazia(bold) hili jambo. Ila wakati huo huo Yesu alikiri na kusema,
"Yohana hakula wala hakunywa, ila alikula nzige na asali, wakasema ana pepo huyu, ila mimi nakunywa nao wananiita mlevi, nakula, nao wananiita mlafi".
Maandiko hayo yanadhihirisha Yesu alikuwa akinywa mvinyo/divai/kilevi, sasa hii ya kusema kunywa pombe ni dhambi imetoka wapi? Nani muasisi wa hili? Tuwekeni wazi raia tupo njia panda.
Pia, agano la kale ni agano na Mungu na Waisrael pekee, bali agano jipya ni la Mungu na wanadamu wote watakaoliitia jina la Yesu na kuliamini. Sasa, hii inamaanisha walioamini agano jipya(jina la Yesu) hawafungwi tena na sheria za agano la kale ambalo limeipa nguvu torati(torah) na sheria zake.
Kama ndivyo, kwa nini basi bado makanisa yanadai zaka(fungu la 10) kwa waumini na kusema ni lazima? Je, ni wizi au hawajatambua kuwa agano la kale na sheria zake halitumiki tena baada ya ujio wa Yesu na kufufuka kwake katika wafu?
Kitabu cha Malachi ambacho ni cha mwisho kama sikosei kwenye agano la kale, kinawaambia WANA WA ISRA'IL kuwa wanamuibia BWANA kwa kutotoa fungu la kumi. Kimsingi walioamini agano jipya hawana nafasi katika agano kati ya Mungu na Wayahudi na vitabu vyake vyote ikiwemo sheria zake zote za torati. Je, watu waachwe au waendelee kulazimishwa na kutishiwa kutoa zaka kinguvu?
Naomba nieleweshwe kwenye haya tafadhalini.
Sent from my A50s using JamiiForums mobile app[/I]