wanawake tunaonewa mabaya yetu yanaonekana ya wanaume hata....
Mnaonewa hata kwa yasiyo mabaya. Hebu ona huyu dada walivyomtendea huko Nairobi kisa vazi alilokuwa amevaa (ambalo halikuwa na ubaya wowote ule na hata kama lingekuwa baya hakustahili kabisa kutendewa hivyo)
Ulikwishawahi kusikia BOSI kachelewa kazini? Siku zote utaambiwa kabosi hakajafika. Sisi ni mabosi kwenye haya mambo yetu ya kikubwa, ingawaje vitoto navyo siku hizi vimovimo. Hapo hatuna jina, na hata ukitupa jina jamii halilikubali.
Mmmmh!!!!!!! na Mungu awalaani hao watu,,,,, huwa najiuliza ivi ni kosa kuzaliwa mwanamke???
Ni kwa namna gani umekuwepo?
Mnaonewa hata kwa yasiyo mabaya. Hebu ona huyu dada walivyomtendea huko Nairobi kisa vazi alilokuwa amevaa (ambalo halikuwa na ubaya wowote ule na hata kama lingekuwa baya hakustahili kabisa kutendewa hivyo)
Well, kwa jinsi mnavyotendewa huko Afrika inaonekana kama vile ni kosa kuwa mwanamke.
Mbaya zaidi unapokuta wanawake wanaounga mkono hayo manyanyaso.
Hapo ndo kabisa unabaki mdomo wazi na kuanza kuamini labda huenda kweli ikawa ni kosa kuzaliwa ukiwa mwanamke Afrika.
Hili tukio linafanana na tukio moja ambalo lilitokea hivi karibuni hapa Nyakato
Kuna dada mmoja ambae alikuwa amevalia sketi yake ambayo iliishia juu ya magoti,wapiga debe wa kituo cha Hiace cha Nationa walianza mayowe na walimvua yule dada,nilipofika kwenye tukio nilikuta ndio wanaanza kumvua,sikupenda kabisa tukio lile ....
Nilipotazama wale ambao walikuwa wanamvua walikuwa wamevalia suruali zao chini ya makalio yao na wengine wamevaa viatu oversize niliishia kusikitika tu ...
Ilibidi niondoke kwa hasira kwasababu wanaoadhibu nao wanafanya upuuzi ule ule na sijui kwanza hayo mamlaka wameyatolea wapi ya kuwadhalilisha watu namna ile
Hata kama alikuwa amekosea kweli hiyo ndio namna nzuri ya kumuadhibu mtu?
Ni hivi, hata kama mdada kavaa sidiria na shemizi tu na akapita mtaani, hakuna mtu mwenye haki ya kumfuata na kuanza kumchania hiyo sidiria yake na hiyo shemizi yake.
Na mara nyingi (kwa yale matukio niliyoyaona mimi) wale ambao huchaniwa nguo zao wala huwa hawajavaa vibaya hata kidogo. Sasa kwa mfano hiyo sketi iliyoishia juu ya magoti ina ubaya gani?
Huo ni uhuni, upumbavu, ujinga, na kwa maoni yangu ni jinai pia.
Hebu fikiria kila mtu akiamua kujipa mamlaka ya kuamua ni mavazi yepi yanafaa kuvaliwa na watu wakiwa barabarani. Patakalika kweli?
Sijui hao wahuni wanataka tuvae kama wavaavyo huko Afghanistan?
Inasikitisha sana kuona jamii ikilea na kuendekeza hayo matendo ya kihalifu. Ningekuwa na mamlaka ya kutekeleza sheria ningekomesha kabisa hiyo tabia ya kuvua watu nguo hadharani.