Hivi hawa matapeli wa kwenye mitandao wanakamatwa na kupewa adhabu kweli?

Karot

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
1,159
1,309
Habari za majukumu wakubwa na wadogo. Poleni na kazi na wale waliofunga kama mimi Mungu atusamehe tulipokosea ndani ya mwezi huu. Niende moja kwa moja kwenye mada.

Iko hivi kila siku tunasikia kuna matapeli wa mitandaoni ambao wanajihusisha na wizi fedha kwa udanganyifu... Sasa nakua nikisikia kwamba serikali imewakamata wezi hao na huku wakiendelea kuwasaka wengine ili kukomesha tatizo hili.

Sasa napata maswali. Je hawa wengine ambao bado wanaendelea na mchakato wao wanakua serikali haiwapati ama inakuwaje?

Au wale waliokamatwa wanakua wanaachiwa na polisi baada ya hapo wanakuja tena kufanya kazi zao?
 
Kuna mmoja Arusha alilipa hadi polisi wa kituo wakavunja paa usiku na kuingia ndani na kuiba laptop yake kupoteza ushahidi. Na alishinda kesi. Alikuwa tapeli mzoefu mtandaoni na kuliza wengi.
 
Back
Top Bottom