Hivi hata bustani zimetushinda?

Hivi hata bustani zimetushinda?

Ok sawa sawa
hapo hapo mzee ..palikuwa pazuri sana ... Ajabu mamlaka husika ikawa inawaacha wahuni wawe wanashinda tu pale .. wakicheza korokoro ...sehemu ya kivutio cha utalii wa ndani kikawa kina tumika ndivyo sivyo mpaka leo kimekufa
 
Aisee inasikitisha sana,mi nilidhani maeneo ndio hayakutengwa kumbe yapo wakayatelekeza!
Yapo mengi mnoo tu .. wameishia kuyaua "... kuna sehemu inaitwa kinondoni garden .. napo palikuwa na garden pia but now limebaki jina tu
 
Taarifa ya BBC pia imeeleza kama nilivyoweka link hapo.
Ni ukweli usiopingika huwezi kuifananisha Dar na miji mingine mikubwa ya East Africa kama Nairobi kwa mpangilio wake hasa kwenye bustani za wazi watu kupumzika katikati ya jiji. Hii inaifanya Dar ionekane kama kichochoro ikizidiwa hata na Tanga, Arusha na hata Sumbawanga (bustani ya mandela).
Cha ajabu kampeni za ajabuajabu tu ndio utaziskia mara tezi,dume mara ushoga, mara makahaba. Yaani kampeni zote zinalenga kwa vitu visivyo na tija utasema viongozi wetu hawafikirii au hawajawahi kutembea nje ya mipaka yetu. Kuna haja sasa kufanya kitu kwenye hili maana hata bustani zilizopo zilishatelekezwa na hazitumiki kwa makusudi hayo. Kwa washauri wa yule jamaa mzee wa kampeni wampe na hii kama kweli anataka kuacha legacy hapa mujini.


Kwa nini watanzania hawapendelei kukaa katika bustani za wazi?
Tanga imeiacha Dar kwa baadhi ya vitu kama sehem za kupumzika na pia hydrants tanga inazo zaidi ya 360,uliza hapa zipo ngapi!
 
Tanga imeiacha Dar kwa baadhi ya vitu kama sehem za kupumzika na pia hydrants tanga inazo zaidi ya 360,uliza hapa zipo ngapi!
Ni kweli mkuu kwa hapa bongo Tanga inaongoza kwa bustani za kupumzikia. Hizo hydrants ni nini unamaanisha?
 
hapo hapo mzee ..palikuwa pazuri sana ... Ajabu mamlaka husika ikawa inawaacha wahuni wawe wanashinda tu pale .. wakicheza korokoro ...sehemu ya kivutio cha utalii wa ndani kikawa kina tumika ndivyo sivyo mpaka leo kimekufa
Mkuu umenikumbusha mbali sana hiyo korokoro hahahahaaaaaaa
 
Ni kweli mkuu kwa hapa bongo Tanga inaongoza kwa bustani za kupumzikia. Hizo hydrants ni nini unamaanisha?
Mabomba ya maji Fire Brigade wakija wanaunganisha na magari yao kuzima moto. Ndio maana siku hizi utasikia Fire engine imeishiwa maji kwa sababu hamna hydrants.

Nakumbuka moja ilikuwa pale Upanga karibu na Takukuru. Nyingine ipo pale Jangid Plaza mataa ya St Peter's.
 
Ni kweli mkuu kwa hapa bongo Tanga inaongoza kwa bustani za kupumzikia. Hizo hydrants ni nini unamaanisha?

Hizo ni water points kwa ajili ya dharura kama majanga ya moto,usafi au hata maji kwa matumizi, yaani kama fire wamefika eneo husika na maji yakawaishia basi wanachukua mpira wao (horse pipe )wanachomeka katika hizo hydrant na zinakuwa zimejazwa maji tayar
 
Ile bustani iliyopo pale posta ya zamani " Aisee watu wananyonyana sana ndimi usiku ''' ukikaa peke yako pale lazima ujihisi upweke

nikirejea kwenye mada " mkuu usemacho ni kweli kabisa bustani nyingi mnoo zilizopo awali kwa sasa zimeshakufa mfano hai upo pale magomeni " "... palikuwa na bustani nzuri sana miaka ya nyuma watu walikuwa wanapumzika pale " kabla ya kuvamiwa na wahuni waliokuwa wanashinda pale na kuipoteza mvuto wake " na mpaka mamlaka husika hivi sasa wameamua kuiua kabisa " na hivyo sasa haipo tena kama ilivyokuwa awali
Bustani ni nzuri sana kwa maisha ya mjini.Nilikuwaga najibebea kakitabu naenda pale posta ya zamani natulia nasoma siku za wikiendi.
Mwanza wamejitahidi kidogo, ukipita wikiendi town unakuta watu wametulia kwenye majani wanapiga stori, sijui bado zipo zile bistani?. Huyo makonda angepambana na kurejesha hizo bustani angekuwa kafanya jambo la maana sana kuliko kutafuta mashoga.
 
Dar bado sana.
Labda JPM na Lukuvi watoe agizo kwa kila manispaa kuwa na bustani mbili au tatu.
Bila hivyo jiji litaendelea kuboa tu.
 
Bustani ni nzuri sana kwa maisha ya mjini.Nilikuwaga najibebea kakitabu naenda pale posta ya zamani natulia nasoma siku za wikiendi.
Mwanza wamejitahidi kidogo, ukipita wikiendi town unakuta watu wametulia kwenye majani wanapiga stori, sijui bado zipo zile bistani?. Huyo makonda angepambana na kurejesha hizo bustani angekuwa kafanya jambo la maana sana kuliko kutafuta mashoga.
Aghh huyo jamaa ni 0 brain hamna kitu pale
 
Taarifa ya BBC pia imeeleza kama nilivyoweka link hapo.

Ni ukweli usiopingika huwezi kuifananisha Dar na miji mingine mikubwa ya East Africa kama Nairobi kwa mpangilio wake hasa kwenye bustani za wazi watu kupumzika katikati ya jiji. Hii inaifanya Dar ionekane kama kichochoro ikizidiwa hata na Tanga, Arusha na hata Sumbawanga (bustani ya mandela).

Cha ajabu kampeni za ajabuajabu tu ndio utaziskia mara tezi dume mara ushoga mara makahaba. Yaani kampeni zote zinalenga kwa vitu visivyo na tija utasema viongozi wetu hawafikirii au hawajawahi kutembea nje ya mipaka yetu.

Kuna haja sasa kufanya kitu kwenye hili maana hata bustani zilizopo zilishatelekezwa na hazitumiki kwa makusudi hayo.

Kwa washauri wa yule jamaa mzee wa kampeni wampe na hii kama kweli anataka kuacha legacy hapa mujini.


Kwa nini watanzania hawapendelei kukaa katika bustani za wazi?
hizo kampeni unazoona hazina tija ndio zinawapa kiki wezako, we baki kuona hazina tija tu, ilhali wezio ndio backbone yao ya kutrendia mitandaoni na mitaani, bustani ka muhimu sana tafuteni visa mzitembelee za ulaya
 
Back
Top Bottom