Hivi Dubai ni rahisi sana kuijengae?!

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,310
12,972
Mimi sijawahi kufika Dubai na wala sijui kukoje. Lakini nimewasikia viongozi wakubwa wanasiasa katika ngazi ya urais mara kwa mara wakiahidi kuzijenga sehemu fulani za Tanzania kuwa kDubai. JK wakati wa kampeni zake wakati huo akigombea mara ya pili alisema ataibadili Tanga kuwa Dubai na pia nilimsikia akisema hata Kigoma ataifanya kuwa Dubai. Sijafika Tanga na Kigoma kuona jinsi zilivyokuwa sasa ni Dubai. Wenyeji wa huko wanaofurahi maisha ya Dubai sasa watatujuza raha wanazozipata.

Hivi karibuni nimemsikia pia rais wa jeecha naye akiahidi kuvifanya visiwa vile kuwa Dubai. Ninacho jiuliza ni kuwa hivi wanasiasa wa Tanzania wanaifahamu Dubai tu au na sehemu nyingine za Dunia? Hivi Dubai ni sehemu iliyoendelea sana kuliko sehemu nyingine duniani au ni rahisi sana kuijenga? Mbona sijawasikia wakisema wataifanya sehemu fulani ya Tanzania kuwa New Yorik, Woshngton, London, Paris, Tokyo au hata Pretoria Afrika ya Kusini au hata pengine Nairobi?! Mimi nawaomba watembelee na miji hiyo niliyoitaja ili angalau wasifanye nchi yote kuwa Dubai wajaribu kutofautisha ili sehemu nyingine ziwe Tokyo, Paris, London, nk
 
Wanaota hao Ndoto za Mchana kweupeeee....!!
KUJENGA siyo kuahidi au kutamka maneno hadharani.... Aliyo ijenga DUBAI hata siku moja hakupanda juu ya jukwaa na kupayuka maneno au kutoa ahadi feki!!

Maneno hayajengi nchi...................................................................... !!
 
Hayo maneno utayasikia kwa makada Wa ccm tu siyo sehemu kwingine jk Ana msemo wake chakuambiwa changanya na zako
 
Jiulize walioijenga hiyo Dubai sijui walikuwa wanataka ifanane na wapi!? Tatizo letu ni ulimbukeni na kutokuwa na vision binafsi kinachopelekea mtu mmoja na familia yake kuiba pesa zote za wizara zaidi ya nne (billion 60 za sare) kisa eti afanane na mzungu kitu kisicho wezekana.
 
Back
Top Bottom