Hivi 'chopa' ya CHADEMA inatumika Arusha na Moshi pekee?

Mbona hizo hisia zako uzionyeshi na kwa CHADEMA na kitendo walicho mfanyia kada wa CCM, Tesha, cha kumlowanisha na tindikali usoni na maeneo mbalimbali ya mwili?

Kama kweli wewe una utu basi ingekuwa ni vyema ukajumuika nasi katika kuiponda mawe CHADEMA kwa vitendo vyake vya kigaidi vya kumwagia raia wa Tanzania tindikali tena kisa mambo ya kiitikadi tu.
Mkuu kesi imeshapelekwa Mahakamani,nadhani mbaka sasa unajua kinachoendelea!Mwisho wa siku mahakama itatamka wazi yule Tesha alimwagiwa tindikali na nani!huu ndiyo utawala wa sheria!kama umejifua ufahamu basi endelea kutukuza ujinga!
 
WanaJF!

Ni imani yangu tuna tambua kuwa Tanzania yetu ni moja na watanzania wote ni wamoja katika mambo yote yanayohusu taifa letu, ikiwemo mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, na wote kama watanzania tuna stahiki kupata mambo haya kwa usawa.

Katika hali kama hiyo ya kupata hayo mambo kwa usawa, nasikitika kusema kuna kundi fulani la watu aidha hawapo tayari kutoa usawa huo ama hawajui kuwa ndio tamaduni na desturi yetu watanzania kushiriki kwa usawa kwenye mambo tajwa hapo juu.

Katika kulisisitiza hili, ningependa tutizame siasa za CHADEMA, hivi karibuni umefanyika uchaguzi wa madiwani kwenye zile kata ambazo madiwani wake aidha walitimuliwa ama walifariki hivyo kata kubaki wazi, katika chaguzi zile CHADEMA walifanya ubaguzi mkubwa mno.

Kata zilizo kuwana uchaguzi zilikuwa maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwemo Mbeya, Morogoro, Mara na Manyara, lakini 'CHOPA' ya CHADEMA ilipaa Arusha tu na wala haikuchungulia sehemu nyingine yoyote hapa nchini.

Aidha, huko Arusha 'CHOPA' ya CHADEMA ilikuwa busy kwenye kata zote, yani haikuwahi kutokea kampeni zifanywe bila matumizi ya 'CHOPA' hiyo kwa kipindi chote cha uchaguzi wa kata za pale Arusha.

Kama hiyo haitoshi, hivi sasa kamanda wa anga, bwana Mbowe, yupo Hai kama mbunge wa jimbo hilo, lakini kwa ubabe wake amehamua atumie 'CHOPA' hiyo kufanya shughuli zake zote, yani kama mbunge na pia mwenyekiti wa chama.

Kwa kufanywa hivyo inakuwa sio sawa, kama itakuwa hivyo basi na majimbo mengine nayo yapelekewa 'CHOPA' ya CHADEMA na isibaki Arusha na Moshi pekee, kwani ikiendelea hivyo itatafsiriwa kuwa CHADEMA ni chama cha ukanda.

thread zako zote ni chadema tu,inaonesha namna gani chadema inavyowanyima raha,mtatoka sana mapovu makamba,huo ni mwanzo muziki wenyewe 2015,gamba mkubwa!
 
Mkuu Ritz,

Ndio nimegundua aisee, ukanda utawateketeza CHADEMA!
Tukisema ukweli kuhusu ukanda wa Chadema nyuzi zangu zinafutwa.

Labda nikuulize swali kiduchu.

Umeishawahi kuiona Chopa ya Chadema imekwenda Ukerewe, Tarime, Mwanza Mjini. Musoma au Bukoba kwa kina Lwakatare?
 
Last edited by a moderator:
Mbona hizo hisia zako uzionyeshi na kwa CHADEMA na kitendo walicho mfanyia kada wa CCM, Tesha, cha kumlowanisha na tindikali usoni na maeneo mbalimbali ya mwili?

Kama kweli wewe una utu basi ingekuwa ni vyema ukajumuika nasi katika kuiponda mawe CHADEMA kwa vitendo vyake vya kigaidi vya kumwagia raia wa Tanzania tindikali tena kisa mambo ya kiitikadi tu.

Utapata vidonda tumbo buree. Hoja zako zinateleza kama udenda tu! Umeacha chopa umehamia tindikali... Hujitambui kabisaa, nakuona kama aina fulani ya Allien limefungiwa ground floor pale lumumba kwa kazi 1 tu ya kipuudhi. Hupati wanachama kwa staili hiyo
 
Tunafuga paka si kwasababu haibi chochote sometimes utakuta kala mboga, lakini vile ni mbaya zaidi kuishi na panya tena panya waharibifu wa kila sekta-utamaduni wameharibu, elimu wameharibu, madini wameharibu, uongozi wameharibu leo tunatukanwa kila kona na majirani, uchumi kutoka 4% hadi 19.2% mfumko wa bei huo, kodi zinapanda mshahara inakuwa duni, ubaguzi na udini, wizi na ufsadi yapo mengi tu, ndo maana tunamudu gharama za paka ili kuwaondosha panya na ukoo wake. Tutachangia helikopta kila siku ipasue anga.

Apo umejibu hoja au umeandika ulichokipenda au ndovile tena ushuzi wa wazazi haunuki
 
Na Tundu Lissu, akijichanganya tu kwenda Zanzibar lazima wamshushe mshipa.


Ah na wewe mfanyabiashara umejitokea? Kununua Chopa hauwezi unakuwa muuaji wa watanzania woote unataka uwafanye machizi kwa tamaa yako ya pesa,

Hebu wahurumie wanadamu wewe ibilisi,sheitwani mkubwa
 
Aende kufanya nini nchi iliyojaa magaidi na wachawi wanaojifanya wachamungu kumbe ni wahuni tu!
Sasa na yule kiongozi wa Chadema Zanzibar anayetembea na Dr Slaa na Mbowe mtamfukuza lini?
 
Ah na wewe mfanyabiashara umejitokea? Kununua Chopa hauwezi unakuwa muuaji wa watanzania woote unataka uwafanye machizi kwa tamaa yako ya pesa,

Hebu wahurumie wanadamu wewe ibilisi,sheitwani mkubwa
Kamanda jenga hoja kwa nini lakini Bavicha mnapenda kutukana.
 
Sinahakika km HAMY-D ni mzalendo, anakataa ukweli kwa kuukumbatia uongo zipo takriban Kanda 7 (Pwani,Nyanda za Juu na kati, Ziwa, Magharibi, Mashariki, Kusini na Kaskazini)

Hospitali za rufaa ziko ngapi na wapi? Viwanja vya ndege vya kimataifa vingapi na viko wapi, viwanda vya saruji viko wapi na vingapi, Gridi ya Umeme kitaifa iko wapi .... ! nimetaja maeneo haya machache ili kuonyesha jinsi ambavyo Ujimbo unaoukataa kwa kuutolea mfano wa CHOPA ni sawa na UJIMBO wa maeneo hayo tajwa? Viwanda na Umeme ni maeneo yanayohitajika kumwendeleza Mtanzania ... Leo umeona CHOPA ndiyo msingi wa maendeleo? Je ikitokea kweli CDM wameweza kuwa na CHOPA kila mahali Tanzania inamaana sawa na kutokuwa na Ujimbo? Au kukosekana kwa CHOPA Mwanza na kwingineko kumewapunguzia nini wananchi wa Mwanza?

Mkuu,

Usiwe na shaka kuhusu uzalendo wangu, kwenye hilo na uzalendo niamini.

Hoja yako umeijenga kutaifa zaidi, ingawa huu mjadala umelenga kuzunguzumzia vyama, ila nitajaribu kukujibu kama ifuatavyo;

Hospitali ya rufaa sio kama dispensari mkuu. kumbuka tunazo za kada, wilaya mpaka za mikoa, na kuna za kanda, sasa rufaa inakuja pale tu mgonjwa anapohitaji huduma zaidi ambayo haipatikana huko kwingine, jambo la msingi hapa ni serikali kuboresha hizo hizo zilizopo, na kuitanua miundombinu ya Muhimbili ili iweze kuhudumia zaidi wale wenye mahitaji ya rufaa. Hizi za rufaa kwa sasa serikali haiwezi kujenga kwenye kila kanda, ila tutafika huko.

kuhusu grid ya taifa, hii hata ingekuwa Mtwara, jambo la msingi ni miundombinu ijengwe ili kuweza kufikia maeneo mengi ya nchi, mechanism ya grid ya taifa ni kupokea umeme kutoka kwa wazalishaji na kuusambaza kwa taifa, hivyo jambo la msingi ni kupata vyazo vipya vya uzalishaji umeme (tunayo gesi tayari na upepo unafanyiwa upembuzi yakinifu) ili wananchi wengi waweze kufaidika na nishati hii ambayo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo.

Serikali haiendeshwi kimajimbo mkuu.
 
Kamanda jenga hoja kwa nini lakini Bavicha mnapenda kutukana.



Tusi liko wapi hapo? Kusema Ibilisi na Sheitwani? Sio tusi ni sifa ya kile ulichoamua kukifanya,kwani unaelewa kabisa kwamba unachokifanya kibaya kwa kizazi hiki lakini kwa kuwa umeamua kuifanya biashara ukiambiwa ukweli unaona unatukanwa

Ukweli ni lazima usemwe hata kama ni mchungu ,na sio kila mtakaepishana nae mtizamo ni Bavicha,ni kutaka kuweka mambo sawa kwani watu wengine ukweli wanaufahamu lakini kwa makusudi wanajifanya vipofu na viziwi,kuendelea kuwa na watu aina hii watapelekea kizazi chote kuwa cha majuha
 
Tukisema ukweli kuhusu ukanda wa Chadema nyuzi zangu zinafutwa.

Labda nikuulize swali kiduchu.

Umeishawahi kuiona Chopa ya Chadema imekwenda Ukerewe, Tarime, Mwanza Mjini. Musoma au Bukoba kwa kina



Lwakatare?



kwa taarifa yako ukerewe na mwanza walishajikomboa kutoka kwa chama cha wauza unga (CCM) halimashauri ya ukerewe hiko chini ya chadema,ccm ukerewe nzima ina madiwan watatu tu,toka dk slaa amwambie yule mama jambazi getrude mongera, wananchi wa ukerewe walimuelewa dr slaa ,na wakasema hapana kwa ccm
 
Tusi liko wapi hapo? Kusema Ibilisi na Sheitwani? Sio tusi ni sifa ya kile ulichoamua kukifanya,kwani unaelewa kabisa kwamba unachokifanya kibaya kwa kizazi hiki lakini kwa kuwa umeamua kuifanya biashara ukiambiwa ukweli unaona unatukanwa

Ukweli ni lazima usemwe hata kama ni mchungu ,na sio kila mtakaepishana nae mtizamo ni Bavicha,ni kutaka kuweka mambo sawa kwani watu wengine ukweli wanaufahamu lakini kwa makusudi wanajifanya vipofu na viziwi,kuendelea kuwa na watu aina hii watapelekea kizazi chote kuwa cha majuha
Bavicha sounds...
 
Back
Top Bottom