Hivi CCM wanaiteteaje TANESCO?

Hivi CCM wanaiteteaje TANESCO?

CHENGU MANURE

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2015
Posts
914
Reaction score
566
Nimemsikiliza kinana na mgombea wa chama hichowote wanalalamikia TANESCO, Serikali inailalamikia TANESCO.

Lowassa anailalamikia TANESCO, hivi hawa jamaa inamaanisha maelezo yao hayakueleweka pote kwa wananchi na wanasiasa.

Mbona wanaonewa aibu, wapo kama wanatoka nchi za nje na hakuna humu nchini wa kuhitaji ufafanizi wao.

Mimi sikuelewa kama gesi ni 305mw umeme unakuwa historia. vyazo vilivyopo leo bila gesi ya mtwara vyote jumla ni zaidi ya 1100mw lakini umeme haujawahi kuwa wakutegemewa.

Kweli mbele kwa mbele.
 
Tanesco ni ishara kamili ya kushindwa kwa CCM kuwatatulia Watanzania kero zao kwa muda wote. Nakumbuka tatizo la kwanza alilolikuta Kikwete miaka 10 iliyopita lilikuwa Umeme. Kikwete baada ya miaka 10 anaondoka akiiacha nchi katika mgawo wa umeme.CCM imeshindwa na sasa ni lazima kila mwananchi aitose 25/10 kwa kukipigia Chadema kura!
 
Matatizo ya mgao wa umeme yamekuwa ya muda mrefu sasa na Serikali ya CCM ndio chanzo cha matatizo hayo. Sio rahisi kwa CCM kumaliza mgao wa umeme kwani uwezo wao kufikiri umefika mwisho, "pumzi imekata" .

Wakati umefika wa kufanya MABADILIKO ili Tanzania ipate japo MAENDELEO kwa kila Mtanzania kuliko sasa maendeleo ni kwa tabaka la viongozi na familia zao.
 
Kinana na Magufuli nao wanailalamikia TANESCO majukwaani utafikiri nao ni wapinzani. Wametugeuza wapumbavu na malofa.

Kisu chao nimewawekea kwenye makoo yao. Nasubiria 0ct 25.
 
CCM wanatusanifu, jana wanadanganya umeme hautakatika lakini sasa hivi wameondoka Arusha umeme umekatika, tangu CCM ianze campaign hapa Arusha umeme ulikuepo kumbe ni kuwadanganya Watanzania, kweli tatizo la umeme linasababishwa na CCM.

Watanzania tutafanya makosa makubwa sana kama tutaichagua CCM, hii ni kama ile ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania 2005. Hata ajira, viwanda CCM inavyoahidi haiwezi kuwapatia watz, Tuchague vyama vingine lakini sio CCM.
 
Hata wao ccm wanajua wana wahadaa wananchi ila kwasababu ya ujinga wa Watz na kupenda kudanganywa
 
mnao afiki semeni ndiyo,,,,,,,,
Ndiyoooooooooooooooooooooo.
Basi hoja imeungwa mkono.
 
Matatizo ya mgao wa umeme yamekuwa ya muda mrefu sasa na Serikali ya CCM ndio chanzo cha matatizo hayo. Sio rahisi kwa CCM kumaliza mgao wa umeme kwani uwezo wao kufikiri umefika mwisho, "pumzi imekata" .

Wakati umefika wa kufanya MABADILIKO ili Tanzania ipate japo MAENDELEO kwa kila Mtanzania kuliko sasa maendeleo ni kwa tabaka la viongozi na familia zao.

Hii ni disqualification kwa CCM kwani, kila kukicha wanakuja na visingizio vipya. wamesema hadi tar 20 October, lakini kwa nijuavyo, itafika tarehe hiyo watakuja na propaganda mpya, cha nsingi tuitoe serikali ya ccm kwa sababu kwenye hili shirika ndo imekuwa kwa sehemu kubwa ndio mtaji wa ufisadi kwa kuchukua hela za uma. Rejea tashiti kama, ESCROW, RICHMOND, DOWANS na etc
 
..kwa kauli za katibu mkuu wa CCM na mgombea urais wa CCM maana yake CCM inakili watendaji katika wizara ya nishati na wa Tanesco ni wazembe na hawafai. Ikiwa rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM ndiye aliyewateua watendaji hao, kwanini asiwabadilishe ili kuondoa tatizo la umeme na aweze kikiongezea Imani chama chake? Badala yake eti tusubiri hadi Magufuri achaguliwe ndiyo wawajibishwe. Kweli hii ni hujuma dhidi ya Magufuri, mgao huu unai-cost CCM, labda tu tushukuru watanzania wengi hatuna utashi wa kujua jema na baya (zero IQ) na ni wepesi kusahau.
 
Magufuli anaendelea KUSHANGAA.
Leo anashangaa umeme kuisha Tanesco😅
 
..kwa kauli za katibu mkuu wa CCM na mgombea urais wa CCM maana yake CCM inakili watendaji katika wizara ya nishati na wa Tanesco ni wazembe na hawafai. Ikiwa rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM ndiye aliyewateua watendaji hao, kwanini asiwabadilishe ili kuondoa tatizo la umeme na aweze kikiongezea Imani chama chake? Badala yake eti tusubiri hadi Magufuri achaguliwe ndiyo wawajibishwe. Kweli hii ni hujuma dhidi ya Magufuri, mgao huu unai-cost CCM, labda tu tushukuru watanzania wengi hatuna utashi wa kujua jema na baya (zero IQ) na ni wepesi kusahau.

CCM imepoteza dira na mwelekeo,JPM amechanganyikiwa hata anayemkemea hajui kama ndio boss wake na Serikali ambayo yeye yupo madarakani.
 
Yani mwaka huu hatufanyi tena kosa kuwapa ccm kura, hawa ni watu wakupigwa chini2
 
Back
Top Bottom