Hivi CCM hawana UKANDA, wao si wadini?

Hivi CCM hawana UKANDA, wao si wadini?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,175
Reaction score
48,459
Chama cha Mapinduzi kwa nyakati toauti kimekuwa kikivishambulia vyama vingine kwa hoja kwamba vyama hivyo vimejaa ukanda, udini na ukabila. Lakini huwa najiuliza maana ya ukanda na udini ni nini kwa Tafsiri ya CCM na wana CCM wenyewe. Mimi nakubaliana na tafsiri aliyowahi kuitoa Mwandishi nguli hapa nchini, Jenerali Ulimwengu kuhusu udini na ukabila.

Ulimwengu anasema kuwa udini ni ile hali ya kuwapima watu kwa kutazama dini zao na wala si wao kwanza kama binadamu. Kwa mfano kuna kazi inatolewa mahala fulani na wewe ndiye mtoa kazi, kuna watu wawili wana sifa zinazotofautiana. Wa dini yako ana sifa hafifu na wa dini nyingine ana zinazojitosheleza, lakini wewe unamuajiri wa dini yako kwa kuwa tu ni wa dini yako ingawa sifa zake hazitoshelezi, huo ndiyo udini na ukabila pia nao huko hivyo hivyo.

Lakini ukienda Pemba na Unguja ambako CUF ina wanachama wengi, asilimia kubwa ni waislam, hivyo haitarajiwi viongozi wengi wa CUF wawe wakristo, huo si udini bali ni matokeo ya Historia na ndiyo uhalisia. Kwa vyovyote vile hawa watu wa kutoka Zanzibar watakapokuwa Tanganyika wataahamiana sana na watu wanaokutuna nao kwenye misikiti kuliko wale wanaokwenda Kanisani, ushawishi wa CUF misikitini hautokani na udini bali unatokana na Historia ya chama chenyewe na uhalisia. Kuwa Mwanachama wa CUF si lazima uwe Muislamu wala Mpemba.

Tunayoifahamu kwa karibu Historia ya CHADEMA tunajua wakati wa kuanzishwa kwake na kabla hakijawa hivi kilivyo, wenye nguvu ndani ya CHADEMA walikuwa ni watu wa Kigoma wakiongozwa kina Alhaj Jaffary Kasisiko, Walid Kaborou na wengine wengi toka Shinyanga kama kina Mzee Philip Magadula Shelembi na Bob Nyanga Makani. Leo CHADEMA inapoitwa chama cha Wachaga eti kwa sababu tu mwenyekiti wake ni Mchaga huwa nashangaa sana!

Hivi CCM haina wanachama huko "Kaskazini"? Kati ya mawaziri Wakuu tisa tuliowahi kuwa nao kama taifa tena wakiwa wakati huo ni wana CCM wanne hawakutoka Kaskazini? Edward Sokoine, Edward Lowassa,Cleopa Msuya na Frederick Sumaye hawakuwa watu wa Kaskazini wakati wanapewa wadhifa huo. Huo ubaya wa watu wa Kaskazini huwa unaonekana wakati tu mtu anapokuwa nje ya CCM peke yake? Kinana ni mtu wa wapi kama siyo Kaskazini?

Kama watu wa dini moja kuwepo kwenye chama ndiyo chama hicho kuwa cha kidini, hivi wajumbe wengi Halmashauri Kuu na kamati Kuu ya CCM si waislam, hiyo peke yake inakifanya chama chao kuwa cha Kiislam? Uteuzi wa Magufuli umejaa watu wengi wa Kanda ya ziwa, hadi mbunge wa kutoka kwenye Jimbo analotoka la Chato, Jee Magufuli kachagua mawaziri na watu wengine kwa kufuata mambo ya Ukanda?

Kwa kufuata vigezo vya watu wa CCM wao kama chama hawana UKANDA na UKABILA na UDINI katka kuendesha siasa zao? Hivi yule mjinga aliyesema tena hata bila ya kukemewa na chama chake kwamba "Rais wa Tanzania hawezi toka Kaskazini" hakuwa anapalilia mambo ya ukanda?
 
Mkuu una hoja yenye mashiko.
Eti mtu anakuwa ni wa kaskazinianapokuwa nje ya ....

Hivi CCM haina wanachama huko "Kaskazini"? Kati ya mawaziri Wakuu tisa tuliowahi kuwa nao kama taifa tena wakiwa wakati huo ni wana CCM wanne hawakutoka Kaskazini? Edward Sokoine, Edward Lowassa,Cleopa Msuya na Frederick Sumaye hawakuwa watu wa Kaskazini wakati wanapewa wadhifa huo.
Huo ubaya wa watu wa Kaskazini huwa unaonekana wakati tu mtu anapokuwa nje ya CCM peke yake? Kinana ni mtu wa wapi kama siyo Kaskazini?
 
Mkuu una hoja yenye mashiko.
Eti mtu anakuwa ni wa kaskazini anapokuwa nje ya ....
Tatizo la Tanzania ni elimu,Elimu, Elimu. Na REDET walishawahi kusema kuwa CCM inaungwa mkono na watu wenye uelewa wa hali ya chini wa hali ya mambo hasa walioko vijijini!!
 
Kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini umezidi kudhihirisha ukanda ndani ya CHADEMA.

Mgombea wa Handeni Mjini aliachwa bila msaada ukilinganisha na mgombea wa Arusha Mjini.

Viongozi wote wakuu wa CHADEMA kama Mbowe wakiongozwa na mwanachama maarufu, Lowassa akishirikiana na Sumaye walipiga kambi Arusha Mjini kumsaidia 'mtu wa kwao' katika kampeni huku yule asiye 'wa kwao' kule Handeni akiachwa bila msaada.

Huhitaji kuingia darasa kufahamu ubaguzi unaofanywa ndani ya CHADEMA based on place where you come from or born! Umuhimu wa mwanachama ndani ya CHADEMA unatokana na sehemu unayotoka.

Mambo yanayofanyika ndani ya CHADEMA huwezi kuyakuta ndani ya CCM.

CHADEMA is not fit for purpose and institutional prejudiced!
 
hakuna wadini kama ccm,rais akiwa muislam atahakikisha kamati kuu ya ccm inakuwa kama kamati ya ujenzi wa msikiti,jk alilazimisha jaji mkuu,jaji kiongozi,CAG kuwa waislam japo hawakuwa na sifa hizo.kuna mawaziri mizigo kama kawambwa na ghasia waliwekwa pale sababu ya dini zao,mambo ya nje,nssf,mambo ya ndani ni kama msikiti.magufuli nae ameanza kufuata nyayo.asilimia kubwa ya teuzi zake za karibuni ni kama kamati ya baba paroko na hajawasahau wanakanda ya ziwa wenzake
 
Wewe ccm umeanza kuijua lini. Usishabikie kitu usichokijua kwa kuambiwa tu au kukariri.Kaome historia ya chama chako ilivyokuwa huko nyuma na ilivyo sasa halafu uje na hoja ya msingi inayoonesha upinzani ulianzaje na kwa nini uwepo.
 
atakayesema CCM kina UKANDA na UDINI watanzania hawatamuelewa. mimi mwenyewe sikuelewi. Bila CCM tungeshaparaganyika. Chama waongoze nchi si ikulu inaweza kuhamishiwa kaskazini
 
Kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini umezidi kudhihirisha ukanda ndani ya CHADEMA.

Mgombea wa Handeni Mjini aliachwa bila msaada ukilinganisha na mgombea wa Arusha Mjini.

Mambo yanayofanyika ndani ya CHADEMA huwezi kuyakuta ndani ya CCM.

CHADEMA is not fit for purpose and institutional prejudiced!
Una hakika Handeni hawakuweko viongozi waandamizi wa CHADEMA?
 
Mkuu una hoja yenye mashiko.
Eti mtu anakuwa ni wa kaskazinianapokuwa nje ya ....

Hivi CCM haina wanachama huko "Kaskazini"? Kati ya mawaziri Wakuu tisa tuliowahi kuwa nao kama taifa tena wakiwa wakati huo ni wana CCM wanne hawakutoka Kaskazini? Edward Sokoine, Edward Lowassa,Cleopa Msuya na Frederick Sumaye hawakuwa watu wa Kaskazini wakati wanapewa wadhifa huo.
Huo ubaya wa watu wa Kaskazini huwa unaonekana wakati tu mtu anapokuwa nje ya CCM peke yake? Kinana ni mtu wa wapi kama siyo Kaskazini?

ukaskazini unapaliliwa na maneno ya viongozi wa CHADEMA, vinara wakiwa MBOWE, SUMAYE, LOWASSA NA NASSARI. kwa nyakati tofauti walisema maneno yaliyowaogopesha watanzania wa kanda zingine.
 
hakuna wadini kama ccm,rais akiwa muislam atahakikisha kamati kuu ya ccm inakuwa kama kamati ya ujenzi wa msikiti,jk alilazimisha jaji mkuu,jaji kiongozi,CAG kuwa waislam japo hawakuwa na sifa hizo.kuna mawaziri mizigo kama kawambwa na ghasia waliwekwa pale sababu ya dini zao,mambo ya nje,nssf,mambo ya ndani ni kama msikiti.magufuli nae ameanza kufuata nyayo.asilimia kubwa ya teuzi zake za karibuni ni kama kamati ya baba paroko na hajawasahau wanakanda ya ziwa wenzake
Bila kusahau nafasi ya umakamu wa urais wa muungno wa tz hiyo nafasi ni ya watu wa dini fulani wakati huko na wakristo wapo huko
 
Kaskazini ya Ubaguzi ni mikoa 2 Arusha na Kilimanjaro.
Kitendo cha kusema kuna Kaskazini halafu kuna Kaskazini ya "ukanda" hizo ni fikra za kibaguzi. Maana wenzako hawajui kama Handeni nayo ni Kaskazini, Halafu Maneno gani yanayosemwa na wakina mbowe ambayo yanapalilia UKANDA?

Unakumbuka baada ya Mkuu wa Mwaka 2010 Kikwete aliwahi kusema kwamba kwenye uchaguzi ule alibaguliwa kutokana na dini yake? Ghafla akasahau kwamba aliyesema kwamba yeye ni "chaguo la Mungu" alikuwa ni Mkristu Mkatoliki Askofu Methodius Kilaini! Yale maneno yaliashiria kwamba Kikwete alibaguliwa na Wakristu. wewe unaamini kuwa wakristu walimbagua Kikwete kwenye uchaguzi wa 2010? CCM mnapotaka kusambaza sumu yenu ya kibaguzi huwa hamna haya wala aibu!!
 
Nimeanza kuijua CCM toka siku ambayo nilifahamu kusoma na kuandika!

Hii ccm ni ile wazee wako waliianzisha au ccm maslahi? CCM ya kurithishana. Baba, mjomba, shangazi, mtoto na maswahibs ktk uongozi. Je, hiyo ndiyo ccm unyoijua wewe kweli.Maana mtu husifia alichokikuta hata kama hajui asili yske. Kalaga baho.
 
CCM ndicho chama pekee cha kila Mtanzania. Vyama vingine ni. SACCOS za wachache

Hili jibu ulilotoa Lizaboni ni sahihi kabisa kwani ndio kazi unayopaswa kufanya hapa jukwaani hata kama unachotetea ni upuuzi. Wewe ndio uliyesifia safari za JK hapa wakati watu wanamuhesabia amefikisha safari ya ngapi. Leo bila aibu na wewe unashangaa upotevu wa kodi zetu. Huo uozo unaompa Magufuli leo watu walishaupigia kelele mpaka wakaamua kumuachia Mungu kisa wenye mamlaka walikuwa sehemu ya uozo huo. Napenda ufahau siasa za udini, ukabila na ukanda zimeletwa na ccm kama sehemu kuendelea kubaki madarakani. Ila tunachofurahi shimo mlilolichimba leo ndio mnaingia wenyewe. Sasa hivi Magufuli anapata tabu kupata watu wa kuwachagua maana anaogopa akifanya uchaguzi kwa kuangalia uwezo peke yake haeleweki. Vigezo vya muhimu kwa ccm ni dini, ukabila na ukanda kwanza. Kwa hiyo usishangae hajapata Mawaziri wanne wakati ana wabunge 250+. Hapo anajaribu kuacha vigezo vya weledi na kujali zaidi vionjo vya kipuuzi vya udini, ukanda na ukabila.

Kwa hiyo unapoona taifa letu linapata maendeleo kwa mwendo wa konokono ni kwa sababu tunaacha kuangalia uwezo na kutumia vigezo hivyo vya kipuuzi, vilivyoletwa na chama kilichopata nafasi ya kulitawala taifa letu kwa sababu za kihistoria na sio kiuwezo.
 
Back
Top Bottom