Hivi Bongo Muvi wana Shida gani hawa watu?

Madimba jr

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
1,577
3,143
Nimejiuliza sana,kuhusu Bongo muvi kuuvalia njuga msiba wa Agnes Nyie kama wakina nani? kwenye kesi yake mbona hamkuonekana hata? mnatoka na taarifa zinazotuchanganya mara mnasema kafa kwa homa ya matumbo na kupungukiwa damu leo mwingine anasema kafa kwa pumu...kila mtu anataka kuchukua ujiko kupitia kwa marehemu mara Irene Uwoya kasema hivi,mara Ka Steve Nyerere kanapanga ratiba ya msiba mara sijui Chopa anasema marehemu alimwambia maneno mawili kabla ya kukata roho WTF!! who are you people? Acheni mambo ya Kikanjunju....Familia ya Marehemu ipo waacheni wao ndio watoe na taarifa za msiba....Tangu lini Age alikuwa msanii wa filamu?
 
BINAFSI SIWAPENDI HATA SIKU MOJA. AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA SIWEZI KUKUBALI. UELEWA WAO NI MDOGO SANA. USANII USANII MTUPU. MAIGIZO MPAKA KWENYE VITU VYA MUHIMU HAPANA.
 
Wanajikaanga tu. Mwisho wa siku yeyote anaefanya jambo kwa marehemu ni sawa. Aggy alikua rafiki yao hao bongo movie kwahiyo wao kuubeba msiba si jambo la kujipendekeza. Ni utamaduni wetu kukitokea jambo kufarijiana bila kuangalia ni familia bongo movie bongo fleva au mwandishi.
 
kabisa ni utamaduni wetu kushirikiana kwenye shida na raha, tatizo linalotokea hapa ni kama usemavyo wanajikaanga na matamko yao kila mtu anakuwa msemaji.
 
Tatizo wanataka waonekane kila mmoja alikua karibu zaidi na marehemu. Kama kawaida yetu ya unafki binadamu mtu akishafariki ndo tunaonyesha wema wetu kwake
 
Haswaaaa, wakati yupo na matatizo ya kesi yake walikaa kimyaaa, hata kumsindikiza tu mahakamani hawakuweza leo wanajifanya wema.

Kweli sisi binadamu ni wanafiki wakubwa sana Mzigua
 
Wanajikaanga tu. Mwisho wa siku yeyote anaefanya jambo kwa marehemu ni sawa. Aggy alikua rafiki yao hao bongo movie kwahiyo wao kuubeba msiba si jambo la kujipendekeza. Ni utamaduni wetu kukitokea jambo kufarijiana bila kuangalia ni familia bongo movie bongo fleva au mwandishi.
Utapigwa wewe shauri yako.
 
Hivi huyu marehemu anahitaji faraja kwa kipindi akiwa marehemu kuliko kipindi kile alipokuwa na kesi mahakamani!? Mbona mimi binafsi sikuwahi kuwaona hao vilaza wanaojiita bongo movies wakimfariji kipindi akiwa na kesi!?
 
Ndiyo hapo mkuu unapojiuliza maswali mengi na kujijibu tu kuwa hawa bongo movie ni wanafiki, sio wote lakini

Walikuwa kimyaaaaaa wakati mtu anataabika na kesi yake leo mtu kaaga dunia wamekuwa wa kwanza kujitokeza na kuwa wasemaji wa familia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom