Hivi Bongo kuna celebrities wanaostahili kufuatiliwa kweli?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Wakati watu wanafuatilia na kujadili lile tukio la jana, mimi kwa kiasi fulani bado nashangaa kuona eti wale ndio miongoni mwa celebrities wa Bongo ambao watu wanatumia muda wao kuwafuatilia na kuwajadili kwa maana ya kuwaona ni watu wanaostahili kufuatiliwa sio tu kwa tukio la jana, bali kufuatilia mwenendo wao wa maisha.

Mtu katoka mtaani kaajiriwa katika chombo fulani cha habari au kawa msanii wa mziki/filamu teyari watu wanaanza kumfutalia na kumuona ni mtu maarufu kwao! Nashukuru Mungu huu ujinga mimi sina na ndio maana hata wale wa jana ndio kwanza nimewasikia hiyo jana na nimejithibitishia nilikuwa sahihi kutowajua na kutojua habari zao.

Kingine kinachonisaidia pengine ni kutoona umuhimu wa kusikiliza baadhi ya vituo vya Radio vya FM kwani huwa sioni la maana la kunivutia kusikilza na ndio maana hata watangazaji wengi wa vituo hivi huwa hata siwajui.

Wabongo sijui tukoje maana hawa ndio watu tunaowafutilia pengine kuliko hata wale ambao maamuzi yao yanaathiri au kugusa maisha yetu.
 
Kwani uongo???We tafuta Mil 2 au 3 tu alafu mtafute Wema au Uwoya Kama hutamla???

Kama una connection mjini fuatilia msanii Young D anakaa na nani alafu Njoo uniambie hapa!!
 
Wengi wanakosa elimu na siyo wasomaji wazuri wa vitabu. Hivyo hushindwa kujenga character yenye msingi katika jamii. Ukienda Kenya wasanii wengi wana master na kuendelea hivyo hufanya Sanaa Kwa sababu kipaji Chao halisi.
 
Kwani uongo???We tafuta Mil 2 au 3 tu alafu mtafute Wema au Uwoya Kama hutamla???

Kama una connection mjini fuatilia msanii Young D anakaa na nani alafu Njoo uniambie hapa!!
Watu wanamla kim kardashian sembuse wema..

Msiwadharau wabongo kisa ni wenzenu kama uchafu unafanyika zaidi Hollywood hapa bongo hata nusu hatujafika
 
Wengi wanakosa elimu na siyo wasomaji wazuri wa vitabu. Hivyo hushindwa kujenga character yenye msingi katika jamii. Ukienda Kenya wasanii wengi wana master na kuendelea hivyo hufanya Sanaa Kwa sababu kipaji Chao halisi.
Wengi wangapi ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom