Hivi Baba Askofu Kakobe alidanganya watu kuhusu "unabii" huu?

Ni wakati wao wa kuzivuna pesa Hawa vibaraka
 

Attachments

  • Screenshot_20201021_133440.jpg
    Screenshot_20201021_133440.jpg
    91.1 KB · Views: 1
  • Screenshot_20201021_133412.jpg
    Screenshot_20201021_133412.jpg
    83.1 KB · Views: 1
Awamu hii tumejua WWTUMISHI HALISI WA MUNGU na MADALALI WA DINI..

Lakini tumemuachia Mungu Mwenyewe aendelee kutofautisha magugu na ngano.
 
Maandishi na maandiko huishi. Yawe batili au halali. Nimekumbuka Baba Askofu Kakobe aliwahi kutoa matamko mazito kwa viongozi wakuu wa Nchi hii aliyodai katumwa na Mungu. Ingawaje kwa sasa amejenga mahaba makubwa na viongozi hao hata kabla ya wao kujirekebisha.

LA KWANZA ni waraka aliomwandikia Rais Kikwete kwa kitendo cha Serikali na Chama chake kuharibu mchakato wa Katiba mpya. Alimweleza Mungu amesema kwa kitendo hicho atauvunja utawala wake na Chama chake vipande viongozi vipande.

LA PILI ni pale alipomuonya Rais wa sasa Magufuli, kwa ukandamizaji wa haki za watu wa Mungu nchini. Alimuonya juu ya ghadhabu ya Mungu na kumtaka atubu.

Leo namuona Baba Askofu yuko mbele akiwashangilia watawala Hawa. Tuseme Baba alidanganya kuwa alitumwa na Mungu anayemtumikia? Au kamsaliti Mungu wake kama Yuda Eskariote?
Unabii umekuja kivingine kwa hiyo mtumishi hana budi kutii yaliyo mema machoni pa Mungu.
 
Back
Top Bottom