Hivi Baba Askofu Kakobe alidanganya watu kuhusu "unabii" huu?

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
1,201
2,000
Maandishi na maandiko huishi. Yawe batili au halali. Nimekumbuka Baba Askofu Kakobe aliwahi kutoa matamko mazito kwa viongozi wakuu wa Nchi hii aliyodai katumwa na Mungu. Ingawaje kwa sasa amejenga mahaba makubwa na viongozi hao hata kabla ya wao kujirekebisha.

LA KWANZA ni waraka aliomwandikia Rais Kikwete kwa kitendo cha Serikali na Chama chake kuharibu mchakato wa Katiba mpya. Alimweleza Mungu amesema kwa kitendo hicho atauvunja utawala wake na Chama chake vipande viongozi vipande.

LA PILI ni pale alipomuonya Rais wa sasa Magufuli, kwa ukandamizaji wa haki za watu wa Mungu nchini. Alimuonya juu ya ghadhabu ya Mungu na kumtaka atubu.

Leo namuona Baba Askofu yuko mbele akiwashangilia watawala Hawa. Tuseme Baba alidanganya kuwa alitumwa na Mungu anayemtumikia? Au kamsaliti Mungu wake kama Yuda Eskariote?
 

ngome1838

JF-Expert Member
Feb 20, 2019
226
250
Subira ni kitu kizuri katika kujua rangi halisi ya kiongozi katika nyanja yoyote iwe siasa au dini. I hate african politics
 

Shambaboy jogoli

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
1,066
2,000
Kwa Mungu ukitubu unasemehewa, haijarishi dhambi ni nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theruji! Tulianza na Mungu tunamaliza na Mungu! Nyie mnaounga mashoga mlaaniwe mpaka mshangae
 

Rogart Ngaillo

Verified Member
Apr 27, 2013
853
1,000
Alishasema kwa sasa anakula bata ikulu....mwache alipe gharama za bata aliowala,hana namna nyingine..ni mapambio tu!
 

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
873
1,000
Askofu Zacharia Kakobe wa FGBF ni mpinzani wa kiukweli toka enzi za Baba wa Taifa, sina shaka kuhusu hilo. Kwenye awamu hii ambayo haifuati utawala wa Sheria (Rule of Law), mkosoaji yeyote anaweza kufanywa chochote na akakosa mahala pa kushtaki. Hili limekwishamtokea Kakobe kwa kuwa tayari TRA ilikwisha tumwa kupitia akaunti za kanisa lake kwenye mabaenki.

Kimaadili ya benki ilikuwa ni kinyume cha sheria kuingia kwenye akaunti hizo, lakini kwa vile nchi inaendeshwa kidikiteta basi Kakobe akabakia hana namna bali kuunga mkono juhudi za Meko. Ikaonekana kuna mabilioni kwenye akaunti na kuna signatories wawili tu ambao ni Kakobe na mkewe.

Pili kuna hekalu kwenye makutano ya barabara ya Mwai Kibaki na Ally Sykes kule Mbezi Beach ambalo ni la kifahari sana bado linajengwa na halina maelezo. Haya ndiyo yamemtisha Kakobe

Mimi namsamehe bure Kakobe
 

Mr Tyang

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
1,266
2,000
Kipindi kile tulimuita shujaa na mtumishi wa Mungu anaejitambua Leo tunamuita Fala na Askofu asiejielewa.
Nyie binadam Ni wapumbavu Sana na itoshe tu kusema nyie niwa kupuuza tu.
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,513
2,000
Nia yako akupendeze wewe peke yako, ikitokea kampendeza mwingine unafura kama mbogo!

Mhogo mkubwa wewe!!
 

jo mose

JF-Expert Member
Aug 5, 2020
3,483
2,000
Aliambiwa si raia akaona sio tabu akaunga juhudi ili awe raia na kurudishiwa pasipoti yake plus usalama wa mabilioni yake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom