Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Tunafahamu kuwa Mbowe ni kiongozi mkubwa kabisa wa nchi hii, akiwa ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na pia ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi wa Hai, mkoani Kilimanjaro
Naye Ester Matiko ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi, kwa tiketi ya Chadema, kwa jimbo la Tarime mjini
Hao viongozi wakubwa kabisa wa Chama kikuu cha upinzani nchini, wanaendelea kusota gerezani kwa wiki ya 3 hivi sasa kwa kile ambacho Hakimu Mashauri wa mahakama ya Kisutu amekiita kuwa wameidharau mahakama na hivyo kuamua kufuta dhamana yao
Tunafahamu kuwa kwa kupitia wadhamini wao walishaiarifu mahakama kuhusu udhuru wao wa kutoweza kuhudhuria mahakama hiyo katika Siku hiyo husika
Tukumbike pia katika ufunguzi wa maktaba mpya ya Chuo kikuu cha Dar, Rais Magufuli alitumia jukwaa lile kwa kumpa salaam Mheshimiwa Lowassa kuwa awaambie viongozi wenzie wa Chadema, kuwa wataozea jela iwapo wataendelea kumis- behave!
Kwanza tutambue kuwa hao akina Mbowe ni watu maarufu nchini kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuziruka dhamana zao
Tukumbuke pia huyo Hakimu Mashauri, hao watuhumiwa akina Mbowe walishatuma ombi la kumkataa Hakimu huyo kuendelea kusikiliza Shauri lao kutokana na mwenendo wa kesi hiyo wanavyouona, ambapo Hakimu huyo anaonyesha upendeleo wa wazi kwa waleta mashitaka, ambao ni serikali, lakini cha kushangaza huyo Hakimu akagoma kujitoa na kuamua kuing'ang'ania kesi hiyo kama ruba!
Ndipo hapo tunapojiuliza hivi kuendelea kusota rumande kwa akina Mbowe, ni kukomolewa na serikali??