Hivi akina Mbowe wanaendelea kusota rumande kwa kukomolewa?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,130
Tunafahamu kuwa Mbowe ni kiongozi mkubwa kabisa wa nchi hii, akiwa ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na pia ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi wa Hai, mkoani Kilimanjaro

Naye Ester Matiko ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi, kwa tiketi ya Chadema, kwa jimbo la Tarime mjini

Hao viongozi wakubwa kabisa wa Chama kikuu cha upinzani nchini, wanaendelea kusota gerezani kwa wiki ya 3 hivi sasa kwa kile ambacho Hakimu Mashauri wa mahakama ya Kisutu amekiita kuwa wameidharau mahakama na hivyo kuamua kufuta dhamana yao

Tunafahamu kuwa kwa kupitia wadhamini wao walishaiarifu mahakama kuhusu udhuru wao wa kutoweza kuhudhuria mahakama hiyo katika Siku hiyo husika

Tukumbike pia katika ufunguzi wa maktaba mpya ya Chuo kikuu cha Dar, Rais Magufuli alitumia jukwaa lile kwa kumpa salaam Mheshimiwa Lowassa kuwa awaambie viongozi wenzie wa Chadema, kuwa wataozea jela iwapo wataendelea kumis- behave!

Kwanza tutambue kuwa hao akina Mbowe ni watu maarufu nchini kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuziruka dhamana zao

Tukumbuke pia huyo Hakimu Mashauri, hao watuhumiwa akina Mbowe walishatuma ombi la kumkataa Hakimu huyo kuendelea kusikiliza Shauri lao kutokana na mwenendo wa kesi hiyo wanavyouona, ambapo Hakimu huyo anaonyesha upendeleo wa wazi kwa waleta mashitaka, ambao ni serikali, lakini cha kushangaza huyo Hakimu akagoma kujitoa na kuamua kuing'ang'ania kesi hiyo kama ruba!

Ndipo hapo tunapojiuliza hivi kuendelea kusota rumande kwa akina Mbowe, ni kukomolewa na serikali??
 
Mbona Ester Matiko naye alikuwa kwenye ziara ya kibunge, huko huko Burundi, ziara ambayo hata Spika Ndugai alikuwa anaijua na aliibariki, lakini Hakimu Mashauri akaamua kuwafutia dhamana hao akina Matiko??

Ndipo hapo ninaposema kuwa ni lazima katika maamuzi hayo upo mkono wa Jiwe, kwa kuwa ameonyesha dhahiri namna anavyowachukia viongozi wa Chadema
 
Mbona Ester Matiko naye alikuwa kwenye ziara ya kibunge, huko huko Burundi, ziara ambayo hata Spika Ndugai alikuwa anaijua, lakini Hakimu Mashauri akaamua kuwafutia dhamana hao akina Matiko??

Ndipo hapo ninaposema kuwa ni lazima katika maamuzi hayo upo mkono wa Jiwe
Spika kujua kuwa Ester Matiko yuko kwenye ziara ya kibunge haina maana yoyote kwenye Mahakama. Kumbuka Mahakama ni muhimili mwingine unaojitegemea ambao una sheria na taratibu zake.

Fundisho alilopata Ester Matiko ndilo ambalo ametumia Mdee kama darasa.
 
Utazunguka, lakini ukweli utabaki pale pale, kuwa kukaa kwao rumande kina Matiko, kuna harufu ya mhimili wa Executive kuingilia mhimili wa mahakama

Refer kauli aliyoitoa Magufuli Siku za nyuma, kuwa mhimili wake ndiyo ambao uko "superior" kwa kuwa ndiyo uliojichimbia zaidi chini!
 
Mimi nimekupa ushahidi halisi lakini wewe unaleta hisia.

Kwa nini Mdee apate ruhusa kwenye kesi hiyohiyo kama hoja yako ni muhimili kujichimbia?

Mbowe na Matiko walitaka kufanya siasa kwenye mahakama lakini kwa bahati mbaya sheria hazina siasa!

Hili liwe ni funzo kwa wengine.
 
Hata ukiangalia chimbuko la kesi yenyewe, utagundua kuwa ni kesi ya kisiasa na wala siyo ya jinai, kama wanavyodai Polisi

Polisi wanadai kuwa Chadema waliitisha maandamano bila kibali chao.

Hivi hao Polisi watuambie ni katika ibara ipi ya Katiba ya Jamhuri inayowapa wao kibali cha kutoa kibali cha maandamano??

Kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 20, inaeleza kuwa maandamano ya amani ni ruksa kufanyika, Bali wao Polisi wanachotakiwa ni kutoa ulinzi pekee
 
Ukiangalia pia kuwa mtuhumiwa namba moja ambaye alistahili kuwa hapo Mahakamani, ni Mkurugenzi wa Kinondoni.

Ni kwanini hajaburuzwa mahakamani hadi hivi sasa??

Kwa kuwa chimbuko la maandamano hayo ni Mkurugenzi huyo kuamua kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe, kutowapa viapo mawakala wa Chadema, wakati alishawapa wenzao wa CCM

Hiyo ndiyo sababu kuu iliyowafanya hao Chadema kuamua kuandamana, hasa ukizingatia kuwa uchaguzi huo wa Kinondoni ulikuwa unafanyika kesho yake
 
Hata ukiangalia chimbuko la kesi yenyewe, utagundua kuwa ni kesi ya kisiasa na wala siyo ya jinai, kama wanavyodai Polisi

Polisi wanadai kuwa Chadema waliitisha maandamano bila kibali chao.

Hivi hao Polisi watuambie ni katika ibara ipi ya Katiba ya Jamhuri inayowapa wao kibali cha kutoa kibali cha maandamano??

Kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 20, inaeleza kuwa maandamano ya amani ni ruksa kufanyika, Bali wao Polisi wanachotakiwa ni kutoa ulinzi pekee
Je sheria inasemaje kuhusu muda wa kuandamana?
 
Mbona alisema pale udsm wataendelea kukaa jela, na alimtuma lowassa awapelekee ujumbe
Uzuri tuna Rais ambaye huwa anaongea ya moyoni mwake......

Kama watatokea wale watetezi wake, basi wajitokeze tu kutetea, lakini wanaujua ukweli wenyewe
 
Tunafahamu kuwa Mbowe ni kiongozi mkubwa kabisa wa nchi hii, akiwa ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na pia ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi wa Hai, mkoani Kilimanjaro

Naye Ester Matiko ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi, kwa tiketi ya Chadema, kwa jimbo la Tarime mjini

Hao viongozi wakubwa kabisa wa Chama kikuu cha upinzani nchini, wanaendelea kusota gerezani kwa wiki ya 3 hivi sasa kwa kile ambacho Hakimu Mashauri wa mahakama ya Kisutu amekiita kuwa wameidharau mahakama na hivyo kuamua kufuta dhamana yao

Tunafahamu kuwa kwa kupitia wadhamini wao walishaiarifu mahakama kuhusu udhuru wao wa kutoweza kuhudhuria mahakama hiyo katika Siku hiyo husika

Tukumbike pia katika ufunguzi wa maktaba mpya ya Chuo kikuu cha Dar, Rais Magufuli alitumia jukwaa lile kwa kumpa salaam Mheshimiwa Lowassa kuwa awaambie viongozi wenzie wa Chadema, kuwa wataozea jela iwapo wataendelea kumis- behave!

Kwanza tutambue kuwa hao akina Mbowe ni watu maarufu nchini kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuziruka dhamana zao

Tukumbuke pia huyo Hakimu Mashauri, hao watuhumiwa akina Mbowe walishatuma ombi la kumkataa Hakimu huyo kuendelea kusikiliza Shauri lao kutokana na mwenendo wa kesi hiyo wanavyouona, ambapo Hakimu huyo anaonyesha upendeleo wa wazi kwa waleta mashitaka, ambao ni serikali, lakini cha kushangaza huyo Hakimu akagoma kujitoa na kuamua kuing'ang'ania kesi hiyo kama ruba!

Ndipo hapo tunapojiuliza hivi kuendelea kusota rumande kwa akina Mbowe, ni kukomolewa na serikali??
Wakati anatuma yale maselfie akiwa dubai na ubelgiji ndio ilikuwa kipindi cha kupiga kelele lakini mlikuwa mkishangalia sasa wacheni kulia na sheria mlioichezea!
 
Mbowe alishindwa kutumia hekima, haiwezekani udhuru upelekwe mahakamani kuwa amekimbizwa south africa akiwa mahututi. Siku ya pili tu picha za akiwa kwingine zinasambaa mitandaoni
 
Msimu huu hakuna hizo mambo. Wacha watu wachape kazi sio kuwaandamanisha kila siku. Kwa hali iliyopo UFIPA mambo yangekuwa hivi
1. Elimu bure- Maandamano
2. Flyover - Maandamano
3. SGR-Maandamano
4. Wafanyakazi hewa -Maandamano
5. Mafisadi wakikamatwa- Maandamano
6. Kununua korosho- Maandamano
7. Kuimarisha bandari- Vita kamili
8. Safari za nje zisizo na tija- Maandamano
9.Uhakika bei ya pamba- Maandamano
10. Madawati- Maandamano
11. Ujenzi wa vituo vya afya- vyanini? - vita
12. Spidi ujenzi umeme vijijini - Maandamano
Aiseee acheni kulialia fanyeni kazi. Hata huko tulikorithi mifumo hii ya tawala za vyama vingi vya siasa watu wao wanafanya kazi. Huwa wanaandamana panapokuwa na mambo ya msingi ambapo panalazimika kuishinikiza serikali. Leo ufaransa wanaharibu taswira ya mji wa Paris kwa wanaoniija Yellow vests kuchoma magari na mali za watu. Hasara zinazokadiriwa kusababishwa na maandamano ya muda mfuoi tu ni zaidi ya dollar bilioni moja sawa na madafu zaidi ya Trillion 2.6. Serikali yetu hasa ya awamu ya tano ni sikivu na hasa kama kuna hoja zinazogusa wanyonge majibu yamekuwa yakitoka mubashara kabisa. Niwaombe watanzania tuendeleeni kumuunga mkono mheshimiwa Rais wetu John MAGUFULI kwa kuchapa kazi.
Hivi wewe unaona maandamano ya Chadema yalikuwa hayana msingi?

Hivi inawezekanaje Mkurugenzi wa Kinondoni afanye upendeleo wa waziwazi kabisa kwa CCM kwa kuwapa viapo vya mawakala wao, wakati wale wa Chadema akiwanyima bila sababu za msingi??
 
Tukumbuke pia huyo Hakimu Mashauri, hao watuhumiwa akina Mbowe walishatuma ombi la kumkataa Hakimu huyo kuendelea kusikiliza Shauri lao kutokana na mwenendo wa kesi hiyo wanavyouona, ambapo Hakimu huyo anaonyesha upendeleo wa wazi kwa waleta mashitaka, ambao ni serikali, lakini cha kushangaza huyo Hakimu akagoma kujitoa na kuamua kuing'ang'ania kesi hiyo kama ruba!

Inajulikana wazi kwamba kesi ya msingi inayowakabili akina Mbowe na viongozi wenza inamsukumo wa kisiasa.

Ninaloshindwa kufahamu ni kwa nini washtakiwa wasingeendelea kumkataa huyo hakimu; na kama ni kulazimisha, basi ionekane wazi kwamba wanahukumiwa kwa kulazimishwa.

Kwa bahati mbaya sana, Mh Mbowe kajiingiza kwenye mtengo mbovu kabisa, hata sielewi ni kitu gani kilichomtokea safari hii akanaswa kishamba namna hii! Amewapa fursa waliokuwa wanamtafuta kwa udi na uvunda waonekane kuwa na sababu halali ya kumtia msukosuko asioustahili. Labda ipo sababu tusiyoielewa.
 
Nami nawauliza wajuvi wa sheria na sio mabush lawyer kuwa, hivi ile kauli ya mfunguzi wa maktaba pale mlimani haiwezi kuibatilisha kesi na kuiondoa mahakamani baada ya kuingiliwa mwenendo wake na mtu mkubwa sana?
 
Tunafahamu kuwa Mbowe ni kiongozi mkubwa kabisa wa nchi hii, akiwa ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na pia ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi wa Hai, mkoani Kilimanjaro

Naye Ester Matiko ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi, kwa tiketi ya Chadema, kwa jimbo la Tarime mjini

Hao viongozi wakubwa kabisa wa Chama kikuu cha upinzani nchini, wanaendelea kusota gerezani kwa wiki ya 3 hivi sasa kwa kile ambacho Hakimu Mashauri wa mahakama ya Kisutu amekiita kuwa wameidharau mahakama na hivyo kuamua kufuta dhamana yao

Tunafahamu kuwa kwa kupitia wadhamini wao walishaiarifu mahakama kuhusu udhuru wao wa kutoweza kuhudhuria mahakama hiyo katika Siku hiyo husika

Tukumbike pia katika ufunguzi wa maktaba mpya ya Chuo kikuu cha Dar, Rais Magufuli alitumia jukwaa lile kwa kumpa salaam Mheshimiwa Lowassa kuwa awaambie viongozi wenzie wa Chadema, kuwa wataozea jela iwapo wataendelea kumis- behave!

Kwanza tutambue kuwa hao akina Mbowe ni watu maarufu nchini kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuziruka dhamana zao

Tukumbuke pia huyo Hakimu Mashauri, hao watuhumiwa akina Mbowe walishatuma ombi la kumkataa Hakimu huyo kuendelea kusikiliza Shauri lao kutokana na mwenendo wa kesi hiyo wanavyouona, ambapo Hakimu huyo anaonyesha upendeleo wa wazi kwa waleta mashitaka, ambao ni serikali, lakini cha kushangaza huyo Hakimu akagoma kujitoa na kuamua kuing'ang'ania kesi hiyo kama ruba!

Ndipo hapo tunapojiuliza hivi kuendelea kusota rumande kwa akina Mbowe, ni kukomolewa na serikali??
Mbona walishaachiwa huru tangu jana?
 
Hata ukiangalia chimbuko la kesi yenyewe, utagundua kuwa ni kesi ya kisiasa na wala siyo ya jinai, kama wanavyodai Polisi

Polisi wanadai kuwa Chadema waliitisha maandamano bila kibali chao.

Hivi hao Polisi watuambie ni katika ibara ipi ya Katiba ya Jamhuri inayowapa wao kibali cha kutoa kibali cha maandamano??

Kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 20, inaeleza kuwa maandamano ya amani ni ruksa kufanyika, Bali wao Polisi wanachotakiwa ni kutoa ulinzi pekee
Akili yako wewe jamaa ni ya kipimb***** sana.Kama unakiri kuwa polisi wanatakiwa wapewe taarifa, je una barua yyt ya chadema kuitaarifu polisi kuwa wanaandamana tena zaid ya saa 12 jioni na wanahitaji ulinzi?Hivi huko ufipa kwanini mnapenda kujitoa ufaham?
 
Tunafahamu kuwa Mbowe ni kiongozi mkubwa kabisa wa nchi hii, akiwa ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na pia ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi wa Hai, mkoani Kilimanjaro

Naye Ester Matiko ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi, kwa tiketi ya Chadema, kwa jimbo la Tarime mjini

Hao viongozi wakubwa kabisa wa Chama kikuu cha upinzani nchini, wanaendelea kusota gerezani kwa wiki ya 3 hivi sasa kwa kile ambacho Hakimu Mashauri wa mahakama ya Kisutu amekiita kuwa wameidharau mahakama na hivyo kuamua kufuta dhamana yao

Tunafahamu kuwa kwa kupitia wadhamini wao walishaiarifu mahakama kuhusu udhuru wao wa kutoweza kuhudhuria mahakama hiyo katika Siku hiyo husika

Tukumbike pia katika ufunguzi wa maktaba mpya ya Chuo kikuu cha Dar, Rais Magufuli alitumia jukwaa lile kwa kumpa salaam Mheshimiwa Lowassa kuwa awaambie viongozi wenzie wa Chadema, kuwa wataozea jela iwapo wataendelea kumis- behave!

Kwanza tutambue kuwa hao akina Mbowe ni watu maarufu nchini kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuziruka dhamana zao

Tukumbuke pia huyo Hakimu Mashauri, hao watuhumiwa akina Mbowe walishatuma ombi la kumkataa Hakimu huyo kuendelea kusikiliza Shauri lao kutokana na mwenendo wa kesi hiyo wanavyouona, ambapo Hakimu huyo anaonyesha upendeleo wa wazi kwa waleta mashitaka, ambao ni serikali, lakini cha kushangaza huyo Hakimu akagoma kujitoa na kuamua kuing'ang'ania kesi hiyo kama ruba!

Ndipo hapo tunapojiuliza hivi kuendelea kusota rumande kwa akina Mbowe, ni kukomolewa na serikali??
Haya yote ni Mapito tu. Kila jambo lina mwisho wake walikuwepo makatili Wa kutisha, lakini wote wamepita, na hawa pia watapita.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom