Hitimisho na majibu ya battle ya Arusha na Mwanza

Arusha ni Geneva ya Africa, Mwanza ni Geneva ya Tanzania
Ilo jina TU NI sawa na singida kwetu tunaita SINGAPORE je kweli inataka kufanana na singay...wahuni tu waliamua kuitungia lete facts za kustahili kuitwa Geneva.....TU BASE KWENYE MAGHOROFA PEKEE MWANZA TOWN NA ARUSHA TOWN KUPI KUNA VIBERITI VYA KWENDA VYA MAANA?
 
Kwenye huu mjadala naweza kusema nina bahati ya kuwepo hizi Sehemu mbili (2) maana Nina mkataba wa miaka 3 sasa Mwanza lakin pia Arusha ndiko niliko zaliwa japo sikukaa sana nikahamia mkoa mwingine pendwa dsm.( u name it! )

Hii mada naweza kuijibu kupitia vipengele vifuatavyo:-

i/MPANGILIO WA JIJI
Arusha ni kubwa na imepangiliwa kisawasawa Toka Enzi za Mkoloni tatizo ni moja tu mji haukui tena kwa kasi takriban kipind cha miaka 60 kutokana na athari za kisiasa . Kuongozwa na chama pinzan kwa mda mrefu .
Uzuri wa ARUSHA ni Jiji lililo katika ardhi isiokuwa na mabonde sana wala milima milima ya mawe mawe .
juhud kubwa za mipangilio ya jiji hili ilifanya tangu enzi za kikoloni ambapo wazungu waliasisi ofisi zao na makazi kitu ambacho kimeathiri watu wake wana mentality ya kizungu. Usishangae kukuta nyumba kali ziko vijijini, vyuo na shule pia miuondombinu ya barabara na mazingira , pia ni jiji pekee tanzania ambapo wazungu wakifika huwa wanapashangaa , Arusha iko vzur sana tofauti na jiji la Mwanza ambayo mwanza imezungukwa na milima na mawe mengi kitu ambacho inafanya watu wejenge miliman na ardhi tambarare ikiwa chache, wakati arusha ikirembwa na milimi iliyojaa mimea na miti ya asili uku maji yakitiririka miez yte 12 ktk mwaka
Arusha inakupa maeneo bora machache yenye nyumba kali kavile vile:- njiro, uzunguzi, mianzin na kaloleni wakat MWANZA ina maeneo mengi bora kabisa ya nyumba za kuishi kama vile kisesa, bwiru, nyasaka, nyamhongolo na buswelu.

ii/MENTALITY(iQ)
Watu wa Arusha wana IQ kubwa ukilinganisha na ya watu wa mwanza Watu wa Arusha mentalility zao nikutafuta hela na kufanya maendeleo pia isitoshe kusema kwamba watu wa arusha wamebarikiwa Akili , ujanja na muonekano wa kuvutia raia wengi wa arusha (machalii/njeree)
Wanamin katika Shule, elimu , biashara na kufanya kazi kwa bidii ili kutusua kimaisha kwa uchunguzu mdogo tu angalia watu wanaotoka kaskazin ktk eneo lako unaloishi(wachaga/wapare/wameru na warusha) kama hana nyumba ugenini basi ana gari au ana kitega uchumi cha biashara .
Wakati vijana wengi na raia wa mwanza ( mamii/ngosha) wakiwa wamejaa ushamba, kupenda kutumia nguvu kubwa kuliko akili na kufatilia maisha ya watu. (Fanya tasmini ndogo tu popote pale ktk mkoa ulipo -(wasukuma ni wauza mabucha , wachapa kazi za kilimo , wafanyakaz za ndani, wachunga mifugo na ni mabodaboda.

BURUDANI PASIPO-PESA
Ni rahisi sana kuburudika ukiwa ARUSHA kuliko MWANZA maana kule kuna parks za bure, vijiwe vya draft , kahawa na maziwa kitu ambacho kitakuburudisha muda wte na kukufanya usi-jihisi mgeni/mpekwe jijin hapo mfano .
Nenda Pale kwa yahaya/ omar alkasusi - noble house( stand ya cruise za karatu)., stand ya zaman ya mabus, na uwanja wa shkh amri abeid.
Sehem kama hizo huwezi kuzi-pata ukiwa MWANZA.

SEHEMU ZA MJINI
Idadi ya watu ARUSHA ni kubwa, na gar za kutembelea (Subaru/alteza/corola/runx /cruizer na premio) zipo kwa wingi barabaran na kwenye parking .
Na watu wa arusha wanakatabia ka kutembea jioni na asubuh kama halaiki wanapoelekea au kurud majumban wanapotoka kazin . Hapa nyomi utaliona kuanzia jogoo house hadi sinoni.

MWANZA idadai ya watu ni kubwa kijijini na maeneo ya Mjini watu ni wachache sana na gar sio nyingi barabarani (hiace/crown/dualis/ist/carina/alphad) zimejaa.
Ili kuona wingi wa watu,
Hapa tembelea jion mitaa ya IGOMA na BUHONGWA ndo utaona nyomi za watu wakizurura barabarani.

iii/ARDHI
Ardhi ya arusha imebarikiwa sana katika nyanja za ufugaji ,kilimo na kuchimba madini, ukirejea kwenye ardhi imebarikiwa rutuba na hali ya hewa ya arusha ni nzur kuliko ya mwanza , bila kusahau MWANZA pia imebarikiwa ardhi yenye madini mengi na dhahabu hasa ktk maeneo yaliyomegwa ya mkoa wa GEITA.
ARUSHA Mazingira mengi yana mito na chemchem asili ambayo yanakupa uwezo wa kufanya shughuli za ufugaji na kilimo kama vile Migomba, kahawa, mahindi, maharage, maua, mboga mboga, ngogwe, bamia, mboga za majani, mipunga na maeneo mengi ya kufanya biashara.
Tofaut na MWANZA inakupa :- uvuvi (sato/sangara/dagaa), ufugaji na kilimo sehem za mbal kama lamadi, ngudu,kisesa,bariad, magu na sengerema na ni kwa kiasi kidogo tu. MWANZA wanapaita kwa washamba lakini sio kweli, labda ushamba ni kutojuwa mambo mengi ambao yameletwa na technolojia kwahyo vitu vingi ambavyo vinafanyiaka mikoa kama Arusha na Dar wao huwa wanashangaa na kukiona ni kipya hii nadhan ni sababu ya changamoto ya umbali vinapotoka vitu hivyo.
Mwanza Unaweza kutembea mji wote na wala usione mtu kashika jembe au kalima hata bustani ya mchicha nje kwake , tofauti na Arusha yenye asili ya kilimo, ndomana miaka na miaka mashamba ya mikahawa pale kisongo yamejaa miti mirefu uku chini wakilima, mahindi, migomba mboga mboga na maharage na haijawahi kukauka miaka nenda rudi.

iv/TASISI ZA KIELIMU NA VYUO VIKUU Ni ukwel usiopingika kwa ngaz ya elimu arusha ina shule nzur za msingi na secondary tofaut na mwanza.
wazungu wanafadhili sana na wamewekeza shule nyingi na wanafanikisha kutoa elimu katika eneo zima la mkoa wa arusha pili arusha ina vyuo kadhaa kama vile chuo cha kijeshi MONDULI, Arusha Technical Collage (ATC) , The aghakan University,IAA, CHUO CHA MANDELA, Chuo cha mifugo kule Tengeru na MAKUMIRA Lakini kwa upande wa vyuo vikuu Mwanza wanavyo vikubwa kama vile SAUTI, CUHAS(Bugando University), Chuo cha walimu BUTIMBA na Campus za vyuo kama vile DIT, CBE, IFM, TIA, OUT.

V/TASISI ZA KIAFYA Kwa upande wa taasisi vituo na hospital zinazotoa matibabu kwa Mkoa wa Mwanza ni bora na nzur zaid kuliko arusha. Arusha wana vituo vya afya na hospital kama vile Mount meru hospital, The aghakan Arusha medical centre, st joseph health care int, shree hindu, Arusha lutheran, sellian hospital.
Kwa mwanza wana vituo kama Mwanza hospital, agha kan, lancet laboratories,Nyamaghana,UMC hospital,Uhuru hospital,Mwanza adventist, Kamanga medics,Bugando, sekoture.

Vii/MIUNDOMBINU NA BARABARA Hapa bado sehem zote 2 zinachangamoto lakin kwa Arusha japokuwa nying zimeharibika kwa uchakavu na mashimo lakin ni nyingi na zinafanya usafiri uwe rahisi:- Barabara kama vile za kalolen hadi maji ya chai, chekeren hadi tengeru, atomic/njiro mpaka kwa morombo, barabara ya USA river mpaka Mbuguni na barabar nyingi za kstikati ya jiji zilizoigawanyika na kulipendezesha jiji.
Mwanza wanajikongoja kidogo kwani kwa sasa wanabara bara mpya na za njia 4 kama ile ya kuanzia Roundabout ya mti wa kunyongea karbu na bank ya CRDB inayoenda mpaka Airport , Barabara mpya ya sabasaba mpka buswelu, barabara ya pansiansi-kiloleli/bigbite mpaka buzuruga na Barabar ya nyashishi mpaka igoma. Uku barabara za nyamadoke, kanyerere, igombe na Tx zikiwa katika hali ya changarawe(vumbi).

ix/VIVUTIO
MWANZA kuna vivutio kadhaa na beach za kutosha kutokana na uwepo wa ziwa victoria tofaut n arusha beach za kule ni za mitoni na kwenye swimming pools : kwa mwanza unaweza kwenda kuenjoy beach :-Malaika, Tunza, Annex, jembe , charcoal, wag hil , ,Bismark rock na bar,Tilapia, ryans bay. Bar kadhaa kama vle :- BONASERE, The casky, Bundasiliga, The wallet , amazon night fashion nk. Kwa arusha machimbo kama Naura spring, texas, pale sanawar, bar za kijenge juu , kula nyama kule kwa mromboo na nk
=HOTELS= kwa upande wa HOTEL Arusha is the Best in Hotels mana wana hotel za kimataifa kutokana na soko lao kubwa la watalii : Hotel bora kama vile Venus premier , Panone hotel sakina, New hotel aquline, The charity hotole international, Mazola safar house, mount Meru hotel, boulevard inn, Masailand safar lodge, Four point by sheraton hotel, kibo palace , Palace Hotel, Arusha Hotel Nk. Hizo zote huwez linganisha na hotel za Mwanza kama vile GoldCrest, Tilapia, Aden palace, Hotel kingdom, couple gateway, Ryans Bay , Victoria palace, Lakairo hotel. *CHA KUFURAHISHA Baadhi ya hotel zilizo mwanza arusha pia zipo kama vile , Goldcrest, Lenana.

DAY TOUR :- kwa arusha unaweza tembelea masai village/ arusha national park, materun waterfalls, cultural heritage, ngorongro crater, hot spring.
wakat kwa mwanza utatembelea kisiwa cha Saa 8, makabur ya mv bukoba , ukerewe , sengerema na kijiji cha wasukuma (Bujora).
KWa ufupi ni rahisi kuizunguka MWANZA kwa siku 1 nakuimaliza.
Ila kwa ARUSHA huwez kuizunguka na kuimaliza pia inakupa vitu vingi zaidi ya vinavyopatikana MWANZA.
Kwa ufupi Arusha inakupa vitu vingi ambavyo Mwanza vipo na Mwanza na haiwez kukupa vitu ambavyo Arusha vipo .
kwa case ya utalii, vivutio , survey ya mji na starehe.
**kwa Bar ARUSHA usiulize ni sehem watu wamezaliwa ili kulewa wana BAR kali ambazo MWANZA hakuna na nikisema nizitaje hapa siwez maliza, Picnik, Club cocoriko, Mrina, the anex, Texasi , Bilionaires lounge, Empire sport bar, Triple A night club, Club D ______________ to infinity. Wakati kwa MWANZA utapata kufika kwenye Bar kama:- Diamonds autolink, The casky, Ms, Laliga, Bundasiliga, Night fashion, The amazon, kibosho resort, Break day, Bonasere, The joint, villa park, Riverside(imefunikwa na Night fashion), waka pub, if not y, not bar, Chicken run Bar.

x/VIWANJA VYA MICHEZO
Viwanja vya michezo MWANZA ina viwanja vikubwa na vzur kuliko ARUSHA.
Kwa Mwanza wanaviwanja kama vile: Monty's sport park, TSC sport ground, Makongoro basketball ground,DIT football ground, Furahisha football ground, Airport football ground, Bwiru boys football ground,Mbao fc groundna viwanja vya michezo sabasaba (japo wafadhili walitoa fedha vijengwe kwa ubora hela ikaliwa na matokeo yake ndo viwanja hivyo vilivyo) , CCM KIRUMBA STADIUM, Nyamaghana Stadium na kile kiwanja cha kule misungwi kiwanja cha Gwambina fc .
Kwa Jiji la ARUSHA kuna viwanja vichache mnoo na vingi sio vzuri ukilinganisha na vya MWANZA kama kile cha SHEIKH AMRI ABEID STADIUM, kile cha Kiwanja cha muekezaji karatu (black rhino) , kiwanja cha pale kisongo na kile kiwanja kidogo cha mpira sinoni .

xi/ MASOKO MAKUU.
MWANZA inajengeka kwa kasi sana na ya kisasa zaidi wakati ARUSHA ina dumaa na haikui, siasa pia inaweza ikawa ndio sababu kuu Kuchangia kuwa ivo kwa kipind cha miaka 10 iliyopita.
Tukirud kwenye lile soko pale mjini MWANZA lipo ktk hatua za mwisho likimalizila litakuwa ni zuri na bora kuliko soko lolote pale ARUSHA na litakuwa la kisasa mno na kuvutia lakin kwa sasa mwanza kuna masoko ya kienyeji tofaut na lile soko kuu la arusha karibu na stand kuu . Masoko Mengi kwa mikoa yote ni local markets kama ya pale Kilombero, soko la buhongwa, soko la nyamilongo na masoko mjinga yte tunayoyajua yakiuza bidhaa za kupanga chini kama kule Tengeru , igoma, kiloleli na stand za vituo vya daladala .

xii/STAND KUU/AIRPORT.
Kwenye eneo hili MWANZA iko vzur na imeaicha mbali sana ARUSHA ukiangalia kiwanja cha ndege Mwanza airport/- Kiwanja kipya kinachojengwa ni kizur kuliko kile cha kisongo japo arusha kwa miundo mbinu ya usafir wa anga bado iko chini na wakitegemea zaid kiwanja cha Ndege KIA.
Pia kwa upande wa Stand , stendi mpya inayojengwa MWANZA ni bora zaid kuliko ile ya Arusha, arusha bado ikiendlea kutumia stend ya pale Majengo karbu na celian Hospital na ile stend ya mabus ya zamani. Apo ndo unapoona MWANZA inapoipiga parefu ARUSHA.
achana na ile stand ingine ya kule Nyamhongolo inayojengwa na mchina.
Hapa kwa masoko/ stand na Aiport MWANZA ni Bora na ya kuvutia zaid kuliko ARUSHA . Kwa point hiyo mwanza ipo juu.

xiii/MAKAZI
Hapa kwenye nyumba za kuishi(Residence House) MWANZA iko juu zaid ukilinganisha na ARUSHA, Arusha bado ina mijengo ya kizaman pia maeneo ya mjini yamejaa nyumba ambazo hazifati mipango miji bado arusha kuna ubeberu mwingi sana ktk kumiliki ardhi na haina mijengo ya kuishi(residenceHouse) za kuvutia na kutikisa kama MWANZA, Maeneo ya uswazi kwa ARUSHA nyumba zimebanana sana nyumba za mabanzi na matope bado zipo (unga ltd, sinoni, sombetini) raman hazivutii.
MWANZA Ina mifumo yao ya nyumba za mapaa marefu lakini zinavutia sana mitaa kama Kiseke, Buswelu, Nyasaka na Nyamhongolo.
Pia sehem za uswazi za MWANZA ni maeneo mengi ya miliman watu wamejenga miliman maeneo kama (mabatini/mataulo/ghana na kirumba).

Yaan ARUSHA sehem za uswazi ni uswazi kweli kweli ikinyesha mvua huwez kutembea.
Kwa MWANZA Ktk swala la kumaintain uswazin limejitahid sana. BIG UP!

xiv/ VITUO VYA UTAMADUNI NA UTALII
Hapa ARUSHA ipo juu sana maana jiji limejengeka kuwa jiji la kitalii kutokana na uoto wa asili uliopo unaofanya kuzungukwa na mbuga nyingii kama vile Tarangire, ngorongoro , serengeti, manyara, na kuvutia wageni wengi. Ndomana usishangae kuutana na wazungu kila baada ya dakika 1 ni kawaida mnoo.
Tofauti na MWANZA, ambapo watalii wengi ni watalii wandan na ndugu zetu kutoka nchi jiran za burundi, uganda na kenya kila weekend wakija tukijumuuika nao kwenye bia za pale casky na samak choma kule Night fasion na bundasiliga.

HITIMISHO :
kila sehem kwa maono na mawazo yangu mm ni nzur, tofaut inakuja tu pale ww unavutiwa na nn?? ktk kila eneo, na sababu za kimazingira pia zinachukuwa nafasi kubwa na kuathiri uwezo wa kupenda kitu mfano, mimi MUBIKU naweza kusema Umbali ni Changamoto kubwa kwa MKOA wa MWANZA , sababu labda kwetu ni zanzibar au Mtwara hivo siwez kuonana mara kwa mara na wapendwa wangu/ watu niliowazoea au kufika nyumban kwa haraka kama kuna jenga limetokea na linahitaj uwepo wangu.
Lakini pia naweza kupapenda Mwanza sbabu kimkakati ni kama vile HUB ya Afrika mashariki popote pale nakwenda, umbal wa kutoka Mwanz - kigali/Mwanz- Bujumbura/Mwanza - Nairobi/ Mwanza - Kampla ni karbu mno ukilinganisha na Arusha na izo sehem nilizozitaja.

ARUSHA ni (NZURI MNOO) kuliko Mwanza maana inakupa vitu vingi ambavyo mwanza hakuna.
MWANZA ni (NZURI KWA KUISHI , USTAWI NA MALEZI KWA FAMILIA)
kuliko Arusha tukija katka swala la:-
i/Utaftaji na Gharama za maisha(Mwanza)
ii/Ujenzi na Umiliki wa Ardhi
iii/Kilimo na Uwekezaji (ardh/bidhaa/mzunguko wa watu)
iv/Ni mji unaojengeka kisasa, nyumba za kisasa, ofisi na miundombinu

ARUSHA ni Nzuri na inavutia hali ya hewa na kimazingira (uoto wa asili) wa Mji na watu (milima , mito, mikahawa, midizi , nyasi za kijani/wanawake wazur wa asili, weupe, sura zenye uchotara, hips na makal** makubwa .
Tofauti na wanawake wa mwanza maumbo makubwa, weupe wachache(dili sna) na wenye sura za baba zao.
ARUSHA:-
(wachapakazi/wanajuakupambana na maisha/wanajiamini/wanajitambua/ wazur kwa sura na wamejaliwa maumbo mazuri , shape/urefu/sura , mat*k** na hips) .
MWANZA uoto na muonekanao wa milima-milima mingi na mawe ila imejaliwa ziwa , beach za kutosha, usafi wa mji .

KWA UPANDE WA Matumiz na Kula starehe, (Bata) na totoz nzuri ARUSHA ni mji bomba kabisa na the Best hivyo unabid utambue nafasi yako ulipo (utaftaji / kutwanga raha(kuishi)
NB: Arusha haikui kwa mijengo na miundombinu yake ni ile ile tangu ya Enzi ya mkoloni na utawala wote wa vipindi vya miaka 60 ya uhuru japo majengo machache kwa sasa yameenza kujengeka hivyo basi kwenye utafutaji.
GHARAMA:
a.Ujenzi ni Juu
b.Chakula na malazi
c.Usafir(nauli)
d.Mavazi (Japo arusha ni moja ya jiji raia wake wana vaa vtu clasic na OG sana.
i/(HUSTLE)- U Deserve Mwanza ila kama ulishatafuta upo kwenye kutumbua na kula maisha
ii/(BATA). ARUSHA ni jiji la kutumia na kula Raha.Being in Arusha
Wish all the Best.
Eti Arusha iko karibu na Serengeti ! Unalinganisha kijiji cha wavuta bangi na jiji la Mwanza
 
Ilo jina TU NI sawa na singida kwetu tunaita SINGAPORE je kweli inataka kufanana na singay...wahuni tu waliamua kuitungia lete facts za kustahili kuitwa Geneva.....TU BASE KWENYE MAGHOROFA PEKEE MWANZA TOWN NA ARUSHA TOWN KUPI KUNA VIBERITI VYA KWENDA VYA MAANA?
Bill Clinton ndiyo aliipa hiyo hadhi ya Geneva ya Africa
 
Jidanganye. Hapa hakuna cha wachagga wala waarusha. Hapa ni wanakanda ya ziwa wanafanya vitu vyao wakiongozwa na Ngoshas wenyewe. Watu wkivuna migodini wanakuja kuwekeza kwenye Jiji lao
Wanaojenga Jiji la Mwanza kwa wingi ni watu wa kaskazini i.e wa Arusha na Kilimanjaro
 
Jidanganye. Hapa hakuna cha wachagga wala waarusha. Hapa ni wanakanda ya ziwa wanafanya vitu vyao wakiongozwa na Ngoshas wenyewe. Watu wkivuna migodini wanakuja kuwekeza kwenye Jiji lao
Wanakanda ya ziwa Bado wamelala watu wa kaskazini wanakamata fursa karibia kila Kona
 
Kote nimekaa tena chuga nilipofika kishua ila nimezunguka mjini chuga kwa mwanza bado sana mwanza mji mkubwa una maendeleo halafu town hamna watu kwanza facilities nyingi kuliko watu ili kundi kubwa lipo nje ya mji

Chuga sasa pamebanan mno watu wake kama wezi yaani unaweza kujshtuki kama utakabwa
Ok.na Mimi niseme maoni yangu
Kwetu singida center so nimepata bahati ya kutembea na kuishi kwa zaidi ya miezi mitatu mikoa tajwa
Mwanza iko vizuri kuliko arusha







Natamani niandike maneno mengi ila itaonekana blah blah na me sipendi blah blah
Ila mchambuzi umechambua vizuri kiasi chake nakupa 70%---80%

Nifafanulie kwenye beach za mito....ziko mto gani themi au?
Wa kisure
 
Umeandika uharo mtupu. Eti Arusha iko karibu na Serengeti ! Unalinganisha kijiji cha wavuta bangi na jiji la Mwanza. Tena ukome kabisa.
Hii nishida ya kuzaliwa na kuzeekea eneo 1, pinga kwa hoja na acha kubwabwaja.
 
Fursa gani mlizokamata Mwanza nyie ? Tai five hotel mmemuuzia msukuma ! Ebu niambie mlichanacho kwenye hilo Jiji la pili. Kwa ukubwa TZ. Ninyi ni wachuuzi wa mayai na viduka uchwara.
Wanakanda ya ziwa Bado wamelala watu wa kaskazini wanakamata fursa karibia kila Kona
 
Fursa gani mlizokamata Mwanza nyie ? Tai five hotel mmemuuzia msukuma ! Ebu niambie mlichanacho kwenye hilo Jiji la pili. Kwa ukubwa TZ. Ninyi ni wachuuzi wa mayai na viduka uchwara.
Ukweli mnujua Moyoni kuwa watu wa kaskazini ndio madoni huko Mwanza na Tanzania kwa ujumla, ona eti tajiri wenu Wasukuma ni Mhe. Msukuma
 
Back
Top Bottom