Hitilafu kwenye ndege

Red Scorpion

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,736
4,252
Msamaha wa kweli unahitaji Neema ya Mungu. Sikiliza hii,

Kuna jamaa mmoja na Mkewe walikuwa wanasafiri kuelekea Italia kwa safari ya kibiashara kwa ndege. Wakiwa angani likatoka tangazo kwamba injini zote za ndege hazifanyi kazi sawasawa hivyo muda si mrefu ile ndege itadondoka, hivyo kuwasihi abiria kuomba sana pamoja na kutubu kwa ajili ya kujiandaa na kifo ambacho kwa vyovyote kilikuwa hakiepukiki.

Yule jamaa akamgusa mkewe na kumwambia, honey naomba unisamehe maana yule mdogo wako tunayeishi nae amekuwa mpenzi wangu kwa muda mrefu sana, na tayari ameshatoa mimba nyingi tu, na tulikuwa na mpango wa kukuua. Hivyo naomba unisamehe.

Mkewe akamjibu, hakuna tatizo dear nimeshakusamehe, kwa kuwa ni kipindi cha kutubu basi ngoja na mimi nikiri mbele yako uovu niliokutendea. John na Esther sio watoto wako, mtoto wako ni Victoria, pia siku ile ulivyoporwa fedha na majambazi, mimi ndiye niliyeandaa huo mpango ili nilipie ada ya Chuo ya mpenzi wangu Juma, hata sasa nilikuwa na mpango wa kukuua ili nirithi mali. Jamaa akamwambia mkewe nimekusamehe.

Wakati huo huo, tangazo likatoka kwamba, tunashukuru abiria kwa maombi yenu, Mungu ametusikia na sasa tunauhakika wa kufika salama safari yetu, Asanteni sana. Pamoja na tangazo hilo ambalo lingewafanya wafurahi, lakini abiria wote walikuwa kimya. Ndipo yule jamaa alipopaza sauti rubani! rubani! lazima uiteketeze hii ndege ukishindwa tutaiteketeza wenyewe.

Abiria wote wakajibu kwa pamoja, ndioooooooooooo!!
 
Back
Top Bottom