Mwanzoni tuliona mistari mistari tu... Na kwa hakika hatukujua kama ni mchoro wa nini, na umeanzia wapi.... Lakini akapotoea Ben Saanane,! Ya kamanda Mawazo na Mwangosi yanajulikana yako wazi kabisa
Picha iakendelea kujichora taratibu, zikaja maiti za ruvu.. Mambo yakazidi kusonga.... Watu wakawa wanatishiwa maisha live, kufuatiliwa na kudukuliwa mawasiliano yao
Picha ikaanza kujitokeza formation yake... Tuliodhani ni picha tu ya kawaida ya pundamilia tukabaki midomo wazi baada ya kugundua ni lipicha litishalo sana la dubwana kubwa lenye maguvu mengi na katili kabisa
LIssu akamiminiwa risasi za kutosha, Mungu ni mwema... Lissu kasalimika japo kabaki na majeraha makubwa
Kalamu ya picha letu tuliiona wino wake na wachoraji wake siku Nape alipotolewa cha moto live.....
Picha letu limekamilika sasa bado kutia sahihi tu na kukoleza rangi
Kila kitu kiko hadharani sasa waliongozwa na ukatili wakasahau weledi katika kutimiza ukatili wao.. Wameacha alama kila walikopita na picha imekamika... Tukae mkao wa kuiona picha yetu katika uhalisia wake
Kila nikitaka kuchangia kii bodi inagoma duh... ngoja nirekebishe nitarudi