Historia Yenye Ukakasi Kuhusu Uanzishwaji wa Taifa la Israel

musacha

Senior Member
Sep 21, 2012
185
250
Wakuu wanajukwaa salaam kwenu.
Binafsi napenda kutambua mchango wa wadau mashuhuri wa jukwaa hili, nikiwataja kwa uchache The bold , MSEZA MKULU , barafu na wengineo wengi ambao kwa kiasi kikubwa mmekuwa mkitoa chambuzi za kihistoria ambazo ni fikirishi lakini pia zinapanua ufahamu na kuburudisha. Hongereni sana.

Binafsi baada ya kusoma machapisho mbalimbali ya kiintelejensia ambayo mmekuwa mkutuletea hapa jukwaani, leo nimeshawishika kuomba kwa hisani yenu mtuletee chapisho la kiintelejensia kuhusu ukweli wa uanzishwaji wa taifa la Israel.

chapisho hilo likijibu maswali yafuatayo itakuwa vyema.
1. Je ni kweli kwamba taifa la Israel ni taifa mkakati lililoanzishwa ili kukabiliana na nguvu ya Urusi huko mashariki ya kati?

2. Je ni kweli kuwa kabla ya kulianziasha taifa hilo huko mashariki ya kati, kuna wakati walifikiria kulianzisha katika nchi ya Uganda? Je ilikuwaje?

3. Nini tofauti kati ya wazayuni (Zionists) na Wayahudi (Jewish)?

4.Nini kilitokea hata kupelekea mauaji ya wayahudi/waisrael kule German? Kuna habari kuwa Rothschild family ambao originally ni jews ndo walikuwa nyuma ya yale mauaji na pamoja na kwamba wao ni jews wenyewe pamoja na miradi yao hawakuathirika na udikteta wa Hitler, na kuna tetesi kuwa hata Hitler a.k.a Alois alitoka katika familia hiyo. Je ni kweli?

5. Hawa wayahudi/israel walitokea wapi mpaka wakatapakaa katika nchi za ulaya na Marekani?

6. Kuna uhusiano gani wa siri kati ya israel na marekani? Je kuna/iliwahi kutokea influence yoyote ya Israel ndani ya Russia?

Wakuu nitafurahi sana kama nitapata maandiko yenu juu ya issue hizo.

Wasalaam
 
Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,374
2,000
Historia ya Israel ina mkanganyiko wa Kidini na Kihistoria....

Ila kwa kupanua tu akili ngoja nikupe hint moja makini sana kama wewe ni msomaji wa vitabu vya dini na historia kwa kina.

Israel ya zamani iliundwa na makabila 12, lakini baadaye ilimeguka na kuwa mataifa mawili moja likiitwa Kabila la Yuda+Nusu ya kabila la Benjamini na jingine likiitwa Israel(makabila 11).

Sasa Israel ya sasa ambayo tunainasibisha sana na Uyahudi japo wengi hawajui kiini chake hasa ni lile kabila moja la Yuda + nusu ya Benjamini, makabila mengine yale 11 japo si yote yalitapakaa sana duniani na kuna mataifa mengi makubwa tu duniani hapa ambayo yalianzishwa na hayo makabila 11 yaliyotapakaa.

Mwenye akili na afahamu hili.
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Historia ya taifa la Israel inaanzia kwenye Biblia,hakuna Israeli bila biblia...

Taifa hili linaanzia pale ambapo Ibrahimu ananunua eneo ambalo baadaye lilikuja kujulikana nkama Kanaani...

Wanaoitwa Waisraeli leo wanatokana na jina Israeli ambalo alipewa Yakobo na malaika baada ya kushindana naye na wanae wakaitwa waana wa Israeli...

Waisraeli yaani watoto wa Yakobo walianza baada ya Yakobo kuzaa watoto 12 kutoka kwa wanawake watatu tofauti...

Hii Israeli ya leo siyo ile ya kale na hawa waisraeli wa leo siyo wale wa kale...

Neno Wayahudi linatokana na neno au jina Yuda ambalo ni jina la mmoja wa watoto wa Yakobo.Jina hili lilikuwa maarufu sana baada ya Israeli kugawanyika na kupatikana Israeli 2 miaka 675 kabla ya Kristo...

Baada ya mgawanyiko huu zikapatikana nchi mbili..

1;Israeli iliyokuwa na makabila 10
2;Yudea iliyokuwa na makabila 2 ambayo ni Yuda na Benjamin..

Nchi hii ya Yudea iliitwa Yudea kwasababu ya wingi wa watoto wa Yuda waliounda kabila hilo tofauti na Benjamin waliokuwa wachache....

Waisraeli walianza kumuasi Mungu na waliadhibiwa kwa kutawaliwa na Waashuru na kuanzi hapo historia yao ikaanza kufutika na hawakujulikana walikwenda wapi...

Wayuda au Wayahudi waliendelea kudumu katika agano la Mungu na huko ndipo alipozaliwa Kristo na wakati Ksristo anakuja ulimwenguni alikuta Waisraeli hawajulikali walipokwenda na ndiyo maana alisema "sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli" hii inaonesha walikuwa "wamepotea" kimwili na kiroho....

Mwaka 70 A.D,Warumi walipoivamia Jerusalem na kulisambaratisha hekalu waliwaua Wayahudi wengi sana na kusababisha wengine kukimbia nchi yao wenyewe ya Yuda [Israeli ya kusini] na kuanzia hapo haikujulikana walienda wapi kwa mujibu wa historia inayokubaliwa na wakubwa wa dunia

Hakuna ushahidi wowote kuwa Wayuda waliokuwa wanaunda taifa la Yudea walikimbilia Ulaya na kuna ugumu mkubwa sana kwa jambo hili kutokea kwasababu ni vigumu mtu akufukuze kwako halafu wewe ukimbilie kwake tena nyumbani kwake.Ni ngumu sana Wayahudi wafurushwe na Warumi halafu wakimbilie Ulaya ambako ni kama nyumbani kwa Warumi....

Kuna ushahidi mkubwa unaonesha kwamba hawa Wayahudi walikimbilia Afrika hasa Afrika ya magharibi na wengine mashariki mwa Afrika.Jambo hili halikubaliwi kabisa na wakubwa wa dunia...

Kwasababu hii,hawa ambao leo tunaambiwa ni wayahudi historia inawakataa kwakuwa walitoka Ulaya na hakuna ushahidi kuwa Wayahudi waliotoka Yudea walikimbilia ulaya maana huko wangemwalizwa zaidi...

Daha ya Wayahudi kukimbilia ulaya ni ngumu sana kukubalika...
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Mkuu vipi dhana ya kwamba walikimbilia Asia? Au kama walikimbilia huku Afrika hawakuendeleza taratibu zao za kimila ambazo zingewatofautisha na wengine? Kama vile dini yao ya kiyahudi.
[HASHTAG]#Eiyer[/HASHTAG]
Dhana ya hawa watu kukimbilia Asia nayo haina ushahidi wa kihistoria kama kukimbilia huku na kuna sababu...

Kwanza Wayahudi na wakazi wote wa eneo la mashariki ya kati wote walikuwa weusi,weupe waarabu unaowaona pale walitoka Uturuki huko ndiyo wakaja pale na kuanza kuwafukuza weusi na kuwaua...

Kwa kifupi maeneo yote ya mashariki ya kati yalikaliwa na watu wesi kabisa na kuna mtaalam mmoja wa mambo ya kale anasema kwamba hakuna kitu kama "midle east" kwasababu haipo,ile inayosemwa kuwa ni middle east ni North east Afrika na ilikuwa ni sehemu ya Afrika kabla ya uvamizi wa weupe...

Anasema dhana ya "Asia Minor" nayo ni ujinga tu,kwanini hakuna Africa minor" au America minor"? Jamaa mule amehoji mambo mengi sana yanayoweza kukuonesha kuwa kuna ujanja ujanja mwingi sana...

Sasa tukiichukua hii ya hawa wakazi wa eneo hilo kuwa weusi utaona tu kwamba eneo ambalo watu hao waliona kuna "wenzao" ni huku Afrika na siyo eneo lingine lolote kwa kuwa wanafanana hata kimuonekano...

Kuna ushahidi mwingi sana wa kuonesha Wayahudi walikuja huku Afrika badala ya eneo lingine lolote duniani.Kuna kushabihiana kukubwa kwa lugha za Kibantu na lugha ya Kiebrania tena cha kale,kuna kushabihiana sana kwa tamaduni za makabila hayo na tamaduni za Kiebrania za kale kabisa,kuna kushabihiana kwa majina pia...

Mambo ni mengi ukifanua tu utafiti wa kawaida na utayaona....
 
Ficus

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
1,448
2,000
Nashukuru kwa maelezo yako mujarabu, hili la kushabiana lugha ya kibantu na kiebrania, majina na tamaduni sikuwahi lisikia kabisa nafikiria kufanya utafiti wangu binafsi kuthibitisha.
Asante kwa kunifungua walau kidogo.
[HASHTAG]#Eiyer[/HASHTAG]
 
Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,343
2,000
kati ya nchi zote Africa kwanini waliitizama Uganda na sio Nigeria, Ghana, Rhodesia zenye vitu vya thamani geographically.
 
afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,924
2,000
Huku [HASHTAG]#The[/HASHTAG] bold# hajapita ili atuletee kitu chenye utafiti? Naona #Eiyer# amemwaga vitu vya kuanzia japokuwa mtoa mada alieleza vitu vingi vya kutembea navyo ktk mada, karibuni wajuvi mjikite ktk maeneo mahususi ya mtoa post
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
16,451
2,000
1. Je ni kweli kwamba taifa la Israel ni taifa mkakati lililoanzishwa ili kukabiliana na nguvu ya Urusi huko mashariki ya kati?

2. Je ni kweli kuwa kabla ya kulianziasha taifa hilo huko mashariki ya kati, kuna wakati walifikiria kulianzisha katika nchi ya Uganda? Je ilikuwaje?

3. Nini tofauti kati ya wazayuni (Zionists) na Wayahudi (Jewish)?

4.Nini kilitokea hata kupelekea mauaji ya wayahudi/waisrael kule German? Kuna habari kuwa Rothschild family ambao originally ni jews ndo walikuwa nyuma ya yale mauaji na pamoja na kwamba wao ni jews wenyewe pamoja na miradi yao hawakuathirika na udikteta wa Hitler, na kuna tetesi kuwa hata Hitler a.k.a Alois alitoka katika familia hiyo. Je ni kweli?

5. Hawa wayahudi/israel walitokea wapi mpaka wakatapakaa katika nchi za ulaya na Marekani?

6. Kuna uhusiano gani wa siri kati ya israel na marekani? Je kuna/iliwahi kutokea influence yoyote ya Israel ndani ya Russia?

Wakuu nitafurahi sana kama nitapata maandiko yenu juu ya issue hizo.

Wasalaam

Mkuu hii mada uliyoanzisha ina mdahalo mkubwa sana,
Japo nitajitahidi kukujibu kwa kadiri ya Uwezo na Mtizamo wangu.
Hivyo basi naomba usininikuu hata kidogo.

1. Je, ni kweli kwamba taifa la Israel ni taifa mkakati lililoanzishwa ili kukabiliana na nguvu ya Urusi huko mashariki ya kati ?

-Jibu ni Hapana, kwasababu Taifa la Israel liliundwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948, ambapo kura zilipigwa tarehe 29 November 1947. Urusi ya Kisovyeti , Marekani na Uingereza ndiyo waliyopiga sana debe Taifa hilo liundwe.

- Kipindi hicho Wayahudi walikuwa wanaonewa huruma na mataifa karibia yote duniani kwasababu ya Mauji yao ya Halaiki yaliyofanywa na Wanazai huko Auschwitz nchini Polandi. Kulikuwa na uvumi kwamba ili jambo kama hilo lisiwakute tena Wayahudi ni lazima watafutiwe nchi yao ya kuishi.

- Upande wa pili ni lazima Ukumbuke kwamba Wayahudi ndiyo waliongoza Mapinduzi ya Kikomunisti nchini Urusi mwaka 1917 na walikuwa mstari wa mbele kwenye kupigana Vita ya pili ya dunia dhidi ya genge la Mafashisti hivyo ushawishi wao huo ulifanya Warusi na Wamarekani wakubali kirahisi kutengeneza hilo taifa.

-Mwisho kabisa, dhana ya kurudi nchini Israeli ilizaliwa tangu zamani hata kabla ya kuwepo Marekani na Urusi. Kubwa zaidi Wazayuni kama wakina Theodore Hertz ndiyo waliyoipigia sana chapuo mnamo miaka ya 1800's.

NB: Japo siku zilivyoenda mbele Mataifa makubwa yalitumia hili suala kama njia ya kueneza ushawishi wao katika eneo la Mashariki ya Kati. Kila taifa kubwa lilitegemea Israeli atakuwa upande wake, hivyo vita baridi ilivyoanza Marekani alitumia Israeli kama mlango wake wa kuzuia maslahi ya Urusi pale Mashariki ya kati. Huu mkakati uliitwa CONTAINMENT POLICY na ulisukwa na Raisi Harry S Truman. Mfano Mzuri tu hata Ujerumani iligawanywa kuwa mataifa mawili adui kwasababu tu hawa wakubwa walivutana. Hili lilienda kuanzia:

  • India (Upande wa Urusi) Vs Pakistani (Upande wa Marekani)
  • Korea Kaskazini (Upande wa Urusi) Vs Korea Kusini (Upande wa Marekani)
  • Vietnam Kaskazini (Upande wa Urusi) Vs Vietnman Kusini (Upande wa Marekani)
  • China (Upande wa Urusi) Vs Taiwan (Upande wa Marekani)
Hivyo hata pale Mashariki ya Kati ilikuwa vivyo hivyo: Ukweli ni kwamba mpango huu ulikuwepo tangu muda lakini mataifa makubwa yalikuwa na Maslahi yake binafsi (wote walitaka kutawala vyanzo vya mafuta) hivyo kila mtu alitegemea Israeli atakuwa swahiba wake.

2. Je, ni kweli kuwa kabla ya kulianziasha taifa hilo huko mashariki ya kati, kuna wakati walifikiria kulianzisha katika nchi ya Uganda? Je ilikuwaje?

- Ndiyo, Wayahudi baada ya kuona kuwa wanateswa sana huko Ulaya walimuomba swahiba wao Uingereza awatafutie nchi ya kukaa. Wazayuni walitaka Kurudi Palestina lakini ikashindikana kwasababu Mashariki ya Kati ilikuwa chini ya Dola la Kiislamu la Uturuki tokea Karne ya 15 hadi Karne ya 20 baada ya kuisha Vita ya Kwanza ya dunia mwaka 1919. Muingereza aliona ni vyema Wayahudi wapelekwe kwenye baadhi ya maeneo ya makoloni ya Uingereza kama Uganda. Wajerumani walifikiria kuwapeleka Madagascar. Hebu pitia hapa:Naomba kujua historia ya Urusi

3. Nini tofauti kati ya Wazayuni (Zionists) na Wayahudi (Jews)?

- Tofauti ni kubwa sana, Uzayuni ni mfumo wa Kisiasa na Uyahudi ni mfumo wa Kidini na Kitamaduni.
Uzayuni ni Mfumo ulioanzishwa na Myahudi anayeitwa Theodore Hertz mnamo miaka ya 1800's ambao unasema ni lazima Wayahudi warudi Sayuni (Mji wa baba yao Daudi). Huku Uyahudi ni dini yenye mizizi ya Kiebrania inayotaka mtu amuabudu MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo tu. (Hata wewe unaweza kuwa Myahudi ukitaka, Mfano. Watoto wa Trump wote wanaabudu dini ya Kiyahudi)

- Professor John Mearshimer kwenye Essay yake inayoitwa "The Israel Lobby" anasema siku hizi mtu yoyote anaweza kuwa Mzayuni (Zionist). Akasema mtu yeyote anayekubaliana na Siasa na sera za nchi ya Israeli ni Mzayuni. Mfano Mzuri ni wale Walokole wa Marekani pamoja na Neo-Cons wote ni Wazayuni. Unaweza kupitia hapa kuipata:http://mearsheimer.uchicago.edu/pdfs/IsraelLobby.pdf

4. Nini kilitokea hata kupelekea mauaji ya wayahudi/waisrael kule German? Kuna habari kuwa Rothschild family ambao originally ni jews ndo walikuwa nyuma ya yale mauaji na pamoja na kwamba wao ni jews wenyewe pamoja na miradi yao hawakuathirika na udikteta wa Hitler, na kuna tetesi kuwa hata Hitler a.k.a Alois alitoka katika familia hiyo. Je ni kweli?

-Mauaji ya Wayahudi yana Historia ndefu kidogo, lakini kwa sababu hasa iliyopelekea Wayahudi kuuwawa kwa kiasi kikubwa ni Vita ya Kwanza ya dunia na Ukomunisti wa Urusi. Ikumbukwe Wayahudi wengi walikuwa wakiishi Ujerumani, Ufaransa, Poland, Yukreini na Urusi. Wakati vita ya kwanza ya dunia inaendelea vugu-vugu la Uzayuni lilikuwa limepamba moto. Wazayuni walimshauri Waziri mkuu wa Uingereza kwamba atoe tamko linalosema endapo Wayahudi watajiunga na Triple Entente (Uingereza, Ufaransa,Urusi na Marekani ) dhidi ya Triple Alliance (Ujerumani, Italia , Austria, Ottoman Empire, Bulgaria) basi Uingereza wangewapa Wazayuni nchi yao kule Mashariki ya kati. Tamko hilo lilitwa The Balfour Declaration. Pitia hapa kulisoma:Text of the Balfour Declaration

-Bahati mbaya Wayahudi wengi walikuwa jeshini Ujerumani na hivyo walisaidia kuvujisha siri nyingi za kijeshi za Ujerumani. Kwa upande wa pili Wazayuni Walisaidia Uingereza na Ufaransa kusaini mkataba wa siri uitwao Sykes-Picot Agreement wa mwaka 1916 ambao ulisema kwamba baada ya vita ni lazima watagawana Ufalme wa Uturuki (The Ottoman Empire) hivyo maeneo mengi ya Mashariki ya kati yangekuwa huru hivyo Waarabu na Wayahudi wangepata nchi yao. Huu mkataba ulipewa Baraka zote na Wazayuni matajiri mfano Familia ya Rothschild. Huu mkataba ulivujishwa na Wakomunisti na ukaonyesha na ukadhihirishia dunia kwamba Wayahudi wanafadhili mbinu chafu ili kuhujumu mataifa makubwa. Pitia hapa uusome huo mkataba: Sykes-Picot Agreement | 1916

- Upande mwengine Vita ya Kwanza imeisha Wajerumani na mataifa mengine wakawalaumu sana Wayahudi kwamba wao ni Wasaliti. Kibaya zaidi Ukomunisti uliingia hadi Ujerumani na Ujerumani ikawa masikini sana. Ikumbukwe waliokuwa wanaeneza Ukomunisti wa Urusi walikuwa ni Wayahudi kama Vladmir Illych Ulyanov Lenin, Leon Trotsky, Felix Dzerzhinsky n.k. Baada ya wakina Lenin kumuua Mfalme Alexander Ramanov wa Pili wa Urusi pamoja na familia yake yote dunia ikazidi kuwachukia Wayahudi. Hii ni moja ya sababu Hitler alivamia Urusi kwa nguvu sana.

-Hilo la Adolf Hitler kuwa mjukuu wa Rothschild halina ushahidi wowote wa kitaaluma hivyo naomba tusilizungumzie kabisa.

5. Hawa wayahudi/israel walitokea wapi mpaka wakatapakaa katika nchi za ulaya na Marekani?

-Hii hoja ya Wayahudi kuwepo Ulaya inapingwa sana na wengi lakini nadhani kuna sehemu kubwa sana ya Historia tunaisahau kabisa. Wengine wanasema kule kuna umbali sana, hivyo Wayahudi wasingeweza kukimbilia Ulaya. Lakini ni lazima tukumbuke kwamba Israeli ilikuwa ni koloni la dola la Mrumi kwa zaidi ya Miaka 500. Hivyo wazungu walikuwepo sana pale,hata Pilato aliyemuhuku Bwana Yesu alikuwa ni Mzungu. Mtume Paulo alishawahi kwenda kuhukumiwa mbele ya Kaisari huko Rumi, sehemu yenye umbali mkubwa kabisa na Yerusalemu.

-Hivyo kama Ulaya,Afrika na Asia ilikuwa ni nchi moja chini ya Rumi kwanini Wayahudi wasiweze kusafiri kwenda Ulaya? Ukisoma hata kwenye Biblia utaona jinsi mitume Wayahudi wengi walivyoenda kuishi Uyunani(Ugiriki), Misri (Bwana Yesu na familia yake walifika hadi Misri) na Rumi. Hivyo walianza kwenda Ulaya wakati wa nyuma kidogo.

-Upande wa Pili baada ya dola la Rumi kuanguka Waislamu walitawala Mashariki ya kati yote ile: Lakini kuanzia karne ya kumi na moja hadi kumi na mbili kulikuwa na Vita za kidini Al-Maaruf kama Crusades ambazo Kanisa la Katoliki chini ya Baba Mtakatifu Urban wa Pili walizianzisha. Walisema wanataka kuwaondoa Waislamu kwenye eneo lao Mji Mtakatifu (The Holy Land). Hivyo wazungu wengi walitoka Ulaya akiwemo Mfalme wa Uingereza Richard The Lion Heart. Kipindi hiki Sultani wa Mashariki ya Kati na Afrika aliitwa Salahadeen ambaye aliwashinda Wayahudi na kuitwaa Yerusalemu hivyo Wayahudi wengi waliondoka na wale wapiganaji wa mataifa ya Ulaya.

- Kuhusu Wayahudi kuwepo Marekani ni swali lisilokuwa na mashiko sana kwasababu Marekani ni nchi ya Wageni. Imejengwa na watu wenye Asili ya Ufaransa, Italia, Irishi, Uingereza, Uhispania n.k. Kwanza kabisa ni lazima Ujue Wayahudi wengi waliishi Uingereza na Marekani lilikuwa koloni la Muingereza, hivyo kama walivyofanya Wazungu Wayahudi nao walienda kutafuta maisha nchini Marekani wakati bado ni koloni. Ikumbukwe Uingereza ilishawahi kuwa na Waziri mkuu Muisraeli aliyeitwa Benjamin Disraeli hivyo walikuwepo sana Uingereza hata kabla ya Marekani kupata Uhuru. Pili Wayahudi wengi walikimbilia Marekani baada ya Uhuru kwasababu The New World was the Land of Opportunity tofauti na Ulaya kwenye manyanyaso. Walienda kwa Awamu tatu,hebu soma hapa:Jewish Immigration to America: Three Waves | My Jewish Learning

NB: Sababu ni nyingi sana lakini naomba niishie hapa na nikuachie maswali ya kufikiria:

  • Wangoni kwao ni Afrika Kusini lakini walifikaje hapa Tanzania?
  • Watutsi kwao ni Ethiopia lakini walifikaje pale Rwanda?
  • Kabila la Wairaki wanatokea huko Mashariki ya kati lakini walifikaje pale Manyara?
  • Marekani yote ni Bara la Wahindi Wekundu lakini Mbona inakaliwa na Wazungu?
  • Misri ya zamani ilikaliwa na Weusi lakini mbona leo Waarabu wamejaa?

6. Kuna uhusiano gani wa siri kati ya israel na marekani? Je kuna/iliwahi kutokea influence yoyote ya Israel ndani ya Russia?

- Hilo la Marekani nimeshakujibu tayari: Ila hili la Urusi nasema NDIYO KUBWA kabisa.
Ushawishi wa Wayahudi ni mkubwa sana huko Urusi na Ushahidi wa hili uko wazi kabisa. Kumbuka sera ya Ukomunisti ni sera ya Myahudi Karl Marx na ilipigiwa chapeo na Wabolsheviki wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 1917.

- Niseme tu haya yafuatayo:
1. Baba wa taifa la Urusi ya Kisovyeti alikuwa ni Myahudi Vladmir Illych Ulyanov Lenin.
2. Muasisi wa jeshi la Urusi na mifumo yake mle ndani alikuwa ni Myahudi Leon Trotsky.
3. Muasisi wa K.G.B (Shirika la kipelelezi) kipindi hicho ni The Cheka alikuwa Myahudi Felix Dzerzhinsky.
4. Mzee Yevgeny Primakov alikuwa Waziri Mkuu kipindi cha Boris Yeltsin.
5. Waziri wa Ulinzi wa Israeli Bwana Avigdor Lieberman alizaliwa Urusi baba yake akiwa mwanajeshi kule.

Orodha ni ndefu sana lakini hata Waziri Mkuu wa Uingereza Bwana Winston Churchill alishawahi kusema yafuatayo kuhusu Wayahudi, Ukomunisti na Urusi. Pitia hapa umsome: Some people like them, some don't

CC: izzo , Kingdom_man , culture gal , Red Giant
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Malcom Lumumba ,

Nimelipitia hilo bango lako hapo juu lipo vizuri...

Nafanya mchakato wa kuandika makala moja na nadhani itakuwa ndefu sana ambayo itajibu kwa kina kidogo masuala ya vita ya pili na mengi sana kuhusiana na uliyoyajadili hapo...

Ngoja tuombe uzima na nadhani tutaweza kuwa na mjadala mzuri zaidi hapo mkuu kuhusiana na yote hayo maana yana impact kubwa sana kwenye shape ya historia na maisha ya leo....

Shukran sana mkuu...
 
holygrail

JF-Expert Member
Mar 24, 2012
1,251
1,500
Historia ya taifa la Israel inaanzia kwenye Biblia,hakuna Israeli bila biblia...

Taifa hili linaanzia pale ambapo Ibrahimu ananunua eneo ambalo baadaye lilikuja kujulikana nkama Kanaani...

Wanaoitwa Waisraeli leo wanatokana na jina Israeli ambalo alipewa Yakobo na malaika baada ya kushindana naye na wanae wakaitwa waana wa Israeli...

Waisraeli yaani watoto wa Yakobo walianza baada ya Yakobo kuzaa watoto 12 kutoka kwa wanawake watatu tofauti...

Hii Israeli ya leo siyo ile ya kale na hawa waisraeli wa leo siyo wale wa kale...

Neno Wayahudi linatokana na neno au jina Yuda ambalo ni jina la mmoja wa watoto wa Yakobo.Jina hili lilikuwa maarufu sana baada ya Israeli kugawanyika na kupatikana Israeli 2 miaka 675 kabla ya Kristo...

Baada ya mgawanyiko huu zikapatikana nchi mbili..

1;Israeli iliyokuwa na makabila 10
2;Yudea iliyokuwa na makabila 2 ambayo ni Yuda na Benjamin..

Nchi hii ya Yudea iliitwa Yudea kwasababu ya wingi wa watoto wa Yuda waliounda kabila hilo tofauti na Benjamin waliokuwa wachache....

Waisraeli walianza kumuasi Mungu na waliadhibiwa kwa kutawaliwa na Waashuru na kuanzi hapo historia yao ikaanza kufutika na hawakujulikana walikwenda wapi...

Wayuda au Wayahudi waliendelea kudumu katika agano la Mungu na huko ndipo alipozaliwa Kristo na wakati Ksristo anakuja ulimwenguni alikuta Waisraeli hawajulikali walipokwenda na ndiyo maana alisema "sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli" hii inaonesha walikuwa "wamepotea" kimwili na kiroho....

Mwaka 70 A.D,Warumi walipoivamia Jerusalem na kulisambaratisha hekalu waliwaua Wayahudi wengi sana na kusababisha wengine kukimbia nchi yao wenyewe ya Yuda [Israeli ya kusini] na kuanzia hapo haikujulikana walienda wapi kwa mujibu wa historia inayokubaliwa na wakubwa wa dunia

Hakuna ushahidi wowote kuwa Wayuda waliokuwa wanaunda taifa la Yudea walikimbilia Ulaya na kuna ugumu mkubwa sana kwa jambo hili kutokea kwasababu ni vigumu mtu akufukuze kwako halafu wewe ukimbilie kwake tena nyumbani kwake.Ni ngumu sana Wayahudi wafurushwe na Warumi halafu wakimbilie Ulaya ambako ni kama nyumbani kwa Warumi....

Kuna ushahidi mkubwa unaonesha kwamba hawa Wayahudi walikimbilia Afrika hasa Afrika ya magharibi na wengine mashariki mwa Afrika.Jambo hili halikubaliwi kabisa na wakubwa wa dunia...

Kwasababu hii,hawa ambao leo tunaambiwa ni wayahudi historia inawakataa kwakuwa walitoka Ulaya na hakuna ushahidi kuwa Wayahudi waliotoka Yudea walikimbilia ulaya maana huko wangemwalizwa zaidi...

Daha ya Wayahudi kukimbilia ulaya ni ngumu sana kukubalika...
Not convincing enough. The mighty bold would have gone extra mile. You are trying hard but you will never touch the bold heights. Kuwa msomaji kama mimi.
 
holygrail

JF-Expert Member
Mar 24, 2012
1,251
1,500
Hah ah hahaha mkuu kwani Hapa kuna ushindani between kaka Eiyer na Bold au topic iko jukwaani watu wachangie
Comment yako sio nzuri ndugu yangu
Tunataka nondo zilizoshiba utafiti na ujazo. His majest the king bold rules jf intelligence kingdom. We are his loyal subjects. Hail to the king!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom