Historia ya Zelothe inaonesha alikuwa RPC akiwa na Miaka 66. Je, ndivyo ilivyo?

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Kila mtu Kila mtaani anajua Umri wa kustaafu Kwa mtumishi wa Umma ni miaka 60, Tena Kwa majeshi Huwa ni kidogo zaidi.

Napenda kujifunza , kifo Cha mwenyekiti wa CCM Arusha ambaye alishatumikia jeshi la polisi ngazi za uandamizi kimenofanya nijiulize mambo mawili matatu, wakati wa usomwaji wa historia ya Zelothe imeonesha kuwa mpaka akiwa na Miaka 66 alikuwa bado ni RPC.

Sijajua je hii ni kutokana na uhusiano wake wa karibu na CCM au Kuna lingine, Kwa maana pia vijana wake wapo kwenye system, wakurugenzi n.k

Hili jambo linafanana na Kiongozi mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Kusini ndugu wa Majaliwa Kasim ambaye ameshafikisha Umri wa kustaafu miaka kadhaa nyuma lakini bado yupo ofisini , kwa kuwa ana god father PM.

Je utaratibu ni upo, hakuna mtu anaependa kustaafu na kuacha mshahara, tuambieni jinsi ya kijiongezea muda
 
Yawezekana kwao watu wenye vyeo vikubwa vikubwa, kustaafu kwao ni tofauti na wadogo.
 
Sina uhakika sana... Narudia sina uhakika sana... Katika majeshi kila cheo kina miaka yake yakukitumikia... kama una miaka 58 ukapandishwa cheo hapo jumlisha mitano kwa askari wa kawaida... sijajua kwa maboss wa juu wanaongezewaga mingapi kwa kila anapopanda cheo.
 
Mfugale alikufa akiwa na miaka 65+ na alikua bado anapokea mshahara. Mfugale hakua mwanasiasa,
Twende CCM Sasa. Sitaki kumtaja mtu. Lakini CCM hakuna umri wa kustaafu hata waliostaafu bado tunawaona wakipiga kasi.
 
Mfugale alikufa akiwa na miaka 65+ na alikua bado anapokea mshahara. Mfugale hakua mwanasiasa,
Twende CCM Sasa. Sitaki kumtaja mtu. Lakini CCM hakuna umri wa kustaafu hata waliostaafu bado tunawaona wakipiga kasi.
Mzee wa Msoga
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Muliro Jumanne alishafikisha umri wa kustaafu,lakini mwezi Mei nadhani kwaka huu alipandishwa Cheo kutoka Kamishna Msaidizi(ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi(SACP) na akaongezewa muda wa kuendelea kuwa Kamanda Kanda Maalum Dar es Salaam,hivyo ni kawaida iwapo wakubwa wako itawapendeza kukuongezea muda wakati wanaandaa wa kukurithi
 
Back
Top Bottom