Historia ya wimbo "Usinipite Mwokozi" tenzi namba 10

vincentmwakisyala

New Member
Jan 30, 2023
3
35
Na Vincent Mwakisyala

Wimbo huu wa usinipite ni moja kati ya nyimbo za kikristo maarufu sana Duniani. Na wimbo huu unaimbwa Na madhehebu karibu yote. Ni wimbo wa maombi, una ujumbe uliotulia, Na una tafakari itakayokuvuta kwa Mungu moja kwa moja. Nikitafakari wimbo huu namkumbuka yule mgonjwa wa Kisima cha Belshaza. YOHANA 5. Kabla ya yote hebu tumuangalie kwanza muhandishi kama ilivyo ada.

HISTORIAN YA MWANDISHI
Mwandishi wa wimbo huu maarufu anaitwa FRANCES JANE CROSBY na alizaliwa kaunti ya Putnam, New York, March 24, 1820 na kufariki katika umri mwema wa miaka 95 mwaka1915.

Majuma kati ya sita hadi nane tu, baada ya kuzaliwa Daktari asiye na ujuzi alimfunika macho na plasta ya kemikali kimakosa, kitendo kilichomsababishia upofu wa kudumu. Upofu alioishi nao tangu akiwa Na wiki 6 mpaka maisha yake yote aliishi gizani, akuweza kuona tena, Na aliishi miaka 95. Kwa makosa ya daktari yalimsababishia asione maishani.

Pamoja na upofu aliokuwa nao bado Fanny Crosby aliweza kugundua kuwa alikuwa na karama ya kipekee ambayo Mungu alimjalia na alifurahia sana kuitumikia karama yake ya utunzi wa Nyimbo za tenzi na injili na mara nyingi alipendelea kusema,"Nina vitu vya thamani sana ndani yangu"

Alipokuwa na miaka tisa tu,aliandika maneno yafuatayo:
"Ni jinsi gani nafsi yangu ilivyo na furaha,Ingawa sioni,
Nimeridhika kuwa katika dunia hii, Nitaishi kwa furaha,
Ni baraka ngapi ninazifurahia
Watu wengine wamezikosa?
Kulia na kujuta Kwasababu ya upofu?
Sitaweza, na wala sitathubutu"

Alipokuwa na umri wa miaka 15 alijiunga na tasisi ya watu wasioona ya New York, rekodi yake chuoni ilikuwa nzuri kiasi kwamba uongozi wa chuo ulimbakisha ili awe mwalimu pale chuoni, alidumu kwenye taasisi hiyo kwa miaka 11 akifundisha.

KISA CHA WIMBO

Mwaka wa 1868 William Doane mtunzi wa muziki na mfanya biashara maarufu wa Cincinnati,Ohio, Marekani , alipenda kuboresha kazi zake za utunzi kwa kushirikiana na watu wenye vipaji vya utunzi wa Mashairi ya nyimbo hivyo akamwomba Fanny Crosby kutunga Mashairi ya Wimbo utakaoanza na Usinipite Mwokozi .

Kazi hii ilimchukua Fanny Crosby majuma kadhaa mpaka siku moja alipokwenda kwenye gereza moja karibu na vitongoji vya Manhattan, New York kuhudumia wafungwa kwenye vipindi vya ibada, ndipo aliposikia mmoja. wa wafungwa akipaza sauti na kusema ,“Bwana Mwema!Usinipite! Usinigeuzie mgongo, nikumbuke" Mfungwa huyo alikuwa aliwaita wale wahudumu au askari wa magereza waliokuwa gerezani humu ili asije akasahauliwa.

Kilio hiki cha huyu mfungwa kilimwingia moyoni na kujaa kwenye fikra zake na kuwaza ni kwa namna gani wafungwa hawa walikuwa ni watu waliosahauliwa na jamii na kutohesabika kama watu wenye umuhimu.

Crosby alitafakari umuhimu wa kilio cha mfungwa huyu aliyekuwa akilia kwamba Bwana amkumbuke. Akawaza jinsi ambavyo watu wanavyoweza kumlilia Mungu Na pengine Mungu akafanya kwa wengine Na akawaacha wao. Ndipo alipoweza kupata wepesi wa kutiririka Mashairi Haya, kwamba siku Yesu atakapokuja Na majibu ya wengine basi namimi asinipite. Na baada ya kuyaandika akamkabidhi Bwana William Doane ili atengeneze muziki ambao ndiyo unatumika mpaka leo.

Hii ilikuwa ni kolabo yao kwanza na baada ya hapo waliweza kushirikiana nyimbo nyingi,Fanny Crosby katika uhai wake alifanikiwa kuandika tenzi 8,000, nyimbo za kawaida 1,000 vitabu vinne vya Mashairi na vitabu viwili vya historia yake vilivyouzwa sana, mojawapo ya nyimbo alizoandika ni pamoja na "NDIYE DHAMANA YESU WANGU"

Wimbo huu wa "Usinipite Mwokozi" ulichapishwa rasmi mwaka wa 1870 kwenye orodha ya nyimbo za devotion na ulipata zaidi umaarufu baada ya kutambulishwa na L.Moody na Ira.D.Sankey kwenye mikutano yao ya uamsho huko London,Uingereza.
na kutokana na maelezo ya Dr.Young huu ni wimbo wa kwanza wa Fanny Crosby uliopata sifa nyingi Ulimwengu ni kote.

Haya ndiyo Mashairi ya wimbo "USINIPITE MWOKOZI"

1. Usinipite Mwokozi,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

Yesu,Yesu,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

2. Kiti chako cha rehema,
Nakitazama;
Magoti napiga pale,
Nisamehewe.

3. Sina ya kutegemea,
Ila Wewe tu;
Uso wako uwe kwangu;
Nakuabudu.

4. U Mfariji peke yako;
Sina Mbinguni,
Wala duniani pote,
Bwana mwingine.

Ahsante na Mungu akubariki sana.

Na Vincent Mwakisyala.
0753114222

#nitajitianguvukwaBwana
#Munguananipendasana
 
Mama alikuwa akiomba wimbo huu alfajiri nyingi na ilikuwa ni dalili kuwa kumekuchaa.
Tupe na stori ya muimbaji wa ule wimbo(jina nimeusahau) kuna ubeti INASEME"MWAMBIE YESU SUMBUKO LAKO"
Enzi hizo mama zetu walikuwa ni wife material haswa baba zetu walipata bahati jamani.

Sio sasa wake zetu wanaamka na kwikwikwikwi mi nitalia aah..
Mi nitalia aah
Ukiniachilia aah..

Tatata ta ta ta
Prupupu prupupu..
🤣🤣🤣🤣
 
Nakushukuru San mkuu kwa nyimbo huu mm Ni mmoja Kati was watu wanao zijuwa nyimbo za tumuambudu mungu wetu kwa ufasaha Sana na ukikozea kuimba kanisani au ktk sehemu bas nauzunika San Sana sipendi huaribifu wowote was nyimbo hzo

Kanisa la ya kkkt ya mijini Moshi wanajuwa Sana kuzimbaa nyimbo hzo bill kukozewa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Enzi hizo mama zetu walikuwa ni wife material haswa baba zetu walipata bahati jamani.

Sio sasa wake zetu wanaamka na kwikwikwikwi mi nitalia aah..
Mi nitalia aah
Ukiniachilia aah..

Tatata ta ta ta
Prupupu prupupu..
🤣🤣🤣🤣
Dah. Hivi ni nini kilitokea hadi tukajikuta tumekuwa na wanawake wa version ya hovyo kama hii tuliyonayo kwasasa? The way ninavyokumbuka mama yangu alivyokuwa industrious na loyal kwenye familia yake, naona ni ngumu kumpata mke kama HI mkubwa alivyokuwa. Baba zetu walienjoy aisee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom