FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,883
- 109,211
Natokana na Ukoo wa kina Muyinga hili la Mkwavinyika (MKWAWA) kuwa muislamu hakika si kweli kabisa. Baba yake Mkwawa, Mnyigumba ambaye kaburi lake liko pale Lungemba hakuwahi kuwa muislamu. Uislamu Kalenga makao makuu ya Mkwawa uliletwa na wanubi na Wamanyema ambao walikuja na Mjerumani kumpiga Mkwawa. Baada ya mkwawa Kujinyonga pale Kikongoma ndipo wajerumani wakaweka kikosi cha askari wao pale Kalenga ambao wengi wao walikuwa ni Wamanyema na wanubi na kwa upande wa dini walikuwa ni waislamu.
Kama FaizaFoxy anavyoshangaa wakristo kuwasaidia wajerumani kumpiga Kinjeketile ndivyo waslamu walivyowasaidia wajerumani kumpiga Mkwawa. Hawa tunaowaona kama "wakristo" au "waislamu" walikuja Afrika kwa maslahi yao na wala si maslahi ya waafrika. Kwa hili la Mkwawa kwamba alikuwa Muislamu husemi ukweli.
Kwenye ukoo wa kina Mkwawa wapo wakristo na waislamu na hii inatokana na ukweli wa migawanyiko kwenye ukoo wenyewe tngu mkwawa akiwa hai.
FaizaFoxy hashangai, anauliza uzalendo uko wapi? Wa kupoteza historia hata ya MajiMaji wacha na hii ya juzi ambao watu bado wako hai, na kwa hili tunamsifu sana Mohamed Said kwani na hii ilikuwa inafifirishwa watu wasiujuwe ukweli. Lakini leo tunajuwa ukweli uko wapi, kama nnavyosema mara zote, hakuna mmoja aliyetokeza kuupinga ukweli wa Mohamed Said kuhusu hawa wazee nnachokiona ni kurukia hiki au kile ukweli unabaki kuwa ukweli. Hata hilo la Mkwawa naona watu wanarukia huku wakirukia kule kwa sababu tu la Songea limekuwa bayana.
Kila tunavyoendelea ndio tunazidi kufunguwana macho. Hakika Mohamed Said unastahili kila sifa na tunakusihi endelea.
Tunataka mpaka iwe bayana uwenye "Heri" wa Nyerere kuelekea "Utakatifu" ni kwa kulitumikia Taifa au kwa kulitumikia Kanisa? Maana kwa upande wangu nimeona kaliacha Taifa hohehahe, hakuna fedha BOT na BOT yenyewe imechomwa moto. Hakuna mafuta ya kutumia kwenye magari, foleni vituo vya mafuta, Jumapili hakuna kuendesha hata gari bila kibali maalum. Hakuna chakula, hakuna hata dawa za meno. Ashaakum si matusi, hata vistiri hali vya kike vilikuwa hakuna madukani. Sidhani kama hivyo ni vigezo vya "heri" na "utakatifu". Tuujuwe ukweli. Na kama ni kwa kulitumikia Kanisa, tuelezwe kwa kiasi kipi? Na kwa mali zipi? Na kwa maslahi ya kina nani? Kila tunapoendelea tutapata mengi ya kuuliza.