Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Mag3, Oct 17, 2011.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kitu kimoja nilicho na hakika nacho kwa asilimia 100% ni kwamba wale wote wenye mapenzi ya kweli kwa taifa letu la Tanzania wanasita sana kuchangia hii hoja inayofinyangwafinyangwa na huyu anayejiita Mohamed Said. Bila kumung'unya maneno nayaita madai ya Mohamed Said la kutoa elimu ya historia ya kweli ni porojo hatari iliyojaa uchochezi ambayo lengo lake hasa ni kuleta uhasama wa kidini miongoni mwa wananchi. Sijui anachotegemea kufaidika nacho kwa kupanda hii mbegu ya hatari ambayo nina hakika mtu kama Mohamed Said anajua fika madhara yake.

  Mohamed Said ni kama kipofu ambaye baada ya kusimuliwa na wazee kwamba tembo ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wengi anapata nafasi ya kumpapasa tembo. Kwa bahati mbaya anaupapasa mguu wa tembo na si mwili wote halafu katika imani yake anadai anao uwezo wa kutoa somo kuhusu umbo la mnyama tembo na ushuhuda wake, kuwa tembo ni kama gogo la mti mkubwa, ndio ukweli na anayesema tofauti hajui kitu. Watu wote wanaolalamikiwa na Mohamed Said kuwa walisahauliwa, wengi wao walikuwa wakazi wa Dar es Salaam eneo la Gerezani.

  Kabla ya uhuru Tanganyika iligawanywa katika majimbo makuu manane na katika majimbo yote hayo, jimbo la pwani kwa ujumla lilikuwa moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma kimaendeleo kiuchumi, kielimu na kisiasa na hiyo ni licha ya kuwa makao makuu ya serikali ya kikoloni yalikuwa Dar es Salaam. TAA ilianzishwa na watumishi wa serikali (civil servants) na kwa wakati wote kazi kubwa ya TAA ilikuwa ni kulalamika ikidai haki ya wafanyakazi bila upendeleo na hasa ubaguzi wa rangi katila utumishi kubwa ukiwa uonevu dhidi ya wazawa, mtu mweusi.

  Jimbo la Ziwa ni moja ya majimbo yaliyokuwa mbele kiuchumi, kielimu na kisiasa na kama kuna kitu kinaweza kudaiwa kuwa kilisahaulika katika harakati ya kupigania uhuru ni mchango wa Jimbo la Ziwa (Bukoba, Mwanza, Mara na Shinyanga) Jimbo la Ziwa ndilo lililoongoza kwa idadi ya watu, idadi ya makabila, idadi ya mali asili na idadi ya machifu ambao nafasi yao ilikuwa kubwa tu katika kuhamasisha watu. Moja wa watu ambao mchango wao nitautaja kidogo tu ingawa alifanya jitihada kubwa labda zaidi ya wazee wa Mohamed Said ni Paul "Kishamapanda" Bomani.

  Historia ya harakati za uhuru ni zaidi ya porojo za Mohamed Said, watu walipigania uhuru kama Watanganyika na bila kubaguana kikabila, kidini wala kijinsia. Ndio maana mimi sitaki kabisa kuwa na majibizano na huyu Mohamed Said moja kwa moja ila kwa kuwa hoja ileletwa JF, akae tayari kupewa somo kuhusu umbile zima la mnyama tembo na sio mguu moja wa tembo alioupapasa. Hapa mimi nitaongea sana kuhusu mchango wa Jimbo la Ziwa na baadaye kuonyesha jinsi maadui wa nchi yetu wanavyowatumia kidini watu kama huyu Mohamed Said.

  Baadaye nitaeleza jinsi Mkoa wa Mara yenye makabila karibu hamsini yalivyoweza kushirikiana bila mfarakano na kuitikia mwito wa Mwalimu Nyerere katika hizo harakati za kudai uhuru. Je mwamko wa wakazi wa jimbo la Ziwa ulikuwaje na mapokezi gani aliyapata kila wakati Mwalimu aliporudi kwenye hili jimbo ambalo idadi ya wakazi wake kwenye miaka ya 50s ilikuwa mara tatu ya majimbo mengi Tanganyika kama Pwani. Pia nitaonyesha ni wakati gani walianza kuyasikia hayo majina anayodai Mohamed Said ya wazee wa Gerezani Dar es Salaam !
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Nimesoma kitabu chako version ya kiingereza, halafu nikasoma makala Annur, Nasaha n.k miaka 20 iliyopita. Nikarudia katika swahili version na nazidi kusoma katika JF. Kote huko nabaki na maswali na nikikuuliza hujibu ila unataharuki na matusi.

  Mzee Said Umewahi kusema EAMWS ilitaka kujenga chuo kikuu( ninayo maandishi yako), vijana wako wakasema shule za Agakhan ni za Waislam(ushahidi upo) na wala hukuwahi kusahihisha kama yalikuwepo makosa. Vijana wako wakaleta 'nondo' kuonyesha kuwa Agakhan ni mkuu wa Ismailia holdings companies (hujawahi kanusha). Inajulikana mlezi wa EAMWS aliyewashirikisha waislam wengine ni Agakhan wa Ismailia(moja ya makala zako). Kwahiyo kama EAMWS ingeweza kujenga chuo ni kwa nguvu ya Agakhan. Kijana wako alileta 'nondo' za kuonyesha kuwa Agakhan alikuja 1945 na baadaye akaamua kuwashirikisha waislam wengine kuunda EAMWS. Hadi hapo hakuna neno langu ni maelezo yako na vijana wako. Ninaposema Ismailia walitaka kujenga chuo cha waislam nimekosea nini kwa mtiririko huo?

  Kupanda mauzo si dalili ya watu kukubaliana au kuelewa hoja, wapo wanaotahamaki, wapo wanofuatilia kujua hatma, wapo wanaoshangaa kusikia (mfano,Nyerere aligoma kutoa majina ya mitaa) n.k.

  Lakini habari zako ni very sensational kwamba kila mtu angependa kuzisoma si kwa sababu ya kuelewa bali kutahmini hali ya utangamano wa taifa unapoelekea. Unaweza kulibaini hili siku watu watakapokuwa wamebeba mizigo, watoto na wake zao wakivuka mipaka( eeh mola tuepushe)

  Mohamed unapaswa pia kuelewa mwenendo wa wasomaji wa Tanzania. Ukieleza kuwa Bilioni 110 zinalipwa mtu mmoja kwa wizi hiyo si habari, habari ni ile ya ndoa ya mtu fulani. Hivi hapo kariakoo hujawahi kuona kuku(aina ya kuchi) wanapopigana watu wamezunguka!

  Vyombo vya habari vina taratibu na miiko yake ya kazi. Vina jukumu la kuliunganisha na kulilinda taifa. Tumeona Rwanada na Kenya vilivyotumika vibaya kuleta maafa kwa wanadamu. leo wapo mayatima, wajane, walemavu, wasiojulikana walipo walioacha nyumba zao na sasa wanaishi kwa dhiki kwingine.

  Habari zinazoonekana kuvunja umoja wa taifa hazifai kuwekwa katika vyombo hivyo, sio kwamba hazitasambaa ila vyombo vya habari vinaosha mikono dhidi ya damu ya wanadamu. Haviwezi kutumika kumuumiza mwanadamu bali kuleta ubora wa maisha.
  Mauzo ya magazeti na vitabu vyako yaweza kuwa yamepanda sana, lakini usisahau kujiuliza kwa gharama ipi !

  Suleiman Rushdie aliandika kitabu na madhara yake tunayajua. Cartoon za wadenish tunajua gharama zake, hadi hapo hatuoni hekima ya vyombo vya habari kwa mustakabali wetu kama taifa!!!! Je, utajisikiaje leo ukisikia Rushdie anasema mauzo yake yamepanda.

  Mohamed linapokuja suala la vyombo vya habari naomba ukae kimya. Unasema(na ni kweli) kuwa serikali imepiga marufuku kitabu cha Njozi, lakini ni Mohamed huyo huyo anaunga mkono serikali kuzuia kitabu cha Rushdie. Mzee Said, double standards kama hizi ndizo zimejaa katika makala zako na vitabu na ndicho chanzo cha kuhoji, si kuhoji ulichoandika tu bali ' paradox'

  Unajificha katika mgongo wa kutahadharisha umma, wenye akili zao wanajua kuwa umeshika kuni na unachochea moto.
  Kwanini usitumie fursa yako kuchochea moto wa fikra,majadiliano na solution badala ya kusisimua umma kwa maneno kama kifo, tutapambana n.k!

  Ninachoshangaa, Mtume Mohamad S.A.W, Nabii Issa A.S na manabii wote waliotangulia waliishi katika jamii na nchi zilizokuwa na imani mbali mbali na hata wasiokuwa nazo, kuanzia Maka, madina hadi Baithleheim, na ndivyo nchi yetu Tanzania ilivyo pia.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nilipo RED.

  Hakika siku zote lazima ujue unaandika katika mazingira gani hususan unapofuata tartibu na kanuun za uandishi.

  lazima uelewe pamoja na uliobainisha lakini msingi mkuu wa uandishi unabaki pale pale ni kuelimishana, kupashana habari na kuburudisha jamii.

  Siku zote mwandishi anapaswa kuandika kile tu alichokiona pasi na kuegemea upande wowote au kutoa suluhisho la tukio zima kwani kazi hiyo ya kuamua inabaki kwa wasomaji.

  Lakini vile vile unatakiwa ujue kuna habari za aina tofauti tofauti. Anachoandika Bw Moh'd katika makala yake ni kuandika historia ya Tanzania. Na amejikita zaidi na kutafiti na kutoa kile anachoamini kuwa ni sahihi kuwajuza historia watanganyika ambao hawakuwepo wakti huo.

  Na lazima ufahamu pia kuwa Historia haiwezi fichika na hakuna mwenye uwezo wa kuifuta au kuificha historia kwani hayo ni mambo yaliyofanyika katika jamii. Yawe mabaya au mazuri ni vyema yawekwe hadharani. (Historia ni kama pembe la ng'ombe). Na wajuzi wa mambo ndio maana wanaunda tume za maridhiano ili kuondoa pale penye kasoro na kuhakikisha mambo yanakuwa sawia siku hadi siku.

  Usione wajinga South Africa kuunda tume ya maridhiano au Rwanda na mauaji ya kimbari. Hiyo yote ni kuisafisha historia kwani itajiandika kutetea kile kilichokuwepo.
  Nawashauri wa Tanganyika ni vizuri kuipokea na kuipinga pale ilipoteleza na kuyafanyia kazi yale ya kweli kwa mustakabali wa nchi yenu. Kwani kuna mengi lakini kubwa kutokana na maandiko yake naona mengi yamejitokeza likiwamo la UDINI ndani ya jamii za wa Tanganyika.

  Eleweni kuwa mficha maradhwi siku zote kifo kinamuumbua.

  Kila la kheir
   
 4. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,778
  Likes Received: 5,775
  Trophy Points: 280

  Hayo yote uliyoweka hapo juu ni sawa kabisa wala hakuna wa kukupinga.

  Naomba pamoja na hayo soma hii kutoka "Tanganyika Political Intelligence
  Summary, March 1952":

  "...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has
  despatched letters to all branches asking members for suggestions under
  the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal
  Commission..."

  ...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as
  reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up
  country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the
  Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then
  visited Kampala alone..."

  (Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya
  kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti
  yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda.)

  Kuna mengi siwezi yote kuyaweka hapa.

  Mohamed
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi achana na huyu mpuuzi, tatizo ni kwamba watu wengi makini wamekuwa wakiyapuuzia haya makala yake ya kichochezi na hatari yake ni kuwa uwongo ukiachiwa nafasi ya kujirudia rudia mwisho wapo watakaoamini kuwa ni kweli vile. Mimi wakati naanza shule 1953, huyo Mohamed Said alikuwa hata hajazaliwa kama alivyokiri kwenye majibu yake hapo nyuma.

  Mimi ni mzaliwa wa kanda ya Ziwa na wakati tunapata uhuru mwaka nilikuwa Sekondari lakini pamoja na kuwa tulikuwa tunafuatilia sana matukio ya kisiasa, sikuwahi kuwaona au hata kuwasikia hao anaodai Mohamed kuwa walikuwa vinara wa harakati za kudai uhuru Tanganyika. Je hii ni kwa sababu nilizaliwa nje ya Dar es Salaam au kwa ni sababu hao wazee wa Mohamed hawakujulikana nje ya Dar es Salaam.

  Pamoja na kwamba mwaka 1965 tayari nilikwishahamia Dar es Salaam kuendelea na masomo yangu, sikuyasikia haya majina hadi miaka ya 1970 ! Baada ya hapo nilijaribu sana kuwadadisi wazee mbali mbali, Musoma, Mwanza hadi Bukoba lakini sikuweza kumpata mzee ambaye kwa hakika angeweza kunisimulia mchango wa hawa wazee wa Gerezani alikozaliwa Mohamed Said katika kudai uhuru wa Tanganyika.

  TAA kwa upande mwingine ilianzishwa na watumishi wa serikali chini ya utawala wa kikoloni na haihitaji akili yoyote ya ziada kukisia kuwa wengi wa hawa watumishi walikuwa wa aina gani. Ni vigumu sana kusema kwa uhakika ni lini TAA iliyoanzishwa mwaka 1929 ilianza kuwa na msimamo wa kisiasa lakini upepo wa uhuru kwa nchi nyingi za Kiafrika ulianza kuvuma kwa kasi miaka ishirini baadaye.

  Harakati za TAA zilipoonyesha dalili ya kudai mambo nje ya haki za wafanya kazi ilibidi kuchagua moja ama ujiuzulu uunge mkono TAA bila kificho au uendelee na ajira lakini usionyeshe wazi msimamo wako. TAA ikawa imefikia kikomo chake na ikawa sasa ni lazima kizaliwe chombo cha kisiasa ambacho malengo yake na dhumuni lake ni kuiondoa serikali ya kikoloni kwa kudai uhuru kamili.

  Madai ya Mohamed Said ni kama leo kudai kuwa wote walioko serikalini hawaungi mkono madai ya Chadema dhidi ya serikali, la hasha, wapo lakini wakijionyesha wazi wazi wakati huu nafikiri sote tunajua serikali ya CCM itakavyowashughulikia. Kulikuwa na faida kubwa kwa wanaharakati wengine kubaki ndani ya serikali ya mkoloni kama ilivyo sasa hivi kwa Chadema kuwa na watu wake ndani ya serikali ya CCM.

  TAA ya Mwanza mpaka mwaka 1948 ilikuwa na wanachama kama 3,000 lakini mwaka 1952 kwa jitihada za Bomani wanachama wa TAA waliweza kuongezeka hadi kufikia 30,000 na ni mwaka moja baadaye ndiyo Katibu Mkuu wa TAA kama anavyodai Mohamed Said alipotembelea Mwanza. Lakini wakati huo tayari Mwalimu Nyerere anaiongoza TAA baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Raisi wake.

  Walikuwapo watu kama Masanja Shija Raisi wa kwanza wa Victoria Federation Cooperative Union (VFCU) na Makamu wake akiwa Daudi Kabeya Murangira wa Majita aliyeuza boti zake za uvuvi. Jamani wana JF, Tanganyika ilikuwa zaidi ya Wazee wa Mohamed Said wa Gerezani na Kariakoo na ukweli ni kwamba Watanganyika walihitaji kuhamasishwa kutoka Mtwara hadi Sirari, Dar es Salaam hadi Kasulu !

  Mwalimu Nyerere hakuwa mtoto yatima, alizaliwa katika ukoo wa kichifu na familia kubwa iliyojaa wazee wa busara wa Kizanaki ambao walimpa baraka zao zote awakabili wakoloni bila woga. Mwalimu Nyere kila aliporudi Musoma hakusahau kufika kuvuka mto Mara kwenda kumsalimia Chifu Odemba Kagose wa Buturi Ujaluoni kupata ushauri wake kwa mambo mbali mbali.

  Wana JF, ni wakati sasa wa kuwakataa hawa wachochezi, ni wakati wa kumwambia Mohamed Said kuwa hata uvumilivu una mwisho. Wamekuwa wakipata free ride wakipanda hizi mbegu za chuki miongoni mwa wananchi huku sisi great thinkers tukikaa kando, no enough is enough, ukweli lazima waambiwe hata kama unauma kiasi gani.

  Majuzi hapa tumeshuhudia Marekani, watu wa kilichoitwa tea party wakiibua mambo yasiyo na ukweli na kuyarudia rudia hadi wakawateka wale wenye uwezo mdogo wa kufikiri ! Mohamed Said ni wa kuogopwa kama ukimwi ! Mohamed Said sasa aanze kuorodhesha majina ya wazee wake waliojiuzulu kwenye utumishi serikalini ili kupigania uhuru wa Tanganyika ili wajadiliwe hapa JF kwa sababu TAA ilikuwa ya Watumishi wa serikali.
   
 6. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,778
  Likes Received: 5,775
  Trophy Points: 280
  Mag3

  Umenitukana kwa kuniita "mpuuzi."

  Siwezi kufanya mnakasha (majadiliano)
  na mtu mwenye matusi.

  Mohamed
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mag3: Nakubaliana na hoja zako mbili kwamba watu wachangie hii hoja na kuwa uongo ukijirudia sana unakuwa ukweli.
  Hii ndio imesukuma wengi kulijadili hili suala kwasababu tunaiona hatari iliyo mbeleni

  Barubaru: Nadhani hujasoma vizuri mtiririko wa mada na umevamia tu kuwa 'Mohamed Said anaandika historia' .Ukweli ni kwamba yeye mwenye amekiri mara 4(ushahidi upo hapa) kuwa anaandika historia ya Uislam. Hilo si jambo baya kabisa, lakini nadhani ni kuchanganyikiwa kwa hoja ndio maana anapata 'slip tongue'. Kwa hiyo watu wajue haandiki historia ya Tanganyika.

  Pili napenda nikuhakikishie kuwa huko mitaani watu wanaishi vizuri, hadi pale ujinga utakapokolezwa na kuwachonganisha.
  Hakuna udini kuna watu wanataka kutumia udini ima kufanya biashara au kwa kutoelewa dini maana yake ni nini.
  Ni watu wachche wanaotaka kuvuruga taifa kwa kujificha nyuma ya pazia la historia, huku wakandaa vijarida vya siri diamond jubilee.

  Hebu tuzirejee kidogo baadhi ya hoja za Mohamed na utata wake.
  Ni Mohamed huyo huyo anasema waislam walipigania uhuru na na kudhulimiwa katika mambo kama elimu. Kama kweli elimu iliyokuwepo ilikuwa na nia ya kumsadia binadamu kimizingira basi kungekuwa hakuna kurudi nyuma na wala ukanda wa pwani usingekuwa hapo ulipo. Nakuhakikishia kuwa hakuna mtu atakwenda Mbeya, Kilimanjaro au Kagera na kuwarudisha nyuma kieleimu kwa sababu tayari wana silaha ya kuona kila kinachokuja, kujipanga na kukabiliana nacho. Ukitaka mfano mmoja wa mikoa hiyo Nitakupa.

  Anasema waingereza wamefuta irabu za kiarabu ili tu kujenga hoja yenye kuunganisha na udini. Mjerumani naye alifundisha watu lugha yake na mmoja wa watu waliyoiongea vizuri ni Sykes( ushahidi upo katika makala alizoweka). Na Maneno ya kiswahili baadhi ni ya kijerumani.
  Kwanini waingereza na sio wajerumani!! Mohamed amesahau kwa makusudi kuwa Rwanda na Burundi wanatumia kifaransa na majuzi tu waliomba iwe lugha rasmi EAC. Hakumbuki kuwa Msumbiji wanatumia kireno kama lugha na Libya bado wamebaki na makapi ya kiitalia.

  Dhima ya mkoloni ni kukufundisha lugha ambayo imebeba utamaduni wake ili akutawale kwa urahisi. Mohamed huwezi kutuaminisha kuwa Waarabu walileta lugha na irabu kwa madhumuni tofauti na yale ya waingereza na wajerumani. Hapa kinachokusukuma na kukusumbua ni ushabiki hatari sana wa kidini tu.

  Mohamed anajivuna kuwa watu walikataa shule za Kanisa. Mimi nina mfano wa mkoani kwetu ambapo elimu ni 'hot cake' waislam wengi sana walitumia fursa hiyo na wamebadili hali za maisha yao bila kuathiri imani zao. Yupo kiongozi mkubwa sana serikalini na profesa mmoja ambao ni zao la wazazi wao kuelewa kuwa elimu haina mpaka na imeandikwa 'itafuteni hadi China'. China sio ya Mao Tse Tung au Hu Jintao, ni China ya fasihi iliyobeba 'Uchina' kimantiki na kifikra

  Sijui hii dhana ya elimu unaitoa wapi maana king Abdullah kasoma huko usikokutaka. Mfalme Fahd watoto wake wapo ulaya.
  Idadi ya watoto wa falme za kiarabu wanaosoma nje ya bara lao ni kubwa sana, Gadaffi, Mubarak, Asad, Ayatolhah Khomeni watoto wake wanongea kifaransa kabisa, angalia wasomi wote wa kiislam Nigeria, Algeria n.k.
  Mohamed, si wewe umerejea kutoka Marekani na Ujerumani! na huko ndiko unafanya reference za kutuonyesha unavyokubalika.
  Hao unao wapa mjadala wamesoma Irab za kiarabu?

  Mohamed anatushawishi kuwa uwepo wa Irab za Kiarabu ungemkomboa Mtanzania. Fair eneough! asichotumbuka ni kuwa kiarabu ni lugha kama kiingereza, kijerumani na kifaransa.

  Katika dunia ya leo hata Mjapan anatumia mabilioni kujifunza kiingereza. Wachina ndio wanatoa ajira kwa wazungu kuwafundisha na waarabu wanafungua shule za lugha kama kiingereza na kifaransa. Lakini cha kushangaza zaidi Mmarekani naye anajifunza lugha zingine.
  Lugha ni sehemu ya maarifa.

  Hii haimaanishi kuwa kiingereza ni lugha nzuri kuliko Kisukuma, lakini ni lugha muhimu sana ya mawasiliano iliyokubaliwa duniani kama tulivyokubali dola iwe 'reserve currency'. Labda utushawishi ujuzi wa Irab utatukomboa vipi na hapo hatutakuwa na chaguo.

  Mohamed, waambie watu watafute maarifa sio wewe uende kuongea kiingereza marekani ukirudi nyumbani unawaambia waongee Irab za Kiarab ambako huendi kutoa mihadhara
  Hapa Mohamed anatuthibitishia kuwa Sykes anayemnadi kama kiongozi wa ukombozi wa Tanganyika hakuwahi kufika Moshi, Mbeya wala Mtwara. Ni Mohamed huyo huyo anasema historia ya uhuru wa Tanganyika. Tanganyika ni ipi? Kariakoo na Gerezani au Tanga hadi Kigoma, Mtwara hadi Musoma. Hizi ndizo naita 'paradox'

  Kuhusu la picha za NF ninamuuliza Mohamed, aliyekataa kuzipokea ni nani? Butiku, Salim au basi Shivji. Nauliza hivi kwasababu Mohamed hawahoji wahusika walio hai anapotoa tuhuma zake, lakini anatuaminisha zile alizosikia ni kweli. Hatukatai kuwa heunda ni za kweli, lakini anapokataa kumhoji Mama Maria Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Salim Ahmed Salim, Butiku, Profesa Shivji kama alivyoshindwa kumhoji mzee fundikira hadi akafariki na sasa anamtuhumu kuua EAMWS inatia shaka na hofu.

  Narudia kauli ya Mag3, ni wajibu wetu tusimame na kukataa mambo kama haya. Uongo ukijirudia utageuka kuwa ukweli. Tusiwapuuze watu kama Mohamed kwasababu jitihada zao za kukuza mauzo ya vitabu zinaweza kutuletea madhara.
  Mohamed, iache jamii iishi kwa utangamano, usipandikize chuki. Sote tusema 'NO'
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Naam, naona tunazidi kupewa elimu hapa. Shukrani wakuu.
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Shida kubwa ya Mohamed Said ni namna alivyouvaa UISLAMU kwa kila kitu. Anadhani watu waliamka kudai uhuru kwa UISLAMU wao. Hii inampunguzia sana nguvu ya hoja zake nyingi. Kingine kinachomhangaisha ni pale anapojaribu kuandika upya historia ya NCHI hii kwa kuhangaika sana na Mwalimu.
   
 10. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mzee Mwanakijiji, mchango wa Wazee wa Gerezani Kariakoo katika harakati za kudai uhuru Tanganyika kwa wastani ulikuwa ni mdogo sana ukilinganishwa na wa sehemu zingine ndani ya Tanganyika. Majimbo yaliotia fora na kutoa mchango mkubwa uliowezesha Tanu kuenea kwa kasi ya moto wa nyika ni Jimbo la Ziwa (Mwanza, Mara, Shinyanga na Kagera), Jimbo la Kaskazini ( Arusha, Kilimanjaro na Manyara) na Jimbo la Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Iringa na Njombe)

  Hebu shuhudia hii mkutoka Upareni;
  Hata wanawake wa Upareni hawakuwa nyuma katika mapambano dhidi ya mkoloni;

  Ni mtu mmoja tu aliyeweza kuwaungaisha Watanganyika kwa ujumla wao na kuwatia mori katika hizo harakati naye si mwingine ila Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na popote pale alipokwenda ndani ya Tanganyika alipata mapokezi makubwa yaliyowaacha hata wakoloni midomo wazi. Moto aliouwasha Mwalimu ulikuwa na nguvu kama wa Tsunami na laiti Wazee wa Mohamed Said wangesita kumwunga mkono wangezolewa na hayo mawimbi. Mwalimu alikubalika na sidhani kwamba kama hangepewa ushirikiano na hao wazee wa Gerezani moto aliokwisha kuuwasha ungezimika, la hasha, sana sana kuna watu wangeachwa kwenye mataa na huu ndio ukweli.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Hili ni suala nililoliibua huko nyuma; kwamba hakuna ushahidi wowote wa kihistoria kuwa wapigania uhuru wa nchi yetu walifanya hivyo kwa ajili ya Uislamu wao au kuongozwa na falsafa na mafundisho ya Kiislamu; wanaweza kuwa waliamini hivyo lakini wengi walipigania uhuru kwa sabau walikataa kutawaliwa na wageni na katika hilo hawakuwa tofauti kwani Wakristu, Waislamu na Wapagani wa TZ wote walikuwa chini ya utawala wa mkoloni. Ushahidi pekee alionao ni wa kusema kuwa wanaharakati wa kwanza wa uhuru jijini Dar wengi walikuwa ni Waislamu hili linaweza kuvutia watu wengine lakini halina mvuto wa kiakili. HIvi mtu akienda Mwanza na kukuta wanaharakati wengi ni Wasukuma au Wanyamwezi anaweza kushangaa sana? Au kwenda Mbeya na kukuta kuwa wanaharakati wa mwanzo walikuwa ni Wanyakyusa tunaweza kusema kuwa ni kwa bahati mbaya?

  Hivi leo, wanaharakati za mabadiliko Zanzibar wengi wao ni Waislamu hii ina maana gani? Je, tunaweza kusema kuwa harakati za mabadiliko ya kisiasa Zanzibar zimeletwa na Waislamu tutakuwa tunasema jambo moja profound?

  Tatizo ni kuwa Nyerere ni kizuizi na alama ya tatizo kwa wanaotaka kuandika historia hiyo mpya. Na hasa kama historia inayotaka kumuonesha kuwa Nyerere alikuwa na chuki ya Waislamu halafu wakati huo huo mtu anadai anapicha nyingi za Nyerere na wazee wa Waislamu ambao wazee hao wamezitunza - sielewi kwanini wametunza picha za mtu aliyekuwa na chuki nao! Ni sawasawa ukute Wayahudi wanapicha za Hitler halafu wanataka kuzionesha kwa furaha kuwa Hitler alipiga picha nao; miye ningedhania lingekuwa ni jambo la aibu kwa wazee wa Kiislamu ambao Bw. Said anawataja kuonekana na Nyerere hasa kina Shehe Takadir na wengine.. ingekuwa ni jambo la fedha kwa mtoto wao au kijana wao leo hii kutaka kuonesha kuwa wazee wake walikuwa karibu hivyo na mtu aliyeuchukia Uislamu na kuwadhulumu Waislamu.

  Binafsi ningeona ni kweli walikuwa wanamchukia kama wangeitisha mkutano wa hadhara na kuzichoma hizi picha hadharani kuonesha chuki yao dhidi ya Nyerere!
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Hii sasa shule; yawezekana kumbe watu kama kina Paulo Kajiru walimtangulia Abdulwahid Sykes katika harakati za kupinga ukoloni Tanganyika. Sidhani kama mgogoro huu wa Upareni Bw. Said kaugusia kwenye kitabu chake maana Mgogoro wa Ardhi wa Meru inaonekana umekuja baadaye.
   
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #13
  Oct 19, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Laah la la! Mkuu Mag3, ahsante sana umenikumbusha kisa kimoja. Unajua hilo la wanawake wa Kipare lilitokana na mambo kadhaa. Mwingereza aliweka kodi ya kichwa na wakati huo ilikuwa ni kubwa sana.
  Wanaume wa Kipare wakalazimika kulala maporini ili wasikamatwe. Wake zao wakaungana na kuwatia ushujaa wa kupambana.

  Wanaume woote( aliyebaki alikuwa mahututi) na wale vijana waliotoka jando wakaungana bila kujali dini zao au koo zao. Wakabeba mishale na mikuki na kuandamana kwa miguu kutoka upare milimani, zaidi ya KM 180 kwenda Boma la iliyokuwa makao makuu ya Pare, Same.

  Maandamano yalikuwa ya amani lakini tayari kwa lolote lile. Mwingereza DC alipoona Boma limevamiwa akapiga simu kwa Gavana na kutoa amri ya kufuta kodi hio hapo hapo.

  Wazee wakarudi mshaujaa. Hiyo inaitwa KODI YA MBIRU. Muulize mzee yoyote wa kipare mwenye 70+ atakueleza. Hili nimeelezwa na wazee wangu na wapo hai baadhi, kama kuna anayetaka ushaidi ahlan wahsalan, nitatoa nauli, malazi na chakula Tukawahoji wazee wangu.

  Ndiyo maana wakati wa kupigania uhuru Nyerere alikubalika sana huko. Je hawa hawakuwa wapigania uhuru!
  Na hao akina mama aliotaja Mag3 na kwingine huko, je si wapigania uhuru wa Tanganyika!
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nguruvi3,

  Hakika nimekuwa na kawaida sana kuusoma mjadala huu adhimu kila siku na kila nitufa ya kila mtu. Na pale nilipoamua kukujibu kwenye post no 3 ni pale ulipoeleza maadili na kaanun za uandishi kwa kutaka kuhalalisha maneno yako. Nimetumia hiyo post no 3 kukufanulia kwa kina sana kaanun na miiko ya uandiki kijumla ili kuleta uwiano ulio sawa kwetu wasomaji.

  Kwa mtu yoyote makini akisoma mjadala huu utaona wewe Nguruvi3, Wildcard na mag3 mnazungumza mambo mengi sana na lugha za kejeli pasi na ushahidi wa kiutafiti kwa maana hamna reference yoyote mnayotumia ukilinganisha na Bw Moh'd Said ambaye ameonyesha umahiri wake mkubwa katika mada yake ya Historia ya uhuru na kujipambanua pasi na shaka kuwa amefanya utafiti.

  Ndio maana narudi pale pale siku zote mtu akifanya utafiti na kutoa mada inataka hata yule anayeona labda kuna upotovu wa maana au kuna jambo lipo sivyo ndivyo basi kitaaluma yule mtu anatakiwa kuleta dalili (reference) za kupinga pale anapoona kuwa hapako sawia. Na mstaarabu siku zote anakuwa makini sana kusoma na hata anapochangia anatumia lugha adhimu isiyo na kejeli wala matusi. Kwani sote tupo hapa kupata darsa na kuelimika.

  nazidi kuwashauri tupo wengi tunapitia mjadala huu kama mna hoja kupingana na Moh'd said basi nanyi tuwekeeni reference zenu ili nasi tukijaaliwa tuweze kuzipitia ili jukumu la kusema kuwa historia inapindishwa au inanyooshwa litabakia kwetu wasomaji na si ninyi.

  nawatakia kila lenye kheir na mjadala mwema.
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Barubaru,
  Mimi sijaanza kumsoma leo wala jana Mohamed Said. Unapoitanguliza DINI kwa kila jambo unakuwa hauna tofauti na mshirikina. Unabagua. Wazee wale wa Kiislamu waliomkaribisha Mwalimu kwenye TAA wangekuwa kama Mohamed Saidi historia ya nchi hii ingekuwa nyingine kabisa.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Nguruvi kasema reference yake ni "wazee wake" kitu ambacho M. Said nacho anatumia je inatosha mtu kusema "wazee wangu waliniambia" kuwa ni ushahidi tosha usiohitaji kuhojiwa? Reference ya vyanzo visivyoaminika yaweza kunukuliwa kila mahali lakini je ni kweli? Kwa mfano, mtu anaweza kusema "Mwinyi alimuambia Malima x,y" lakini Malima ni marehemu na Mwinyi yupo lakini Mwinyi hajahojiwa bado unaweza kusema huko ni kuonesha weledi wa kufanya utafiti? Fikiria kwamba, karibu wengi wanaoshtumiwa au kuwekewa maneno na Bw. Said wamekufa lakini wale wengine wanaotajwa wakiwa bado hai hajawahoji yeye mwenyewe angalau kupata mawazo yake. Kwa mfano, mtu anaweza vipi kusema Nyerere alikuwa na chuki na Uislamu au Waislamu bila kwenda kujaribu kukaa na mke wa Nyerere ambaye bado yuko hai, ana akili timamu na nina uhakika angeweza kabisa kueleezea na kutoa msaada wa taarifa mbalimbali? Kweli unaweza kuita huo ni uchunguzi wa kisomi? KUrusha references tu si usomi au weledi kwani kama hujibu maswali yanayotokana na references hizo na kutuambia tu kuwa "kama hamuamini basi, kama mnaamini safi".

  nadhani anachofanya Bw. Said ni chema sana lakini hakifanyi chote au kwa nia safi ambayo ni kuongezea ujuzi. Yeye anachotaka ni a. Ikubalike Nyerere hakuwa na mchango wa kipekee katika harakati za Uhuru kulinganisha na wapigania uhuru wengine. b. Waislamu ndio pekee waliokuwa wanataka Uhuru na Wakristu walikuwa hawataki kwa sababu walikuwa wananufaika na ukoloni (rejea kitabu chake hicho cha Sykes) na c. Waislamu wameonewa na Kanisa na kanisa bado linawaoena Waislamu and by extension Wakrisu wanawakandamiza Waislamu.

  Yote haya anayejenga kwenye hoja ya "wazee wangu". Really? Hana ushahidi ambao anaweza akautoa mahakamani ukasimama siyo dhidi ya Nyerere wala siyo dhidi ya Kanisa. Ana tuhuma nyingi nzito ambazo zintolewa vidhibiti vingi lakini kila akihojiwa kuhusu hivyo vidhibiti anasepa.
   
 17. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #17
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,778
  Likes Received: 5,775
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu kanitukana na kwa kuwa mimi si mtu wa matusi bali hoja
  nimeamua kujiweka pembeni.

  Sheikh wangu Maalim Haruna (Mungu amrehemu)akitueleza katika madras
  wakati anatufunza adab za mnakasha (majadiliano) kuwa dalili ya kwanza
  ya mtu kushindwa ni ukali na lugha zisizokuwa kiungwana.

  Dalili ya pili ni kukutukana kabisa.

  Sheikh akaendelea kusema kuwa akitoka hapo katika matusi atakutoa ngeu.

  Akashauri kuwa unaejadiliananae akifika daraja ya kukutukana basi jiondoe.

  Hii ni salama kwake yeye na kwako mtu kuepusha shari ndiyo ustaarabu.

  Waungwana wasomi hawakejeliani katika mnakasha wala hawatukanani.


  Mohamed
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Muwie radhi nduguyo huyo maana wakati mwingine nawe waweza kujikuta umesema kitu cha kumkwaza mtu na ikawa kumbe ni kughafirika tu kwa ubinadamu. Vizuri ni kufuata maxim yangu ya muda "hoja hujibiwa kwa hoja si viroja"
   
 19. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,171
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Umejidhirisha ni mtu wa namna gani na umeonesha uwezo wa upeo na fikra zako. Kuzaliwa mapema hakumfanyi mtu awe na maarifa kuliko wengine, kutomsikia mtu hakumfanyi kuwa hayupo au hakuwepo na pia kunga'ng'ania yale tu unayoyafahamu ni kipangamizi kikubwa katika kuelimika. Historia ina kawaida ya kuchagua kutegemea nani anayeandika historia hiyo lakini pia historia ina tabia ya kuchagua mambo na watu wa kuwaandika. Mtu mmoja akiandika historia ya Gerezani na kuwazungumzia waislamu walioshiriki katika uhuru hakumfanyi mmtu mwingine asiandike kuhusu menonite wa mara walioshiriki katika uhuru Bibi Titi amesema yake, Sykes amesema yake, Bomani nae amesema yake na pia kila mtu aliyeshiriki nae aseme yake. Hii itasaidia kuondoa machungu ya watu wengi ambao walishiriki katika uhuru ambao nafasi zao hazithaminiwi wala kutambuliwa. Mohamed ameonesha njia, kama muungwana yeyote amsaidiaye mtu aliyepotea sasa leo muungwana anaonesha njia unaanza kumkashifu. Nafahamu udhaifu wetu binadamu na tofauti zetu katika kukabili mambo ndio maana kila siku tunatafuta maarifa ya kuweza kuimiliki na kuitawala miili yetu kwani yampasamtu kuukabili mwili wake kwa kuufahamu uimara na madhaifu yake kabla hajaenda nje kwenye hadhara ya watu.

  Juzijuzi kulikuwa na kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu, swali kubwa watu walijiuliza kuwa iliwezekanaje kumpata Nyerere yule na imeshindikana kumpata Nyerere mwingine. Mimi naamini Nyerere si tukio ni zao, alizaliwa kutokana na harakati zilizofanywa na watu mbalimbali akafinyangwa akatokea Nyerere. Namna ya harakati hizo zimefichwa na watu waliozifanya hawatambuliki, Je tutawezaje tena kumfinyanga Nyerere mwingine na wazee wengine kama akina Rupia, Bomani na wengineo ikiwa tunachagua na kubagua kuwaambia watoto wetu na vizazi vyetu tulipitia wapi na akina nani walifanya nini? Wajue kuwa hata mchuuzi wa samaki anaweza kuyafnyia makubwa nchi hii, ajue pia kuwa hata akina mama ambao hawajakanyaga hata darasa moja wanaweza kulifanyia makubwa taifa hili ( Soma wanawake wa TANU cha BIBI TITI MOHAMED). wajue kuwa hat shilingi mia mia zikichangwa na kutumika vizuri zinaweza kuyafanya makubwa.

  Kila mtu aseme na aandike aliyoyaona, yote haya yajumuishwe na watanzania wayajue wajue hasa nchi yao imetoka wapi na nani alifanya nini. Tena hii itasaidia sana kufahamu uwezo wetu watanzania katika kulijenga taifa letu na hivyo kuamua kama uwezo tulio nao hautoshi hivyo tuwekezwe na kujiwekeza au kujitegemea sisi wenyewe.

  Kama unayo yako na wewe iseme na ukiweza iandike. Tatizo kubwa tulilonalo watanzania ni kushindwa kutunza kumbukumbu za maisha yetu katika maandishi. Hivyo sasa huu si wakati wa kumtukana na kumkashifu mwenzio eti kwa vile tu ametunza kumbukumbu anayoifahamu yeye.


  Mtu mwema ni yule anayetambua mapungufu yake na si yule anayetambua mapungufu ya mwenzake na pia wahenga walisema ni bora kutafuta na kuviondoa vipangamzi vilivyo ndani yako ambavyo vinakuzuia kupokea maarifa mapya kuliko kuyatafuta maarifa mapya
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Shukran sana Mzee Mwanakijiji.

  Hayo ndiyo hasa ninayosema wakti wote. kama unaona kuwa kuna mushkeri wowote katika makala yake basi mtu makini anachukua jukumu la kwenda kuwahoji hao uliowataja na kuja na majibu muafaka wa makala ake na kuleta weledi mkubwa wa kuonyesha kuwa umeifanyika kazi waraka wake katika kuweka historia iliyo sahihi na kusiwe na kuchakachuwa kwa aina yoyote.

  sasa suala hilo linabaki kwetu hadhira kuwauliza hao ili kujua ukweli au uchakachuaji wa makala yake ili tuweze kumpongeza au hata kumlaani kwa kupotosha historia.

  ndio maana kila wakti nasimama kusema kuwa kazi ya mwandishi ni kuandika pasi na kuegemea upande wowote ila kazi ya uamuzi ni a wasomaji.

  Sasa tusimame na kuamua kwa hoja zenye mashiko.

  Ahsante kwa ufafanuzi wako.
   
Loading...