Historia ya mji maarufu wa Roma au Rumu

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Roma au Rumi ni mji wa zamani sana ambao zamani uliitwa dola la Warumi
Sasa ni mji mkuu wa Italy lakini kabla ya hapo Italty haikujulikana bali ikijulikana kama dola la Roma

Tarehe 21/4/753 ndio tarehe ya kimapokeo ambayo inasemekana kuanzishwa ila ukweli ni kwamba mji huo maarufu kote duniani ulianzishwa miaka 1000 hivi kabla ya kristo
Mji huo unaosemekana ndio mji uliojengwa kwa uimara kuliko miji yote duniani hata kukiwa na msemo unaosema hata Roma haikujengwa kwa siku moja ni mji ulioanzishwa na mapacha wawili ROMULO na REMO

Dola la Roma lilikuwa ni dola kubwa mno kuwahi kutokea
Achana na madola kama babeli,waajemi,na wamedi,dola la Warumi lilikuwa na nguvu mno
Huku likitawala eneo lote la Meditereneo, Ulaya kusini,Ulaya Magharibi,Asia ya Magharibi, na Afrika ya Kaskazini mnamo miaka ya 1600 hadi 2400 iliyopita
Liliendelea katika dola ya Roma ya Mashariki au bizanti hadi mwaka 1453 baada ya kristo

Jina la mji huo limekuwa pendwa kiasi kwamba baadhi ya nchi zina maeneo yanaitwa Roma au Rumi
Nchi kama Australia, Ecuador, Marekani, Mexico
Jina la mji huu pia limetumika katika meli ya kijeshi ya Italy
Pia filamu mbalimbali zimetumia jina hili kama Roman Empire

Pia kanisa la Roma ni jina la jimbo ambalo majimbo yote ya kanisa katoliki yalitegemea ili kudumisha umoja na amani duniani kote
Kwa sababu hiyo jina la Roma linatumika kumaanisha kanisa katoliki lote
Mfano mtu akisema anasali Roma anamaanisha ni muumini wa kanisa hilo

Pia jina Rumi lilitumika kumuita Mungu wa kike katika dini ya dola la Warumi kabla ya Kristo

Ongezea na wewe kama kuna nilichosahau kuhusu historia ya mji wa Roma au Rumi
 
Mkuu, asante kwa uzi wako wenye tija. kuna kitu cha kujifunza. ingawa umesahau vitu fulani muhimu. je ilianzaje kukuwa na kuwa Dola imara na madhubuti kushinda zote? nini kilichangia kukuwa huko? what about it's demise/fall? na kwa nini ulimwengu wa sasa or tuseme baada ya kristo, wameendelea kutukuza dola hiyo licha kwamba ilishaanguka?...mkuu, nikipata muda nitaongezea machache kwenye uzi huu...thanks in advance mkuu
 
Mkuu, asante kwa uzi wako wenye tija. kuna kitu cha kujifunza. ingawa umesahau vitu fulani muhimu. je ilianzaje kukuwa na kuwa Dola imara na madhubuti kushinda zote? nini kilichangia kukuwa huko? what about it's demise/fall? na kwa nini ulimwengu wa sasa or tuseme baada ya kristo, wameendelea kutukuza dola hiyo licha kwamba ilishaanguka?...mkuu, nikipata muda nitaongezea machache kwenye uzi huu...thanks in advance mkuu
Karibu sana mkuu
 
Mkuu, kuna tetesi kwamba kulikuwa na mji wa kale kule Kilwa, mji huu ulikuwa mkubwa mno kibiashara - historia inasema kwamba mji huu ulifukiwa na udongo ila kuna baadhi ya mabaki yanaonekana. Mji huu ulikuwepo kabla ya Kristo.
 
Back
Top Bottom