Historia ya Maisha yangu baada ya chuo mwaka 2009

Historia ya Maisha yangu baada ya chuo mwaka 2009

Mkuu umepambana Sana, kununua mahindi vijijini ni risk Sana na kitendo Cha kulala juu wa miti Kama makomandoo ni hatari, ila ume hastle Sana.
 
Mkuu umepambana Sana, kununua mahindi vijijini ni risk Sana na kitendo Cha kulala juu wa miti Kama makomandoo ni hatari, ila ume hastle Sana.
Mwana kufanikisha yataka moyo sana.., nanimekuja kugundua hakuna kazi rahisi. Kazi zote ni ngumu kikubwa ni nia na Dhamira tu masee.
 
Kahama kuna ishu gan ya kuingiza pesa ukiachana na uchimbaji madini?
Kahama hata biashara tu inalipa, maana mzunguko unategema machimbo na kilimo. Pia mwingiliano wa watu ni mkubwa sana maana Uganda, Rwanda, Congo mpaka Sudani kusini huwa wanaijia Mchele Kahama.
 
zipo za kila aina ni wewe kuja kujionea.fursa siku zote siyo ya kusimuliwa
Kusafiri kunahtaji niwe na muda kaka. Ndo maana nkakuuliza ww ulie huko maana technology imerahisisha haya. Mm nko dar ww upo kahama ila tunawasiliana kama tupo pamoja vile.
 
Kusafiri kunahtaji niwe na muda kaka. Ndo maana nkakuuliza ww ulie huko maana technology imerahisisha haya. Mm nko dar ww upo kahama ila tunawasiliana kama tupo pamoja vile.

dar ni kwetu nilipozaliwa ila mazingira yalinibidi kuja huku kutokana sehemu kama dar sasa kunataka kuwa na mitaji mikubwa sana ili uweze kuishi.

sehemu kama kahama bado kuna unafuhuu kuanza maisha,mtaji mdogo ambao unaweza kumudu flemu,makazi ya kulala na chakula.

unaweza kutoka na wazo dar ukaleta huku na ukafanikiwa.

kuna watu mfano tulikuwa nao dar kutokana na soko ushindani wa mitaji kuwa mikubwa watu wengi wamehamua kukimbilia sehemu maitaji yanaitajika.
 
Hongera kwa kuanza kuuona mwanga.Mungu akubariki upate mafanikio zaidi.
 
dar ni kwetu nilipozaliwa ila mazingira yalinibidi kuja huku kutokana sehemu kama dar sasa kunataka kuwa na mitaji mikubwa sana ili uweze kuishi.

sehemu kama kahama bado kuna unafuhuu kuanza maisha,mtaji mdogo ambao unaweza kumudu flemu,makazi ya kulala na chakula.

unaweza kutoka na wazo dar ukaleta huku na ukafanikiwa.

kuna watu mfano tulikuwa nao dar kutokana na soko ushindani wa mitaji kuwa mikubwa watu wengi wamehamua kukimbilia sehemu maitaji yanaitajika.
Sawa sawA mkuu.
 
Maisha yanahitaji mapambano ya hali ya juu sana! Kuna wakati unakatishwa tamaa na watu,au hata mtu wako wa karibu kabisa!

Mfano unamwambia demu wako,nataka nianze walau kazi ya kubeba mizigo ubungo bus terminal,utasikia hivi uliosoma nao wakikuona watakuonaje?? Ni aibu bwana usifanye! Kumbe kwenye kubeba kwako mizigo huko unaweza kutana na mtu akakupa mchongo na akakutoa huko!

Maisha ni safari ndefu sana,kuna wakati unaweza kufuru kwamba hivi mbona ni Mimi tu!

Cha msingi omba Mungu azidi kukupa afya njema,uweze kupambana zaidi na zaidi! Changamoto za afya ndiyo hua tatizo kubwa! Siku hizi vyeti havifanyi kazi, ila kinachofanya kazi ni wewe kuchanganya akili yako tu!

Kuna Mwamba kasota kweli,nasema kasota hadi mke alimkimbia,watoto akawarudisha kwa dada yake,lakini Mwamba kaja kupata kazi,sasa hivi ametusua na ana miradi yake ya maana tu,bank hakosi mpunga wenye triple digits!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii inshu ya kubeba mizigo stand hii,,, anyway ipo sku ntaielezea
 
SEHEMU YA NNE (MWISHO)

Jamaa baada ya kuniambia mfumo mzima wa uendeshaji wa zile kazi nikaridhia nanikaona hili nitumaini jipya juu ya maisha yangu. Mfumo wa sasa nitofauti sana na ule mfumo wa zamani yaani ule wakumuuzia Tajiri mwenye Plant ule mchanga. Mfumo wa sas mnapiga kazi mpaka pale mtakapoona mmekuza mnaenda Plant kuozesha, ila kila hatua mnakuwa mnachukua mchanga na kwenda kuupima ili kujuwa mwenendo mzima wa kazi yenu. Mkishakodisha Gold Plant kwa ajili ya kuozesha mnasomba ule mchanga na kwenda kupakia kwenye matenki ya kuuozeshea, na baada ya mda flani mnabeba mzigo kwenda kupakia tena kwenye mashine (Elution Plant) kuchenjua, sis huwa tunasema kukoboa na kupata kilichomo ambacho ni Dhahabu.

Nakumbuka tulipiga kazi mpaka mwisho mwa mwaka 2020 na tukapeleka Plant, nashukuru sana Mungu alitubariki tukatoka fresh japo hela nyingi ilikuwa ya watu, na tunashukuru tulifanikisha kurudisha tukawa tumebakiwa na balansi flan hivi tukawa tumenunua karasha la pili pamoja na compresa zile ndogo za kutumia Engine za Makarasha. Mfumo wa kupeana pesa huku huwa niwakienyeji tu, yaani hakuna taratibu za kuandikishana., Mtu anakupa hata milioni 15 ufanyie kazi baada ya miezi 4 urudishe milioni 20 yaani kikubwa uwe mwaminifu tu na ujitahidi sana kulinda jina lako lisichafuke. Kwa upande wa serikali kwa kweli Hayati Magufuli kuna vitu vingi sana kasaidia kwenye hii sekta ya madini hususan kwenye hii migodi midogomidogo. Zamani serikali ilikuwa haipati chake kwenye hii migodi midogomidogo na mchimbaji alikuwa hapati kama anavyopata hii leo, maana wizi kwenye huo mlolongo mpaka ukapate Dhahabu ulikuwa ni mkubwa sana.., lakini kwa sas kila sehem serikali ipo ndio maana hata yule mnunuzi mdogo wa Dhahabu analipa kodi., hata kama awe na gram moja akienda tu sokoni kuuza kuna asilimia flani serikali inapata.

Mwaka huu tuliiendelea na kazi na maisha nikawa nimeyazoea japo mazingira ni magumu, kazi ni ngumu ila unapofanya kazi na kupata kipato kinachoridhisha, kiasi flani unaridhika nacho inakubidi ukomae tu ili kufanikisha zaidi. Kiukweli hii kazi inalipa tena sana unaweza sema ni biashara chache sana zinaweza lipa kama inavyolipa hii kazi. Mwaka huu mwezi wa sita tulisomba tena na tukafanikisha kiasi na sasa mtaji wetu naweza sema umeimarika vyema. Tulifanikisha kuongeza karasha la tatu na DUARA kadhaa., maana tuliona tuimarishe kwanza vitendea kazi ili kurahisisha uendeshaji wa kazi. Naweza sema hivi niviwanda (Makarasha) na raw material inapatikana mlimani, yapaswa uwe na DUARA za kutosha ili kiwanda kisiwe na uhaba wa raw material yaani Mawe. Kwa sas tunapambana tena kwa mara nyingine na Mwenyezi Mungu akijaalia mwishoni mwa mwaka huu tutaingia tena Plant. Tuna vijana zaidi ya kumi tuliowaajili kwa kazi ya kuosha na kusaga pamoja na wanaopiga duarani. Japo kazi za duarani huwa tunawapa mkataba yaani mnakubaliana kuwalipa kwa tripu za gari, gari ni zile tipa ndogo zenye ukubwa wa 4.5M2.

Kwa wasiojuwa hizi ndio DUARA, sehemu ambayo huchimbwa Raw Material (MAWE) kwa ajili ya kwenda kusaga na kuosha Mwaloni.

[file:///storage/emulated/0/Android/data/com]

Ila kwa jinsi nilivyoona hizi kazi return yake ni kubwa sana obvious hata kukata kwake ikiamua kukata lazima ukatike saaana, kikubwa nikujitahidi kuwa na other source ya kipato ili kuwa na sehemu Kadha wa kadha za kujipatia kipato. Hakuna kazi isiyokuwa na changamoto, chamgamoto kubwa ni Mitaji pamoja na Maji ya kuoshea hususan wakati wa kiangazi na wakati wa masika Duara hujaa maji kutokana na nvua, kazi hufanyika kwa taratibu sana na kusababisha kuchukua mda mrefu sana.

Hitimisho,

Nawashauli vijana wenzangu wahitimu wa Vyuo vikuu tusichague kazi, na tusiwe tunatumia mda mwingi kutafuta kuajiliwa., kikubwa wew angalia kazi unayofanya kama ina matumaini mbele ya safari. Halafu tusing'ang'anie mjini tu, hata pembezoni mwa miji pana fursa tena kubwa tu. Mimi niliingia Dar mwaka 2000 lakini nimekuja kuridhia kutoka mwaka 2019 baada ya kuona ramani hazisomi, kitu ambacho nilikuwa nimekataa katakata kutoka mjini. Ujue hapa duniani Kuna mwajiliwa (Employee), Mmiliki wa biashara (Business Owner) pamoja na Mwekezaji (Investor). Nijukumu la kila mmoja wetu kuamua uwe kwenye group lipi kati ya hayo matatu, japo wengi hupendelea saaana kwenye Employee maana hapo ndio penye Security na hapana Risk kubwa., japo huwa hailipi kama sehem ya Business owner pamoja na Investor. Unakuta raia ana Capital nzuri tu ila amekosa cha kufanya, wew kama uko na pesa jenga nyumba nyiingi tu za wapangaji kadri uwezavyo., maana hazihitaji hata management kama zilivyo bness zingine. Kusema ukweli kwa mda huu niliokaa kwenye hizi kazi, nimegundua kazi ya aina yeyote ile inahitaji usimamizi sana vinginevyo utakaa kuwalaumu watu tu. Maana hata Sisi hapa tusipokuwepo yaani tukirudi tunaona kabisa mambo hayajaenda inavyotakiwa, inabidi kujitahidi kuwepo mda wote wa kazi. Nahis enzi za zamani inaweza kuwa Uaminifu na Uadilifu ulikuwa mkubwa sana kuliko ilivyo hivi sas. Mimi naamini kabisa ya kwamba, UAMINIFU NA UADILIFU NI MTAJI TOSHA hata kama hauna hata shillingi mfukoni lakini unaweza kupata kitu kupitia UAMINIFU..

Na unapoamua kuingia kwenye hizi kazi nje ya kuajiriwa hususan za vijijini kama kilimo na migodi midogomidogo, wew jishushe na usijionyeshe kama umeenda shule ili uendane na jamii iliyokuzunguka, maana ukitanguliza shule yako raia watakutenga nakukuona wew siyo mwenzao. Wew tulia komaa na kazi, wala hakuna haja ya kuingia kwenye mambo ya sias wala uongozi., kikubwa wew piga kazi kwa sana tu na ufuate taratibu zote za sehem husika maana unajuwa kabisa nini unataka na nini kimekuleta.

Huwa nakumbuka mzee wangu aliwahi kuniuliza swali nikiwa Chuo " unajuwa unapokwenda" nami nikajirahisi tu nikamjibu ndio najuwa, unaenda wapi nikamjibu nilipokuwa nafikilia. Mzee alicheka akaniambia hujuwi unapokwenda, leo ngoja nikwambie unapokwenda. Leo hii wew ni kijana na una nguvu nyingi za kufanya kazi na kujipatia kipato, inatakiwa ujiulize Naenda wapi?Jibu lake nikwamba naenda kuzeeka, sas nikishazeeka na nguvu zitakuwa zimeisha na sitaweza tena kufanya kazi Nitakula Nini. Wakati ni sasa wakutengeneza chakula chako cha uzeeni, maana hautasumbuana na mtu yeyote kama utaweza kuweka Asset kadhaa hususan Nyumba kwa ajili ya chakula chako cha uzeeni. Daaah nilitafakari sana nanikaona mzee kasema jambo la muhimu sana, Vijana wenzangu wakati ni sasa tungali na nguvu za kuweza kufanya kazi na kujiwekea akiba ya uzeeni japo kuufikia uzee ni majaaliwa yake Mwenyezi Mungu. Kusema ukweli kwenye hii kazi naamini ntakifanya tena saana tu kile alichokisema mzee wangu.

Ahsanteni sana wana janvi, maana kuna mengi yakujifunza kupitia jukwaa letu pendwa la Jamii forum.

Hii hapa chini ni moja ya mazao yanayopatikana kwenye hizi kazi zetu za migodi midogomidogo.
Mungu awabariki sana.


[file:///storage/emulated/0/Android/data/com]
Nimejifunza vingi sana hapa, asante sana
 
Back
Top Bottom