Historia ya kusisimua ya Sumbawanga

Airmanula

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
3,758
5,249
Kwenye neno Sumbu wanga, likiwa na maana ya tupa uchawi , na lilianzishwa na mtawala mmoja wa zamani wa eneo hilo
aliyeitwa Mwene Ngalu.

Sumbawanga ni makao makuu ya mkoani Rukwa, uliopo Nyanda za Juu Kusini Magharibi mwa Tanzania. Mkoa huu unapakana na nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Zambia, Burundi na mikoa ya Tabora na Mbeya na una jumla ya watu milioni 1.5, kwa mujibu
wa sensa ya mwaka 2002. Ulianzishwa rasmi mwaka 1972.

Mkoa huo una makabila mbalimbali ila kabila kubwa na la asili ni Wafipa ambao ndiyo asili ya jina Sumbawanga, mji ulioanzishwa mwaka 1803, chini ya chifu wa kwanza wa Ufipa aliyeitwa Kapufi ambaye alitawala miaka ya 1885.

Chifu Kapufi wa Kwanza alianza milki yake ndani ya Ufipa yote na makao yake makuu yalikuwa Kijiji cha Kisumba nje kidogo ya mji wa Sumbawanga. Mke wake aliitwa Mwene Wakulosi ambaye walijaliwa kupata watoto watatu, wa kwanza wa kiume na wawili waliofuata wa kike ambao ni Mwene Kiatu wa pili aliitwa ‘Mwene Ngalu Chisichaafipa’ (jina la utawala) na wa tatu aliitwa Mwene Mwati.

Baada ya kifo cha Chifu Kapufi wa Kwanza, milki ilitawazwa kwa mwanae wa kwanza, Mwene Kiatu ambaye alihamia kijiji cha
Lwiche ambako kwa mila na desturi za kiutawala, ukitawazwa kuwa chifu ni lazima uhame na kwenda kuanzisha kijiji chako kama alivyofanya Mwene Kiatu.

Katika kipindi chake cha utawala wa eneo la ufipa, chifu Mwene Kiatu hakujaliwa kupata watoto na alipokufa, milki ilichukuliwa na dada yake, Mwene Ngalu ambaye ndiye mwanzilishi wa Sumbawanga.

Chifu Mwene Ngalu alikuwa mtu mwenye upendo na hakupenda uchafu wa aina yoyote ukiwamo uchawi, hivyo kabla ya kuingia kijiji cha Sumbawanga alichokianzisha, aliwataka wananchi waliomfuata watupe uchafu wote kwenye mto Lwiche pamoja na uchawi kisha
waingie wakiwa safi.

Kutokana na imani hiyo watu walitupa uchawi wote na taka nyingine kisha wakaingia kijiji cha Sumbawanga wakiwa wasafi. Aliyekiuka amri hiyo na kuvuka mto Lwiche kutaka kuingia kijiji kipya cha Sumbawanga alikufa katika mto huo.

Hapo ndipo ikawa asili ya Sumbawanga na kijiji kikawa na watu walio wasafi na hakukuwa na matatizo na utawala wa Mwene Ngalu. Alipendwa na kila ilipotokea ishara ya matatizo ndani ya ufipa ilikuwa rahisi kutatuliwa kwa kuwa Chifu Mwene Ngalu aliomba na majibu yalipatikana haraka, hasa kwa imani ya usafi waliokuwa nao.

Hata hivyo Chifu Mwene Ngalu alijaliwa kupata watoto saba ambao wote aliwazalia katika nyumba yake ya utawala iliyojengwa kwa kipindi cha miaka miwili katika mwaka 1918 hadi 1920 chini ya usimamizi wa Mabruda wa dhehebu la Roma yaani wakatoliki ambao walikuwa Wajerumani.

Nyumba hiyo hivi sasa imebomoka na limebaki gofu ambalo kwa nje kuna sehemu ya makaburi yanayotumika kuzika kizazi cha utawala huo, na jambo la ajabu kwenye gofu hilo wapo nyuki waliojenga kwenye pango na wapo kwa muda mrefu tangu kipindi cha uhai wa baadhi ya watawala wa kizazi hicho.

Watoto wa Mwene Ngalu ni Maria wa Ngao, Joseph Kapufi wa Ngao, Thadeo wa Ngao, Teresia wa Ngao, Jacob wa Ngao, Victoria wa Ngao na Antony wa Ngao, ambao baada ya kifo cha mama yao, mtoto wa kwanza Joseph wa Ngao alitawazwa kuwa Chifu wa kizazi hicho na kupewa jina la Joseph wa Ngao-Kapufi wa Pili.

Chifu huyo aliyejaliwa watoto wanne, ambao ni Olanda Joseph, Adolf Joseph, Veneranda Joseph na Yovita Joseph na alipofariki dunia nduguye ambaye ni mdogo wake wa mwisho, Antony wa Ngao alitawazwa mwaka 1989, kuwa Chifu wa Ufipa na kupewa jina la Kapufi wa Tatu. Kapufi huyo wa tatu, Antony wa Ngao, alitawala ufipa tangu mwaka 1989 hadi Desemba 6 mwaka jana alipofariki dunia na kuzikwa kwenye eneo la makaburi ya kizazi cha utawala huo, karibu na jengo la Mwene Ngalu ambalo hivi sasa limebaki gufo tu.

Katika kipindi cha utawala wake, Chifu Kapufi wa Tatu, alijaliwa kupata watoto watatu ambako mkewe wa kwanza alijaliwa kupata mtoto mmoja wa kike aliyeitwa Ntalu na mke mdogo alijaliwa kupata watoto wawili wa kiume ambao ni Oscar na Apolinary. Hata hivyo baada ya kifo cha Kapufi wa Tatu, hivi sasa ukoo huo wa kichifu uko kwenye mchakato wa kutafiti mrithi wa kiti hicho.

Msemaji wa familia ya akina Kapufi Adolf Joseph (61), ambaye ni mtoto wa Chifu Joseph wa Ngao wa Pili, anasema jinsi ya kumpata mrithi huyo ni kwa njia ya kuwashirikisha wazee wa mji huo (wa zamani) walio hai hivi sasa pamoja na wale wa vijiji vya karibu kisha kuteua majina kadhaa na kuyachambua kupata anayestahili.

Anasema jina la mrithi likipatikana sherehe za kumsimika kuwa Chifu wa kabila hilo huanza kufanyiwa maandalizi, na kwa kawaida hufanywa nje ya mji kwa kutengeneza sehemu maalumu ya kumpitishia ambayo huiita mzingo.

Piahuvuka mto Lwiche kwa imani kuwa ni moja ya hatua za kudhihirisha kiwango cha usafi wake kabla ya chifu mtarajiwa kutawazwa.

Baada ya sehemu hiyo kukamilika kutengenezwa chifu mtarajiwa hupitishwa kwa nyuma kuingia kwenye mzingo huo huku akipuliza filimbi tatu, ya kwanza ikikataa kulia hupewa ya pili nayo ikigoma hupewa ya tatu ambayo nayo ikigoma ni dalili kuwa hafai kuwa chifu, hivyo huenguliwa na kutafutwa mwingine.

Adolf anasema ikiwa filimbi moja au mbili zikilia na moja kugoma watampa utawala wa muda huku wakijiandaa kumtafuta chifu mwingine, kwa imani kuwa filimbi zote lazima zilie kwa sababu ni ishara ya sifa njema za utawala za kiongozi anazopaswa kuwa nazo ndipo apewe mamlaka.

Wakati mchakato huo ukiendelea, wa kumpata mrithi wa kiti hicho, mavazi ya Chifu Kapufi wa Tatu, Antony wa Ngao amepewa Vicent Kafumu ambaye ni mjukuu wa Chifu Mwene Ngalu kwa mzaliwa wake wa kwanza aliyeitwa Maria wa Ngao.

Pamoja na hayo yote pia enzi za utawala wa viongozi hao walitumia silaha mbalimbali ambazo hadi leo baadhi yake zimehifadhiwa ili mtawala ajaye akabidhiwe kwa ajili ya kudumisha mila.

Zana hizo ni upinde (ulapwa), mishale (ncheto), fimbo (wasi), mkuki (ilawa) na chombo cha kubebea mishale (untontowaancheto).

Silaha nyingine ni shanga (inkasi) zinazovaliwa mikononi na shingoni kwa chifu, kiti cha miguu mitatu (kisumbi) na vazi la kujifunga kiunoni na mabegani (seketa) ambayo husukwa kwa pamba.

Anasema mabadiliko ya dunia na teknolijia na mapinduzi ya kilimo kwa kiasi kikubwa zilibadilisha mtazamo na fikra za wakazi wa Sumbawanga ambako muingiliano wa watu ulipoanza imani ya uchawi na ushirikina zilipungua na watu wakaingia katika shughuli za uzalishaji mali ingawa baadhi yao wanaendelea na ushirikina kama zilivyo sehemu nyingine nchini.

Mabadiliko hayo pia yalipunguza nguvu ya kuabudu mizimu iliyokuwapo hapo awali kwa kuwa misitu mingi ilifyekwa kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji hivyo, imani ya kuwapo mizimu iliondoka kwa asilimia kubwa na watu wakabakia kuabudu katika nyumba za ibada kufuatana na imani ya dini zao, anasema Adolf.

Hata hivyo bado kuna sehemu au vijiji vyenye kuendelea kuamini mizimu na ushirikina kama vile kijiji cha Chipu kilicho kilomita kama 30 kutoka Sumbawanga mjini na vijiji vya Milanzi na Kalambo ambavyo bado imani ya uchawi na vitendo vya kishirikina vinaendelea kwa baadhi ya wakazi wake.

Kwa kijiji cha Milanzi baadhi ya wakazi wakehutumia mapango yaliyo kwenye mlima uitwao Itwelele kwa kufanya matambiko na mambo mengine ya kishirikina kwa imani kuwa mizimu iliyopo huko huwasaidia kutekeleza mahitaji yao na kumdhuru mtu au watu waliotenda makosa na kuyakana.

Adolf anasema hilo siyo tatizo kubwa kwa sababu hakuna anayemdhuru mgeni anayeingia mkoani hapo kwa kufanya
shughuli zake kama vile biashara au kilimo.

Ila kwa wale ambao hawajafika Sumbawanga hudhani kuwa huo ni uchawi na ushirikina tu, dhana ambayo si ya kweli kwa kuwa maendeleo yanayopatikana katika karibu makabila yote nchini hivi sasa yapo pia Sumbawanga.
 
hilo jumba kwanini lisikarabatiwe na historia hio iwekww vizuri kwa familia kuanzisha museum yao waweke na pucha za toka miaka hio na vitu vingine iwe inawapatia mapato.na kuelimisha kizaz kijacho?

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Hii ni changamoto kubwa sana tulionayo nchi hii haswa ya namna ya ku preserve historia ya zamani kwa vizazi vijavyo, nimeshatembea baadhi ya nchi za huko ulaya na sehemu nyinginezo, kuna system nzuri sana ya kuhifadhi kumbukumbu haswa kama hizi zinahusu kurithishana ufalme n.k, system ambayo nilijitahidi kuonana na wizara husika hapa nchini lakini sijui kama walichukulia umuhimu, tunajitahidi lakini bado sana, sasa embu ona sehemu hio ni gofu tu na halina preservation yoyote..
 
Mtiririko ni mzuri sana uliopangika.mpaka na miaka.Familia za machifu hata hio wana kipaumbele cha kuanzisha Museum zao zza familia na wao wakahitaji mtaalam mkoja tu kuandika hio Chronological order,family tree. Fursa hio wala wasiiache sheria inawapa uwezo wa kuanzisha Museum yao.The antiquity acts of 1962 na amendment yake 1970.wasipoteze historia nzuri hio.mimi nimetembelea nyumba za.machifu ila hii imepangika vizuri sana. aliyekaribu na hao awape maelezo.waweke rekof zao vizuri picha za toka mababu zidurufiwe ziweke displays,vitu hivyo kama mishale.upinde waongezee na kila kitu.wanakosa pesa kweli kweli

Binafsi napanga kwenda huko nionane na wazee niwashauri
 
... nimependa sana suffix ya majina yao - "wa Ngao"; Maria wa Ngao; Joseph wa Ngao; Mwene Ngalu; Mwene Kiatu, etc. safi sana. Wange-maintain na majina yao ya kwanza kwa lugha ya kwao ingekuwa safi zaidi.
 
hilo jumba kwanini lisikarabatiwe na historia hio iwekww vizuri kwa familia kuanzisha museum yao waweke na pucha za toka miaka hio na vitu vingine iwe inawapatia mapato.na kuelimisha kizaz kijacho?

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
... Africans tuko nyuma sana kutunza historia zetu. Kwa ukoo mkubwa kama huo ni ajabu wanashindwa kukarabati hilo jumba. Kapufi/wa Ngao ni kati ya koo zinazojiweza nchi hii ila ndio hivyo, fitna/wivu/majungu ndani ya familia/koo nazo sometimes ni changamoto.
 
Unamik
Mtiririko ni mzuri sana uliopangika.mpaka na miaka.Familia za machifu hata hio wana kipaumbele cha kuanzisha Museum zao zza familia na wao wakahitaji mtaalam mkoja tu kuandika hio Chronological order,family tree. Fursa hio wala wasiiache sheria inawapa uwezo wa kuanzisha Museum yao.The antiquity acts of 1962 na amendment yake 1970.wasipoteze historia nzuri hio.mimi nimetembelea nyumba za.machifu ila hii imepangika vizuri sana. aliyekaribu na hao awape maelezo.waweke rekof zao vizuri picha za toka mababu zidurufiwe ziweke displays,vitu hivyo kama mishale.upinde waongezee na kila kitu.wanakosa pesa kweli kweli

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile ap
Jamaa u must be a genius,no wonder unamiliki tecno😀,ila nimekukubali asilimia Mia,tatizo walioko kwenye system wengi ni vilaza.Kuelewa haya Hadi Magufuli aseme,yapo tu ofisini yanasubiri mshahara ..
 
Tataitu kalesa ..Kama itakupendeza utuletee na historia ya Mwene Maria wa Mpui ya sumbawanga mkuu ..japo ipo taarifa kuwa machifu wote wq mkoa wa Rukwa wana asili ya kitusi
 
Mwene Antony Kapufi Wangao wa III mjukuu wa Mwene Ngalu

PICHA%2020001.jpg
 
Kitabu kilichoandikwa na Mkuu wa wilaya wa enzi za Ukoloni wa wilaya ya Sumbawanga Mr. Roy Willis ambaye alikusanya historia ya kabila la Wafipa na mila zao kutoka kwa ndugu wa ukoo wa Ufalme wa Wafipa.
PICHA%2040001.jpg
 
Mwene Aldorf Kapufi Wangaa IV akiwa na zana zake za Uchifu..huyu mzee wetu alipewa baada ya Anthony wa III
Picture%20032.jpg
 
Back
Top Bottom