Historia ya Joseph Kusaga

Marehemu Abdulhakim Magomelo alikuwa mtu poa sana.

Aliturusha sana kwenye "Yo Rap Bonanza" na concerts nyingune watoto wa mjini wa siku hizo.

DJ Kim mtu mmoja mtaratibu sana, halafu ana akili ya kuweza kukaa na watu wa kila aina, kuanzia wa Uswazi kina GWM mpaka wa Ushuani Masaki IST, wakorofi wa ghetto mpaka Waswalihina.

Alikuwa na apartment yake katikati ya mji hapa Mchafukoge ukipita kidogo tu ilipokuwa Billicanas.

Tulikuwa tunaenda tunapiga stories sana za mambo ya muziki na burudani.

DJ Kim anaandaa concert kubwa sana wanakuja mabishoo wote wa mjini. Wanakuja wagumu wote. Anatuunganusha tunafurahia muziki kistaarabu buka kujali tofauti zetu.

Lakini ukimuona alivyo mpole na mtaratibu hana majivuno hata huwezi kujua huyu ndiye DJ Kim Magomelo.

Umenitajia rafiki yangu umenikumbusha zamani sana Dar. Aliturusha sana.

RIP Kim Magomelo.

Alivyofariki gazeti la This Day lilimuandika hapa.
Home » Columnist
Asante umenikumbusha mbali.
 
Kim&Boyz ndiyo ilikuwa ya Magomelo?...
Enz za kina Digadiga,Black Moses ,Saba Jackson....
Namkumbuka Black Moses, alipanda chati na akaporomoka mwaka 1998 alikuwa singida kwa mama ntilie pakiitwa mrumbani akicheza tunampa bia na kumnunulia ugali nyama choma! Maisha yasikie tuu.
 
Marehemu Abdulhakim Magomelo alikuwa mtu poa sana.

Aliturusha sana kwenye "Yo Rap Bonanza" na concerts nyingine watoto wa mjini wa siku hizo.

DJ Kim mtu mmoja mtaratibu sana, halafu ana akili ya kuweza kukaa na watu wa kila aina, kuanzia wa Uswazi kina GWM mpaka wa Ushuani Masaki IST, wakorofi wa ghetto mpaka Waswalihina.

Alikuwa na apartment yake katikati ya mji hapa Mchafukoge ukipita kidogo tu ilipokuwa Billicanas.

Tulikuwa tunaenda tunapiga stories sana za mambo ya muziki na burudani.

DJ Kim anaandaa concert kubwa sana wanakuja mabishoo wote wa mjini. Wanakuja wagumu wote. Anatuunganisha tunafurahia muziki kistaarabu bila kujali tofauti zetu.

Lakini ukimuona alivyo mpole na mtaratibu hana majivuno hata huwezi kujua huyu ndiye DJ Kim Magomelo.

Umenitajia rafiki yangu umenikumbusha zamani sana Dar. Aliturusha sana.

RIP Kim Magomelo.

Alivyofariki gazeti la This Day lilimuandika hapa.
Home » Columnist
Nini kilimuua?
 
Namkumbuka Black Moses, alipanda chati na akaporomoka mwaka 1998 alikuwa singida kwa mama ntilie pakiitwa mrumbani akicheza tunampa bia na kumnunulia ugali nyama choma! Maisha yasikie tuu.
Baadae akajiingiza katika mambo ya sembe,na umauti kumkuta R.I.P.
 
Joseph M. Kusaga

Joseph Kusaga ni mwanzilishi wa CLOUDS Entertainment Limited, alizaliwa na kulelewa Musoma, mji uliopo kwenye ufukwe wa Ziwa Victoria. Alihamia Dar es salaam akiwa na umri wa miaka 5 baada ya baba yake aliyekuwa mtumishi wa serikali kuhamishiwa kwenye jiji la biashara. Yeye ni mtoto wa nne kwenye familia ya watoto tisa, wavulana watano na wasichana wane.

Kusaga alikuwa na shauku ya muziki tangu umri mdogo sana. Alianza kuandaa matamasha tangu alipokuwa chuoni akisomea Electronics. Ingawa Baba na Mama yake hawakuwa na matumaini makubwa katika kuandaa matamasha, walimwamini na kuwa na uhakika nae, na hatimaye, kwa msaada wa wazazi, na baada ya kipindi kifupi alikuwa DJ maarufu na mtayarishaji matamasha.

Alipata wazo la kuanzisha kampuni ya vyombo vya habari wakati wa ziara yake nchini Marekani alipoishi New York City na Los Angeles na kuvutiwa na hali ya muziki wa sehemu hiyo. Alipokuwa Los Angeles aliungana na mbia mwenzake wa biashara wa muda mrefu Ruge Mutahaba na kuanzisha mpango wa kufungua kituo cha redio nchini Tanzania ambacho kitajulikana kuwa ni CLOUDS FM.

CLOUDS-ambacho ni kifupisho cha Cool, Lovable, Outrageus, Unique, Dynamic, Sound ilianzishwa mwaka 1998 nakukua na kuwa miongoni mwa vyombo vya habari maarufu sana nchini Tanzania. Hivi sasa Clouds Entertainment Limited inajumuisha Clouds FM, PrimeTime Promotions, Choice FM, Coconut Radia Station, Clouds TV, Ngoma Web Tv na Kitangoma Magazine.

Upo wasifu wa Clouds Television katika Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ambapo Alex Mkama Kusaga ana (25%) ya hisa, kama alivyo Joseph Kusaga. Clouds Entertainment Limited ina 50% ya hisa. Wamiliki wa sasa wa hisa za Clouds Entertainment ni Joseph Kusaga 50%, Judith Violet kusaga 10%, Sheba Martha Kusaga (10%) Dogan Andrew Kusaga (10%), Joyce Alex Kusaga(10%), Alex Justine Kusaga (5%) na Prisca Mkama Kusaga (10%) .
i
na maana Ruge hakuwa na shea
 
Hii mbona sio full story na je kusaga Kwa sasa ni muumini wa dini ya kiislamu ila bado anatumia jina la Joseph?
 
Hii historia haijakamilika kabisa either aliyokuwa anaiandika alikuwa anakimbizwa au hakuwa anajua anachotuandikia ilikuweje ghafla tu alipofika Dar akahamia Marekani hakuna maelezo ya kutosha.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Stori za kijiweni

Inasemekana eti ruge alikuwa na wazo la radio. Kipind wanakutana na kusaga huko marekani ila baba ake ruge prof. Mutahaba hakuwa mpenz kabisa wa music so hakufurahishwa kabisa na mwenendo wa ruge na ndo maana jamaa hata chuo hakuwa na maendeleo mazur so ruge alipeleka wazo kwa mzee wake akakataa kumsupoort ndo ruge akamwambia rafik ake kipenz kusaga kusaga akapeleka kwa wazaz wake baada ya majibizano ya muda mrefu ndo wakakubaliana kwamba mzee kusaga atachukua mkopo benk kwa ajili ya kuanzisha hyo studio ila wamiliki watakuwa kusaga family na ruge yy atakuwa mkurugenz mwenza na joseph ndo hvyo ikawa jamaa hajawah kumiliki CLOUDS ila alikuwa na say kubwa kwa sababu yy alikuwa na wazo lote la media
Maanake kwamba ruge ni promoter, wataalamu wa company law wanaelewa...
 
A
Hemu tuleteeni historia inayoendana na uharisia wa kijana bana yaani unaandika tu

“eti alipendezwa na muziki akaamua kufungua TV yake na mbia mwenzie”

HOW inamaana kijana wowote leo akipendezwa afunguo kiwanda cha maji Safi anafungua tu kwasababu alipendezwa, tunataka kujua MTAJI aliupata wapi, aliupataje ??
Akikujibu hilo niite fisi maji nipo hapa nyuma ya phone's keypads
 
Shule ya msingi alisoma wapi? Inaitwaje?
Shule ya sekondari alisoma wapu?inaitwaje?Chuo kikuu alisoma wapi ? Kinaitwaje?
Mtaji alipata wapi?
Alifanya kazi kwanza kabla kuanzisha vituo vya habari ?
Anafamilia ya watoto wangapi ? Single or married.

Andika wasifu wa Mtu Vizuri Mkuu
Wasifu wake unapungufu au unafahamu kidogo
I see something missing?
Janja janja tu huyo mla asali ya maskini enzi hizo (wasanii)..

Washukuriwe wasafi media kuwaumbua hatimaye wasanii wameanza kula jasho lao
 
Back
Top Bottom