Historia ya Hayati Abeid Amani Karume iliyosimuliwa na Global TV inapotosha

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,199
10,932
Kuna historia ya raisi wa mwanzo wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume inayosimuliwa na Dennis Mpagaze na Ananieli. Hii historia inamwita Karume ndiye aliyewatoa wazanzibari utumwani. Na kila ilipotaja waarabu imewataja kwa sura mbaya sana.

Hawa jamaa inaonekana wana ajenda maalumu kwa Zanzibar na hawana haja na historia ya kweli. Wangekwenda kumhoji marehemu Ameir bin Ameir wa Bwejuu Zanzibar kabla ya kifo chake mwezi uliopita kwani anavyomfahamu Karume aliyeishi naye visiwani humo na kumshuhudia tangu udogo wake ana historia tofauti na akina Dennis.

Zaidi ya hivyo utumwa ulishaondolewa duniani zamani kabla hata Karume hajazaliwa inakuwaje tena gobal tv wanasema yeye ndiye aliyezaliwa ili aje kuuondosha. Nani hao waliokuwa wakiendeleza Utumwa.

CC Mohamed Said
 
Kumbe bado hujui nini maana ya utumwa. Utumwa bado upo hadi leo kwa tarifa yako.

Enzi kabla Karume hajafanya mapinduzi* zenji ilikuwa iko kwa Waarabu wakiwa vibaraka wa Waingereza. Watu weusi wa Zenji walikuwa bado utumwani wakibaguliwa kwa kila namna.

Hivyo Karume na kina Okelo ndio waliouondosha huo utumwa wa Kiingereza na Kiarabu.
 
Umesema utumwa mpaka leo upo.Huo Utumwa upo wapi na wapi na jee Karume kumbe ni kazi bure hakufanikiwa.Kwa hivyo Global tv ni wapotoshaji tu.
 
Si historia ya Karume senior tu ndio inapotoshwa, kwa nchi hii historia ya mambo mengi tu inapotoshwa au kwa kutokujua au kwa makusudi! na bahati mbaya sana hao wanaojifanya kusimulia historia hizo hawataki ama ni wavivu wa kujifunza. Mfano historia ya mapambano ya kuleta uhuru nchi hii imepotoshwa kwa sehemu kubwa! hata historia ya mapinduzi ya Zanzibar!
 
Watu kama hawa global iwapo wanapotosha mambo yaliyotokea nchini mwao tutawaamini vipi wanaposimulia habari za nje ya nchi kama Sudan.Mwisho wa historia yao kuhusu Karume eti walimuhoji mkuu wa mkoa mjini Magharibi.Wanasiasa wachanga kama hao hupati lolote la maana.
 
Kuna historia ya raisi wa mwanzo wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume inayosimuliwa na Dennis Mpagaze na Ananieli. Hii historia inamwita Karume ndiye aliyewatoa wazanzibari utumwani. Na kila ilipotaja waarabu imewataja kwa sura mbaya sana.

Hawa jamaa inaonekana wana ajenda maalumu kwa Zanzibar na hawana haja na historia ya kweli. Wangekwenda kumhoji marehemu Ameir bin Ameir wa Bwejuu Zanzibar kabla ya kifo chake mwezi uliopita kwani anavyomfahamu Karume aliyeishi naye visiwani humo na kumshuhudia tangu udogo wake ana historia tofauti na akina Dennis.

Zaidi ya hivyo utumwa ulishaondolewa duniani zamani kabla hata Karume hajazaliwa inakuwaje tena gobal tv wanasema yeye ndiye aliyezaliwa ili aje kuuondosha. Nani hao waliokuwa wakiendeleza Utumwa.

CC Mohamed Said
Hivi kweli mtu mwenye uelewa utasikiliza au kusoma historia ya vitu, watu au matukio kwa kutumia source kama hizi za kina Ayo, Global nk? Anyaways ni vizuri ume-alert wanaopenda kufuatilia makanjanja kama haya.
 
Haya makanjanja katika teknolojia ya kisasa yanawafikia watu wengi zaidi ndio tukasema wanapotosha.Bahati mbaya katika hali hii hakuna sehemu ya kuchuja kinachokwenda hewani na usishangae hata wanafunzi wa historia wa vyuo vikuu wakawa wanatumia uoza huu.
 
Umesema utumwa mpaka leo upo.Huo Utumwa upo wapi na wapi na jee Karume kumbe ni kazi bure hakufanikiwa.Kwa hivyo Global tv ni wapotoshaji tu.
Mzee inamaana hujui waafrika wengi wakimbizi nchi kama somalia,ethiopia,Sudan nk. wanakuwa Hijacked na kupelekwa kugeuzwa Watumwa especially nchi za kiarabu?
Hii sio miaka ya 60 hii ni ongoing issue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom