Historia na chimbuko la Jamii ya Waarabu

Internal

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
3,575
3,894
Habarini wanajamvi.. Nipende kuwapongeza mashujaa wote wa jukwaa LA inteligence mnatupanua akili kwa nyuzi zilizojaa mambo mapya kila wakat.
Mwisho wa kushukuru niwakaribishe kwenye thread moja kwa moja.

Ikiwa Leo ni tar 19 July 2017 Ikiwa ni siku ya 200 tangu tuuanze mwaka 2017 zikiwa zimesalia siku chache tu kuumaliza mwaka 2017(165zimebakia).

Ni siku ya kihistoria kwani ndio siku pekee ambayo waafrika wenzetu wa uarabuni wanatimiza miaka 1306 toka mwaka 711 walipoiangusha ngome ya jeshi LA wagoti was magharibi huko nchini uhispania.

HISTORIA YA WAARABU

Leo duniani kuna watu wengi wanajinasibisha na waarabu wakiwa wanaishi Bara Arabu,mashariki ya kati, au kwingineko ulimwenguni.

Watu hawa ambao wanatofautiana rangi, kimaumbile, kisura baina yao wote wanadai kuwa ni waarabuau asili yao ni uarabuni.

Walakini ni nani hasa hawa waarabu na nini asili yao?


ASILI YA WAARABU

Waarabu wote ulimwenguni wametokana na jadi moja tu ambayo no mtoto wa nabii nuhu aitwaye SAM lakini baadaye waligawanyika katika makundi matatu.

1.Waarabu ( AL-BAIDA)

Hawa in waarabu ambao Leo hawapo tena ulimwenguni kwasababu ya kaumu yao kuteketezwa na mwenyezi Mungu kwa kutokutii maagizi yake.


Kaumu hizo zilizoteketezwa ni ksumj ya HUD ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina LA A ad na kaumu ya saleh iliyokuwa ikijulikana kwa Nina LA Thamud. Kaumu hizi mbili ziliteketezwa kwa kutokufuata maagizo ya mwenyezi Mungu.

2.Hawa nao in waarabu waliotokana na mtoto wa nabii HUD ajulikanae kwa jina LA Qattaan na kutokana na kizazi chake ndio hawa waarabu wanaoitwa Al-aribawakaenea kila upande.

Waarabu hawa ambao makabila yao makubwa yalikuwa ni Himyar na Kahlaan walikuwa wakiishi Yemeen na kuwa na ufalme na ustaarabu mkubwa Yemen mpaka yalipotokea mafuriko makubwa Yemen yakawatawanya na kuwasukuma kwenda sehemu nyingine mbalimbali za Bara LA Arabu na shamu na Iraq misri na Afrika mashariki.

3. Waarabu AL-Masyaariba.

Nao ni waarabu waliotokana na nabii Ismail ambaye aliletwa na baba yake Ibrahim na kumuweka katika binds LA makka pamoja na mama take hajiri yule mjazi wa ibrahimu na kuachwa hapo kwa amri ya mwenyezi Mungu.

Nabii Ismaili hakuwa muarabu lakini baada ya kukaa hapo makka na kufufuka chemchemi ya zamzsmu,walikuja waarabu wa kiyemen wa kabila LA jurhum nacwapoona maji hapo waliombavkubaki hapo na ndipo nabii ishmail akakulia kwenye kabila hilo, kwahiyo kizazi chake kiliinukia kuwa waarabu kwa kuchanganyikana na waarabu was Yemen.

Maskani ya waarabu ya asili

Kama yulivtyooan hapo awali kuwa mwanzo kabsa walikuwa wakiishi Yemen lakini baadaye wakaanza kutawanyikaka kwenye sehemu nyinginezo za Bars Arabu. Na kwakuwa wengi wao walikuwa wakiishi kibedui ya kusafiri mahili pamoja kwenda kwingine kutafuta chakula na maji kwa nafsi zao na wanyama wao waliweza kuenea sehemu zote za Bara Arabu. Iraq, Misri, A. Mashariki na Kaskazini.

Kigawanyika huku kulizidi kasi baada ya kuvunjika bwawa lao kubwa lililopo maarib huko Yemen lililokuwa likilimbikiza maji mengi kwaajili ya ukulima, bustani, pamoja na malisho yao ya wanyama wao na mtawanyiko mkubwa wapili ni baada ya kuja kwa uislamu na kuhitaji kuupeleka kwa watu mbali mbali ulimwenguni kusud kueneza ujumbe wake na ndio maama Leo tunaona waarabu katika kila bara.

Jimuiya ya nchi za kiarabu.

No ushirikiano wa nchi za Afrika kaskazini na Asia ya magharibi. Jumuiya hii ilianzishwa hasa na nchi za waarabu.

Imepokea pia nchi kama komori zidizoongea kiarabu kama lugha rasmi.

Nchi Wanachama.

1.. Zilizoanzisha mnamo tar 22 march 1945. Ni misri,Iraq,Jordan,Lebanon,Saudi,Arabia,srya,pamoja na Yemen kama chimbuko.

2.. Zilizojiunga baadaye

Ni Libya, moroko, Sudan nk

DINI

Watu wengi sana ulimwenguni wanafikiria kuwa dini ya waarabu ni uislamu. Lakin ukweli ni kwamba kuna idadi kubwa ya waarabu waliopo nchi mbalimbali zinazoinda umoja wa waarabu na zisizounda umoja huo ambao ni wakristo na wengine ni waumini was dini yofauti tofauti na sio waumini wa dini ya kiislamu.

Hii kutokana na kwamba kabla ya uislamu uliokuja na mtume Muhammad walikuepo waumini mbalimbali wa dini mbalimbali ikiwemo ukristo.

Asanteni... Wakuu it my first time kuleta Uzi umu ikiwa kuna error nisichelewe kuomba radhi.
 
Ningelipenda sana siku nyingine utupatie historia ya sisi waAFRIKA nasi nipate kujua chimbuko letu ni nabii nani? haiwezekani historia itutenge!
 
Back
Top Bottom