Kyungai
Member
- Sep 30, 2022
- 16
- 2
Leo nimepata kusikiliza chimbuko la kabila linalopatikana Arusha chini ya vilima vidogo vidogo chili ya Mlima mkuu Meru
Asili
Kabila hili limetoka katika milima ya usambara na kusogea katika mkoa wa kilimanjaro miaka 800 iliyopita ambapo kila walilpo pita waliacha alama, ambapo waliishi na kuchanganya Tamaduni na watu wa Kilimanjaro hususani maeneo ya Siha na Machame.
Mgawanyiko
Kabila hili liligawanyika katika makundi mawili baada ya kuishi Kilimanjaro kwa muda mrefu na kuanza kutokea kwa ugomvi ambapo kundi la kwanza waliitwa 'Varwa' ikimaanisha wapandaji milima ambao walielekea chini ya mlima meru hasa Sakila, wakiwa na koo kama Mbise, Akyoo, Pallangyo. Kundi la pili walibaki maeneo ya Siha na Machame ambao walijulikana kama 'Shami'
Asili ya jina Varwa na Wameru
Varwa hili ndio jina halisi la kundi la kwanza ambalo linamaanisha wapandaji hasa milima ambao wenyewe
walijenga na kuelekea zaidi kaskazini hasa Sakila
Wameru kuna nadharia mbili la jina Wameri
1. Jina wameru limetokana na kabila hilo kukaa chini ya mlima Meru hivyo kuitwa Wameru japo kiuhalisia hawa sio Wameru ni kundi la Varwa
2. Jina Wameru limetokana na vita iliyopigwana kabla ya ukoloni ambapo wanaume wengi wa jamii hii walichukuliwa mateka hivyo wanawake wakawa wanalia wakisema 'Omi Veeru' wakimaanisha 'Wame zetu' hivyo kupelekea wageni kutamka maneno 'Omi Veeru' kama 'Wameru'
Uthibitisho wa Kinadharia wa Wameru/Warwa na Wamachame/Shami
1. Koo
Kuna baadhi ya koo ambazo zinaonekana kuwepo kwa makundi yote mawili ya Meru na Machame mfano Urio, Ayo, Urassa, Ndossi nk
2. Majina ya Kimila ya Wameru
Kuna baadhi ya kimila wanayoitwa Wameru ambayo yana uhusiano wa moja kwa moja na Machame mfano Silaa, Massawe, Sawe, Urassa, Murassa, Swai, Maswai, Mamboroo. Kimaro nk
3. Ukaribu wa maneno na lugha
Lugha ya Kimeru/ Kirwa ina ufanano kiasi fulani na kimachame ambapo maneno mengi yanaonekana kuwa na maana sawa kwa kabila zote mbili.