Hisia za mapenzi zikifa unafanyaje?

Hisia za mapenzi zikifa unafanyaje?

Kuna kitu kinaitwa kukinaii...!! Ukishamzoea sana mtu unamkinaii yani sawa na demu kabla ya kumpata unamuona mzurii ilaa ukishampataa sasaa
Unamuona wa kawaida kinachokuvutia kwakwe ni matamanio kuna mengi katika mawazo yako juu yake au na yeye kajiweka wa kawaida sna kiasi kwamba hana ashiki tena
 
Wengi hapa wanaongea nadharia zaidi ya uhalisia. Kiukweli hata mwanamke awe mzuri kama malaika, ukishaishi nae kwa muda fulani ndani, mnalala, mnaamka kila siku.. hua unaanza kumuona wa kawaida tu na hisia nae zinaisha, awe amezaa au hajazaa. Kama amezaa ndio hali inakua mbaya zaidi!

Ndio maana kuna wakati watu hua wanashangaa eti jamaa mbona mke wake mzuri lakini anachepuka na demu wa kawaida kabisa? Ni kwasababu huyo mzuri umeshamzoea na hakusisimui tena.

Ndio maana mimi siku zote nawaona ndugu zangu waislamu wapo sahihi sana kuruhusu mwanaume aoe hadi wake wanne. Hayo mengine ni kujipa moyo tuu sijui muende hotelini.. mtaenda hotelini mara ngapi? Kila wiki? Kumbuka hapa tunaongelea mfano mke wa ndoa ambae upo nae from january to december
Ila hata nyie wanaume huwa mna tu chosha hamna unakuta hamna hamtu *** vizuri. In short ukikaa na kitu kimoja kinachosha ni Kama kula maharage daily. Vile wanawake huwa hawasemi na kupiga kimya ndio maana inatakiwa ukiwa na mtu umpende Toka moyoni ngono isiwe kiupaumbele, maana apart from ngono mwenzi wako ana offer kitu gani zaidi extra?
 
ukiona umemchoka mtongoze tena kwa mara nyingine..sisi huwa tunaita system update

Kama Hard disk imekuwa kubwa au Ndogo Maana kuna vitu vitashindwa kukaa sawa kwa sababu ya ku update system

Alafu kuhusu swala la Kumtongoza tena changamoto iko kwenye vitu hivi
-Vocha ya simu ili uwe kila wakati unapiga simu na kutuma sms
-Lakini pia mazingira wakati huo alikuwa kwao lakini leo yuko kwako(Kwake)
-Na kama kuna viumbe vimeongezeka pia nalo sijui linawekwaje ila kubwa sana Me na nadhani kukumbuka mazuri yake na kupunguza kama sio kumaliza kabisa FRIEND MATCH maana hizo ndio hasa zina sababisha ulinganifu bila kujua kuna kitu kina Kinaitwa Margina utility
 
Ila hata nyie wanaume huwa mna tu chosha hamna unakuta hamna hamtu **** vizuri. In short ukikaa na kitu kimoja kinachosha ni Kama kula maharage daily. Vile wanawake huwa hawasemi na kupiga kimya ndio maana inatakiwa ukiwa na mtu umpende Toka moyoni ngono isiwe kiupaumbele, maana apart from ngono mwenzi wako ana offer kitu gani zaidi extra?
Kama haku.....vizuri na zamani alikuwa anakut...... vizuri ,jichunguze tatizo linaweza kuwa kwako mwenyewe
 
Mkuu uliposema ,issue ya kemikali,hormone, hebu fafanua zaidi nahic kuna vingi hatuvijui
 
Kama haku.....vizuri na zamani alikuwa anakut...... vizuri ,jichunguze tatizo linaweza kuwa kwako mwenyewe
Kama hafanyi vizuri kanikwaza Sina hisia naye, naona Hana jipya, mahusiano ni complicated sana
 
Ukweli ni kwamba wanawake wakijifungua watoto kadhaa hubadilika sana. Na kama hajiangalii akajiachia tu anaweza kuchakaa mapema sana. Sasa kama ulimpendea wembamba wa tumbo, sijui ngozi laini ndiyo utajijua. Na wakati mwingine hata misambwanda hupotea. Yaani mkeo aliyekuwa na msambwanda wa kutingishika sasa kazaa watoto wawili kajiachia kenenepa jumla kama vile kavaa ovaroli hata msambwanda huwezi kuuona tena. Hata akipita unamwangalia kwa jicho la kuibia unajisemea kimoyomoyo dah hapa nilipiga chini kuchagua.

Kama mdau alivyosema hapo juu, mwanaume una wajibu pia wa kuhakikisha kuwa mapenzi hayafi. Hakikisha mkeo anavaa vizuri. Anajipamba. Manukato uyapendayo. Kama unene wake unakukera fanyeni mazoezi pamoja. Mitoko (dates) angalau kwa mwezi mara mbili. Sehemu nzuri tulivu ambako mtakaa tu na kutathmini penzi lenu kwa ujumla. No hard talk. No ishu za watoto. No ishu za pesa. Just simple light talk. Mkumbushe kuwa bado unampenda na kama kuna kitu unakimisi mwambie. Open communication. Na wewe muulize kama kuna kitu anataka uwe unafanya ili kumsisimua. Yaweza kuwa ni kumsaidia jikoni akiwa anapika. Au kutandika kitanda pamoja kama mlivyokuwa mnafanya zamani. Au hata kumpaka mafuta na kumkanda kidogo akitoka kukoga au akitaka kulala. Wakati mwingine utakumbushwa kuwa mume wangu siku hizi wala huniambii kama unanipenda. Nakumisi sana mume wangu. Vitu vidogo ulivyokuwa unafanya zamani na sasa huvifanyi tena. Vizawadi vile vidogo vya kichokozi ulivyokuwa umemzoesha...

Mapenzi ni hisia na hisia, japo ni suala la kikemikali na homoni, saikolojia pia ina nafasi kubwa sana. Na mara nyingi ni vitu vidogo dogo tu...

...na jambo la muhimu sana ni kusali pamoja kama wote ni waumini. Hakuna jambo linaloleta amani ya kweli kwa wapendanao kama kupiga magoti mbele ya Mungu mkilia pamoja na kumkabidhi Mungu mapungufu yenu na kumuomba awasamehe ili nanyi msameheane na kuanza upya. Pure spiritual and emotional karthasis kwa wapendanao...

Tunachokosea sisi wanaume ni ile kuona hisia zimepungua na badala ya kutafuta suluhisho tunaamua kukata njia ya mkato kutafuta mchepuko ambao utakuwa unatufanyia yale ambayo tungependa wake zetu ndiyo watufanyie. Mapenzi nyumbani hakuna na watu mnaishi tu ali mradi mpo. Frustrations, tension na stress kibao hasira nje nje mwishowe hata maana ya ndoa inakosekana.

Wanandoa Mungu na Awasaidie

"kama amevaa ovaroli"
 
Ukiongea na wanandoa wale walokuwa kwa ndoa kwa muda mrefu watakwambia hicho ni kipindi ambacho karibia kiiiila ndoa hupitia, haijalishi hata kama ulioa malaika. Na ndicho kipindi kigumu kweli na kipimo cha uvumilivu wenu. Mkivuruga hapo basi anniversary mtaishia kuzisikia tu kwa wenzenu.

Mambo mengi sana hupelekea maana kadiri mnavyoishi, maisha na majukumu pia hubadilika na kuongezeka. Wanaume hukimbilia kuwaona wanawake tu ndio wamepoteza mvuto ila hata wao hupoteza mvuto. Ndio ile unatamani mumeo hata asafiri angalau upumue maana kumuona kila siku hutaki hata hisia nae huna tena.

Nimekumbuka kuna mama yeye mumewe kahamishiwa mkoani ila kagoma kumfuata maana kwanza imekuwa ni furaha kwako wao kuwa mbali mbali. Anadai amechoka suffocation na hana hamu tena na mumewe.
 
Ukiongea na wanandoa wale walilokuwa kwa ndoa kwa muda mrefu watakwambia hicho ni kipindi ambacho karibia kiiiila ndoa hupitia, haijalishi hata kama ulioa malaika. Na ndicho kipindi kigumu kweli na kipimo cha uvumilivu wenu. Mkivuruga hapo basi anniversary mtaishia kuzisikia tu kwa wenzenu.

Mambo mengi sana hupelekea maana kadiri mnavyoishi, maisha ma majukumu pia hubadilika na kuongezeka. Wanaume hukimbilia kuwaona wanawake tu ndio wamepoteza mvuto ila hata wao hupoteza mvuto. Ndio ile unatamani mumeo hata asafiri angalau upumue maana kumuona kila siku hutaki hata hisia nae huna tena.

Nimekumbuka kuna mama yeye mumewe kahamishiwa mkoani ila kagoma kumfuata maana anadai amechoka suffocation na hana hamu tena na mumewe.
Huwa nashangaa wanaume kulaumu wake zao, huwezi linganisha uchumba na ndoa na mkishapata watoto na majukumu huongezeka.
 
Huwa nashangaa wanaume kulaumu wake zao, huwezi linganisha uchumba na ndoa na mkishapata watoto na majukumu huongezeka.
Hawalionagi hilo, huwa wanafikiri ni sisi tu ndio hupoteza mvuto.
 
Hawalionagi hilo, huwa wanafikiri ni sisi tu ndio hupoteza mvuto.
Wao hukimbilia kulaumu tu, hata ukiwa tu kazini huwa Kuna mda unachoka na hyo kazi au Mambo mengine tu na solution sio kulaumu kazi ni wewe tu kutokutaka kubadilika.
Hali nyingine hyo huwa ni stress tu inabidi kutafta wataalamu basi.
 
kweli nimeamin tabia has nothing to do kitandani
 
Kama tatizo ni kutokufanya Vizuri mwambie tu,Ila Kama huna hisia huwezi kumwambia
Una mwambia ukweli na yeye ukute ana feel same situation unayopitia. Shida watu huwa hawawi wawazi kwenye mahusiano, Mimi ningemwambia tu ikiwezekana mupeana distance kwa mda
 
Inategemea zmekufa mda gani unatoa taarifa kwa watu wako wa karibu kwanza wakati unaendelea na taratibu nyingine,taratibu nyingine hapa nadhani nimeeleweka (katamtipandamti)usilazimishe kuzifufua kwani utaishi kw wasiwasi siku zako zilizobakia
 
Back
Top Bottom