Nolelo Nobert
Member
- Mar 22, 2016
- 22
- 18
Tafakari Huru:
Katika tathmini yangu ya kimazingira,sisi kama watanzania, tunashuhudia majanga mengi sana ya kimazingira, nadhani kwa upofu tulionao bado hatujaona ni kitu cha kushitusha kutokana na madhara mengi yanayotokana na majanga hayo bali tunaona na kufikiri ni sababu ya nguvu za asili au kwa kuamini kuwa labda ni ghadhabu ya mwenyezi mungu, jibu laweza kuwa ni ndio kiimani au kwa kukosa maono ya kimaarifa juu ya matatizo haya, kwa kuwa na mtizamo mpana wa kuliona na kutambua tatizo kuanzia kwenye mizizi kwa kuunganisha matukio na sababu halisi zinosababisha tatizo husika. Hii ni falsafa na imani iliyojenga mizizi katika maisha yetu ya kila siku, yakuona matatizo mengi yanayotukumba hatujahusika kabisa katika uwepo wake katika maisha yetu, iwe katika nyanja ya kimazingira,kijamii,kiuchumi ama kiutamaduni, zaidi yakutoa lawama kwa wengino kuwa wao ndio chanzo cha shida zetu.
Katika kujadili, leo nitajikita zaidi katika nyanja ya kimazingira ambazo miongoni mwa tulio wengi hatuoni tija katika kuizungumzia kama ni moja ya mihimili wenye tija katika ustawi wa maisha yetu ya ndani na nje ya miili yetu. Hivyo hatuna muda wa kufanya jitihada zozote za maksudi katika kutatua changamoto katika upande huu wa kimazingira, ambao nitajaribu kuangazia maeneo kadha wa kadha katika mjadala huu kwenye andiko hili;
Mfano suala la taka ngumu na taka maji katika jiji la Dar es salaam na kwingineko, kama ni mkazi wa eneo tajwa ama kwa kuwa mhanga au kukerwa na changamoto hii, ambayo kwa hakika imeota sugu katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam, utiririshaji wa maji machafu,taka kutupwa miferejini, madampo bubu, mifuko ya plastiki kila upigapo hatua, mabonde yamegeuka ndio dampo na pindi mvua zinaponyesha huzisomba na kuzipeleka baharini ambako madhara yake hayasemekeki,
Kwa uongozi uliopita kulikuwa hakuna jitihada zozote za maksudi juu ya kulipa kipaumbele tatizo hili, hivyo kila ambaye ukijaribu kumpelekea tatizo hili, majibu yao yaridhihirisha kabisa kukata tama na kuona tatizo limezidi uwezo wao na hivyo hawana namna yakulishughulikia( they felt overwhelmed with the situation, they have nothing to do with it). Tumaini jipya likaonekana baada ya uongozi wa awamu ya tano wa raisi Magufuri kutoa tamko juu ya Usafi nchi nzima baada ya kusimamisha shughuli za kusherekea sherehe za uhuru, nakutumia siku hiyo kama siku ya usafi, ndipo watanzania wakaona uwezekanao watatizo hili kupata ufumbuzi upo. Hivyo toka tamko hilo limetolewa naweza kusema kumekuwa kuna mjongeo wa namna Fulani katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu juu ya changamoto ya taka katika jiji la Dar es salaam.
Katika kutizama athari na madhara ya uharibifu wa mazingira iwe kwa kuchoma taka, utirishaji wa maji machafu mtoni kutoka majumbani na viwandani au utupaji wa taka kwenye mitaro au mabondeni na kwenye makazi yetu, sina hakika kama tulishawahi kutafakari kwa kina juu ya athari za tabia hizi kwa afya zetu na mazingira kiujumla? Swali la kujiuliza kiasi gani Maradhi mengi yakibinadamu yanaotakana na udhibiti mbovu wa taka hizi? je ni kiasi gani cha kipato chetu huelekezwa kwenye kutibu magonjwa yanayosababishwa na uchafu wa mazingira yetu? Ambao wachafuzi wakubwa ni mimi na wewe, jibu rahisi ni hapana.. kwasababu maralia inasabishwa na mbu wa Anoferesi, kipindupindu kinasabishwa na bacteria wa vibrio kolerai, homa ya tumbo, labda wameniroga na kansa ni Mungu labda amependa au shetani anafanya kazi yake(kiimani). Ni upofu na ubutu wa macho yetu kushindwa kuona uhusiano mkubwa wa mazingira yetu na afya zetu. Hapa ningependa ni mnukuu mmoja kati wadau wakubwa wa mazingira wa hapa nchini Tanzania, mkurugenzi wa taasisi ya Nipe Fagio Tania Hamilton, anasema (rivers and storm drains are very much like our blood veins. When they are polluted we get sick) ukichafua mfereji umechafua mto, hivyo huwezi kuepuka maradhi kwa kuleta madhara sehemu moja kwa kuwa hayo maji ya mto ndio yanayoelekea baharini, hivyo ni uchaguzi wako mwenyewe kuhatarisha afya ya familia,jamii na taifa kwa ujumla ama kuokoa nafsi za mamia ya watanzania kwa kuweka mazingira yako safi. uchaguzi ni wako.
Mfano katika kutibu suala la Maralia,jitihada nyingi zingewekezwa katika kuhamasisha jamii kuweka mazingira safi, kwa kuhakikisha sehemu zenye nyasi zinafyekwa,madimbwi na maji yaliyotuama yanaondolewa na taka taka ngumu zenye kuhifadhi maji zinadhibitiwa ipasavyo, kwa maana hayo ndio makazi ya Mbu, Mbu wakitoweka maralia itatoweka, lakini unahamasishaji wa kutumia vyandarua wakati watu wanaishi kwenye madimbwi na uchafu uliotopea, maralia itakwisha vipi?
Rai yangu, Nakumbuka nilivyokuwa chuoni nilisoma kozi moja inaitwa Disaster management (Udhibiti wa majanga). Nikajifunza njia pekee kukabiliana na majanga ni kuweka jitihada kuzuia janga lisitokee au hata likitokea liwe na less impact kwenye jamii husika( Pro actives measures) rather than responding to the disaster after massive impact to the particular society (Re active measures), nadhani wanauchumi wanajua kudhibiti tatizo lisitokee na kutibu tatizo likisha tokea gharama kubwa ni ipi ? wenyewe wanaita (cost benefit analysis). Nadhani tufike wakati tubadilike tuache kufanya kazi kwa mazoea, la sivyo tutakuwa na mashtaka makubwa sana kwa mwenyezi Mungu kwa kusabisha vifo vya watanzania wasiokuwa na hatia, ambavyo chanzo kikubwa ni uzembe wetu wakutokufikiri kwa weledi ambao tumeupata kupitia kodi za watanzania.
Uzembe huu umekuwa ukijidhihirisha kwenye kila janga linalotukumba iwe ni mafuriko,ukame,njaa,migogoro ya wakulima na wafugaji,magonjwa na umaskini, yote hayo ni matokeo ya uharibifu wa mazingira yetu, ambao hatuoni kuwa ni tatizo linalohitaji jitihada za haraka kunusuru uhai wa watanzania.
Mimi kama mdau wa mazingira napendekeza wadau wamazingira,watu binafsi,viwanda,taasis, wizara husika za afya na mazingira, kwa umoja wetu na nguvu zetu tufanye juhudi za maksudi za kutafuta suluhu ya kudumu na yenye tija kutatua matatizo yetu, hasa haya ya kimazingira.
Niongeze kuwa suala la uhifadhi bora wa mazingira ni suala Mtambuka, katika dunia ya sasa,na hata mataifa makubwa hayana mchezo katika suala la uhifadhi wa mazingira, hivyo nasi hatuna budi kulipa kipaumbele suala hili. Mimi naamini, mazingira yakiwa safi matatizo ya umaskini,uharifu,magonjwa na Njaa vitakuwa ni kitendawili miongoni mwa wakazi wa maeneo ya hali duni. “When you solve the small dragons, the bigger will take care themselves”
Mwisho, kila mmoja wetu kwa nafasi yake, awe mstari wa mbele katika kuelimisha jamii umuhimu wa kuweka mazingira safi.