Hisia ni nini?🤔


You deserve a platinum membership 🫡

Nimeelewa vizuri sana kwamba moja ya kazi ya hisia ni kukusukuma kufanya kitu ambacho, kama ungetumia akili pekee, pengine usingefanya kwa sababu akili isingekuruhusu. Hapo sawa kabisa nimeelewa

Sasa swali linakuja
Je, mtu ambaye anaendeshwa zaidi na hisia anawezaje kujicontrol na kuacha tabia ya kutumia hisia pale ambapo alipaswa kutumia akili zaidi?
 
Hisia ni hali ya ndani ya akili na mwili inayokufanya uhisi jambo fulani kihisia—kama furaha, huzuni, hasira, hofu, au upendo. Ni namna ubongo wako unavyoitikia kile unachopitia au kufikiria.
hisia zinahusiana na:
Ubongo (hasa sehemu kama limbic system)
Homoni (mfano adrenaline, dopamine)
Mwili (mapigo ya moyo kuongezeka, jasho, n.k.)
Kwa hiyo, hisia si mawazo tu—ni mchanganyiko wa mawazo + mwitikio wa mwili + uzoefu wa ndani.
 

Kuinua EQ ni mchakato wa kujifunza na kujiboresha kila siku wanaita kujenga kujitambua, emotional awareness. Kadri unavyojielewa na kuelewa wengine, ndivyo unavyokuwa kiongozi bora, mfanyabiashara mzuri, na mtu mwenye mahusiano imara.

Tunaanza kufundishwa tangu utotoni taratibu kwa sbb binadamu anapozaliwa anaishi kwa hisia, ukitazama ni kwamba kila anapokua na hitaji analia ili kutuma message, then anavyokua anafundishwa taratibu kufanya rational thinking, yani km ana njaa badala ya kulia aseme, akihitaji toy achkue, na inaendelea hadi anakuwa na maamuzi ya kufikiria maana tunapoona mtoto kaacha hata tunasema amekua! Ukiona mtu mzima bado yupo emotional ni kwamba tunasema alidekezwa, mtoto wa mama, hakupata malezi bora, nk. Kwa sababu through human growth and development kuna achievements katika kila stage zinategemewa kuonekana anaweza, na ndio maana ukipeleka mtoto clinic unaulizwa maswali anaweza kufanya nini ili walinganishe na benchmark.

So kujibu swali lako ni kutibu ni kufundishwa self awareness/kujitambua in general ambayo ni topic ndefu by itself!
 
Nimerudia kusoma zaidi ya mala 1
Lakini nimechukua hicho kipande hapo👆 Asante Mkuu nimepata kitu
 
Asante sana Mkuu
Hivi ni nini hua kinatokea mpka unasikia mtu akisema Mf: yule anaendeshwa na hisia je kuna namna ya mtu kujigundua kia ni mtu wa hisia zaidi kuliko akili

Na unaweza vp kuthibiti matumizi ya hisia kuliko akili
 
Nimerudia kusoma zaidi ya mala 1
Lakini nimechukua hicho kipande hapo👆 Asante Mkuu nimepata kitu

Yes ukisikia mswahili anasema huyu jamaa ana utoto mwingi ujue anamaanisha ana emotional immaturity au low EQ na anatawaliwa na hisia, na mtu wa namna hii anakuwa na mapungufu mengine mengi kwenye mahusiano na watu kwa kuwa anakuwa more of self directed and selfish asiyejali hisia za wengine au anajali kidogo lakini anajipakulia kila kitu kwa ulafi mkubwa bila kujali maumivu ya watu wengine
 
Hisia ni mihemko ambayo binadamu na wanyama hujisikia moyoni na huathiri mwili pia kupitia ubongo. Kadiri ya saikolojia zinaweza kuwa za pendo, hamu, furaha, au kinyume chake za chuki, woga, hasira, huzuni na nyingine nyingi tu.

Kibiblia zaidi..
Wanadamu wangekuwa wapi kama hatungekuwa na hisia, ikiwa tulikuwa na uwezo wa kudhibiti hisia wakati wote? Pengine tungekuwa kama wakala, tuitikia hali zote kwa mantiki na kamwe si hisia. Lakini Mungu alituumba kwa mfano wake, na hisia za Mungu zinafunuliwa katika Maandiko; Kwa hivyo, Mungu alituumba viumbe vya kihisia. Tunahisi upendo, furaha, uheri, hatia, hasira, kukata tamaa, hofu, nk. Wakati mwingine hisia zetu ni nzuri kwa uzoefu na wakati mwingine sio. Wakati mwingine hisia zetu zinatokana na ukweli, na wakati mwingine hisia "hudanganya" kwa kuwa zinategemea ahadi za uongo. Kwa mfano, ikiwa tunaamini uongo kwamba Mungu hawezi kudhibiti hali ya maisha yetu, tunaweza kupata hisia za hofu au kukata tamaa au hasira kulingana na imani hiyo ya uwongo. Bila kujali, kama hisia ni za nguvu na halisi kwa mtu anayehisi. Na hisia zinaweza kuwa viashiria vya manufaa ya kile kinachoendelea ndani ya mioyo yetu.

Hayo kusemwa, ni muhimu kwamba tujifunze kuhusu kudhibiti hisia badala ya kuruhusu hisia zetu kutudhibiti. Kwa mfano, tunapopatwa na hamaki, ni muhimu kuweza kuacha chenye tunafanya na kutambua kwamba tuna hasira, kuchunguza mioyo yetu kuamua ni kwa nini tuna hasira, na kisha kuendelea kwa njia ya Biblia. Hisia sizizodhibitika huwa hazizalishi matokeo ya kumheshimu Mungu: "Kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu" (Yakobo 1:20).
 
Kwa mkutadha huu ni kwamba hisia ni sehemu nzuri inayotoka ndani inayofanya mambo mbali mbali
Muhimu idhibitiwe
Hisia ni mihemko ambayo binadamu na wanyama hujisikia moyoni na huathiri mwili pia kupitia ubongo. Kadiri ya saikolojia zinaweza kuwa za pendo, hamu, furaha, au kinyume chake za chuki, woga, hasira, huzuni na nyingine nyingi tu.
Sawa sawa dear
 
Umeeleweka mkuu asante🙏
 
ShesRise_1
 
Ni kuhisi
 
Asante sana Mkuu
Hivi ni nini hua kinatokea mpka unasikia mtu akisema Mf: yule anaendeshwa na hisia je kuna namna ya mtu kujigundua kia ni mtu wa hisia zaidi kuliko akili

Na unaweza vp kuthibiti matumizi ya hisia kuliko akili
Mjukuu,
Nadhani wameshajibu tena vizuri kabisa, hasa wanasaikolojia maana hii ni sehemu ya fani yao.

Ila mtu kuendeshwa na hisia ni vile anakosa vitu fulani ili kufanya maamuzi sahihi, anakosa ukomavu wa kihisia(emotional maturity), kama hisia ni hasira, furaha, majonzi, upweke nk maana yake mtu akiwa katika extreme situation ya hasira for instance, anashindwa kujitawala na kufanya irrational decisions, ambazo baadae anakuja kujutia.
Mtu anakuwa mpweke baada tu ya kuachwa na mchumba, anashindwa kujizuia na kujiingiza kwenye mahusiano bila tafakuri ya kina, mwishowe anaumizwa tena.

Kuendeshwa na hisia ni kushindwa kufanya maamuzi sahihi wakati mtu yupo kwenye extreme situation inayohitaji utulivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…