Hisabati: msaada kidogo

Hisabati: msaada kidogo

Ziltan

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Posts
2,746
Reaction score
7,023
Kijiji kilivuna jumla ya magunia 200 ya mazao mbalimbali,

Iwapo ⅕ ni maguni ya maharage, 1/10 ni magunia ya mahindi na sehemu iliyobaki ni ya zao la mtama, je kijiji kilivuna magunia mangapi ya zao la mtama?

Naomba msaada pia itapendeza kama utafanyia kwenye karatasi halafu piga picha utupie hapa nione njia.
asante.

Karibuni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh
1/5 * 200
1/10 * 200
x =200 - (1/5 * 200 + 1/10 * 200)
 
x=200 - ((200÷5) + (200÷10))


Labda tumsaidie kwa njia hii;

(1) --- Idadi ya magunia ya maharage ni, 1/5 ya magunia yote; 1/5×200=40.
(2)---idadi ya magunia ya mahindi ni, 1/10 ya idadi ya magunia yote; 1/10×200=20.

Hivyo idadi ya magunia ya mtama ni;

Idadi yote ya magunia toa jumla ya idadi ya magunia ya maharage na mahindi:-

200- (40+20)=140, hiyo ndiyo idadi ya magunia ya mtama.
 
Kaichabati kanapigaga chenga😜😅
 
Ziltan,
Au unaweza kutumia njia hii;

Maharage ni 1/5 , Mahindi ni 1/10 na Mtama ni sehemu "a" ya Magunia yote ambayo ni sehemu 1 kamili.

# 1/5+1/10+a=1,
Sasa tutafute a ni sehemu gani ya magunia yote.

a=1-(1/5+1/10)
=1-3/10
=10/10-3/10
=7/10.

a=7/10 ya idadi ya magunia yote 200.

Hivyo idadi ya a ambayo ndiyo magunia ya mtama ni:-

7/10×200= 140. Hiyo ndiyo idadi ya magunia ya mtama.
 
Back
Top Bottom