Hisa za NMB zinashuka sana:Ushauri

Hisa za NMB zinashuka sana:Ushauri

Leo 27-10-2026 hisa za NMB zimeshuka mpaka 1,870 , je sisi tulionunua kwa Tshs 2100 baada ya kusikiliza influensa tuziuze saa hii kukwepa hasara zaidi?
Wewe umenunua juzi tu. Mimi nilinunua zikiwa na bei ya 600 tu mpaka leo nimesharudisha faida kwa zile dividents za kila mwaka.

Kabla ya invest yoyote jua unawekeza kwenye kitu gani na malengo yako ni nini!
 
Wewe umenunua juzi tu. Mimi nilinunua zikiwa na bei ya 600 tu mpaka leo nimesharudisha faida kwa zile dividents za kila mwaka.

Kabla ya invest yoyote jua unawekeza kwenye kitu gani na malengo yako ni nini!
SAwaCFE, tunaendelea kujifunza na kutorudia kosa, sasa je niuze maana zinazidi kuporomoka?
 
Sasa mkuu unaona kabisa zimeshuka kwa maana ukiuza zitakuoa hasara sasa unalazimisha uuze ili upate hasara?
Kwani ukisubiri mpaka zikija panda si utauza kwa faida?
Mbona unakosa subra!
 
Atulie! Hisa si kama genge!
Note: Elimu ya Fedha ni muhimu sana
Kwamba zilivoshuka ndo hazipandi tena!!
Kama elimu ya fedha ndo iko hivo dollar ingepotea duniani maana hushuka mno isingepanda.
Elimu ya fedha na fedha yenyewe ni vitu viwili tofauti.
 
Usiuze hata moja, narudia tena usiuze, just hold it. Tena Kipindi hiki cha hisa kushuka ndio inabidi ununue nyingi Sanaa, mm binafsi hisa zikishuka ndio nafurahi Sana kuliko zinavyopanda....zipo Taasisi ambazo hutakiwi kuuza hisa hata moja, miongoni mwao ni NMB, wale walionunua Kwa 600 Kipindi cha nyuma walikuwa hawaelewi pia kama ww....kaza mshipa usiuze ikiwezekana sahau.
 
Back
Top Bottom