Hisa za NMB kupitita NICOL na TCCIA

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,337
5,574
Ndugu zangu, mimi nilinunua hisa za nmb kupitia nicol na tccia mwaka 2006. Tangia hapo sijawahi kupatas gawio hata shilingi moja. Je kuna mtu ambaye aliishawahi kupata gawio kutoka hayo makampuni niliyoyatata. Ili kupata taarifa zaidi juu ya hisa zangu naweza kufanyaje. Naomba ushauri wandugu
 
Ndugu zangu, mimi nilinunua hisa za nmb kupitia nicol na tccia mwaka 2006. Tangia hapo sijawahi kupata gawio hata shilingi moja. Je kuna mtu ambaye aliishawahi kupata gawio kutoka hayo makampuni niliyoyataja. Ili kupata taarifa zaidi juu ya hisa zangu naweza kufanyaje. Naomba ushauri wandugu
 
Hata mimi nilinunua hisa za CRDB kupitia NMB bank mwaka 2009 na sijawai kupata gawio hata summni na hivi sasa nina mpango wa kuzipiga bei kwa kweli sijui hii biashara ya hisa ina mizengwe gani
 
  • Thanks
Reactions: Aza
Mambo ya hisa tunakimbilia tu lakini bado sana, mazingira ya nchi yetu hayana ushawishi mzuri wa mtu kumiliki hisa na kumpatia faidi akaiona zaidi ya wajanja wachache kukopeshana hiyo hela na kujiendeleza kwa kujenga mahekalu, kununua magari, na kusumbua dada zetu kila kukicha.

Huwezi kuwa mwanahisa, harafu ukienda kuulizia unakutana na secretary huyo alivyofuraaaaa utadhani kalazimishwa kuwa pale. Bora ufungue kampuni/Joint venture fulani hivi mkafanya kitu cha maana.
 
tulishaliwa uzeni tu hisa zenu,binafsi niliziuza zote
 
Ndugu zangu, mimi nilinunua hisa za nmb kupitia nicol na tccia mwaka 2006. Tangia hapo sijawahi kupata gawio hata shilingi moja. Je kuna mtu ambaye aliishawahi kupata gawio kutoka hayo makampuni niliyoyataja. Ili kupata taarifa zaidi juu ya hisa zangu naweza kufanyaje. Naomba ushauri wandugu

Hawa walikuwa wakala, wa kuuza hizo hisa, kwani na wenyewe ni wabia NMB, wakumuliza sio NICOL AU TCCIA kawaulize hao NMB wenyewe kwani wao ndio wamiliki wa hisa
 
Hawa walikuwa wakala, wa kuuza hizo hisa, kwani na wenyewe ni wabia NMB, wakumuliza sio NICOL AU TCCIA kawaulize hao NMB wenyewe kwani wao ndio wamiliki wa hisa

Sidhani kuwa umemtendea haki muuliza swali; NICOL na TCCIA waliwashawishi clients wao wapitishe fedha zao kwao ili wao kwa niaba yao ndio wanunue hisa MNB. Hivyo basi gawio lolote kutoka MNB linapelekwa NICOL na TCCIA ambao ndio walinunua hisa kwa niaba ya wanachama wao. Kama hivyo ndivyo wanachama wa Hizo taasisi mbili hawawezi kwenda moja kwa moja MNB kuulizia juu ya dividends zao kwani hulipwa kwa NICOL na TCCIA ambao ndio walikuwa wakala wao!! Wawaulize NICOL na TCCIA dividends zao ziko wapi; they will be lucky if they will find anything kwani at the moment NICOL is in dire straits!!
 
Nenda kawaulize NICOL na TCCIA ambao ndio wanapokea gawio kwa niaba yako!!
 
Ndugu zangu, mimi nilinunua hisa za nmb kupitia nicol na tccia mwaka 2006. Tangia hapo sijawahi kupatas gawio hata shilingi moja. Je kuna mtu ambaye aliishawahi kupata gawio kutoka hayo makampuni niliyoyatata. Ili kupata taarifa zaidi juu ya hisa zangu naweza kufanyaje. Naomba ushauri wandugu

NMB walipouza wewe hukuwaamini? Haya mtafute Mosha au Mengi wakuambie kulikoni?
 
Ndugu zangu, mimi nilinunua hisa za nmb kupitia nicol na tccia mwaka 2006. Tangia hapo sijawahi kupatas gawio hata shilingi moja. Je kuna mtu ambaye aliishawahi kupata gawio kutoka hayo makampuni niliyoyatata. Ili kupata taarifa zaidi juu ya hisa zangu naweza kufanyaje. Naomba ushauri wandugu
Hisa za NMB ziliuzwa kwenye IPO na wananchi walichukua kulingana na kilichopatikana kwa mtindo wa wazi . Hizo za nicol na tccia zilikuwa kabla ya IPO ya NMB ambapo makada kadhaa wa chama walitumika kupiga debe wananchi wachukue hisa hizo kwa mategemeo ya kuwekezwa kwenye NMB mara ubnafsishaji wake ukikamilika .Kikawaida kampuni huwajulisha wanahisa taarifa za maendeleo ikiwamo na kuwaalika kwenye AGM pia maamuzi ya Gawiwo, kama hupati hata mawasilianao kuna giza hapo watafute hao mawakala wakufafanulie vizuri juu ya nini kinaendelea kwenye uwekezaji wako.
 
Asante waugwana kwa majibu.nahisi hapa tumewachangia wajanja kujenga mahekalu.mungu atawaalani
 
Kama NICOL yenyewe ndio hiyo ya Kina Idd Simba we unategemea nini?
 
Sidhani kuwa umemtendea haki muuliza swali; NICOL na TCCIA waliwashawishi clients wao wapitishe fedha zao kwao ili wao kwa niaba yao ndio wanunue hisa MNB. Hivyo basi gawio lolote kutoka MNB linapelekwa NICOL na TCCIA ambao ndio walinunua hisa kwa niaba ya wanachama wao. Kama hivyo ndivyo wanachama wa Hizo taasisi mbili hawawezi kwenda moja kwa moja MNB kuulizia juu ya dividends zao kwani hulipwa kwa NICOL na TCCIA ambao ndio walikuwa wakala wao!! Wawaulize NICOL na TCCIA dividends zao ziko wapi; they will be lucky if they will find anything kwani at the moment NICOL is in dire straits!!

Wewe nadhani ndio hukuelewa walichofanya NICOL na TCCIA

Ni hivi, NICOL na TCCIA waliwashawishi watanganyika wanunue HISA zao, wao wakatumia huo mtaji kununua hisa NMB. sasa kama wewe ulinunua hisa NICOL au TCCIA hiwezi kwenda kudai gawio NMB. kwani haya makampuni mbali na kuwekeza NMB waliwekeza sehemu nyingine, na usifikiri NMB wakigawa gawio kwa wanahisa wao usifikiri TCCIA au NICOL watakugawia gawio kesho yake. mpaka wabalance vitabu vyao kwa kuangalia mapato na matumizi ya mwaka, kama kuna hasara lazima ita affect gawio la kila mwanahisa.

Kama ulinunua hisa moja kwa moja NMB,unayohaki ya kupewa gawio kila wanapotoa,kama ulitaka faida ya mapema ulitakiwa kununua hisa za kampuni ya sigara, simba cement, kampuni ya bia kwenye soko la hisa la dar es salaam. hivi vikampuni vinavyokusanya mitaji, mpaka viiimarike inachukua muda saana. Kwa waliowekeza NICOL ni vema makaandika hasara kwani kampuni iliwekeza kwenye miradi iliyokuwa inakaribia kufa na uongozi wa kampuni ulikuwa mbovu, na kwa sasa kampuni iko kaburini inasubiri kufukiwa
 
ulinunua hisa za nico ambayo iliwekeza hela yako nmb na kwingine walipoona "panafaa", ikiwepo na kiwanda cha madawa cha kakake mengi kilichokua kinakufa!. Sasa nicol yenyewe imesimamishwa dse kwa kutoa taarifa za uongo na kutowakilisha hesabu zake itakiwavyo.↲Walionunua nmb kwenye ipo wanapeta, waliopitia nico maumivu.
 
Back
Top Bottom