Hiroshima yakumbuka miaka 80 ya bomu la atomiki

Hiroshima yakumbuka miaka 80 ya bomu la atomiki

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Mji wa kihistoria wa Hiroshima unafanya kumbukumbu ya miaka 80 tangu Marekani ilipoushambulia mji huo wa magharibi mwa Japan kwa bomu la atomiki
Wengi wa manusura ambao sasa wameshazeeka wakielezea hasira zao kwa jinsi viongozi wa dunia wanavyoonekana kuunga mkono silaha za nyuklia kama njia ya kuoneshana ubabe.

Mmoja wa manusura hao, Minoru Suzuto mwenye umri wa miaka 94, alisema ndani ya kipindi cha miaka 10 hadi 20 ijayo hakutakuwa tena na mtu wa kuelezea uzoefu wa kutisha uliotokana na mashambulizi hayo ya Marekani dhidi ya ubinaadamu.

Tarehe 6 Agosti 1945, Marekani ilidondosha bomu la atomikikwenye mji wa Hiroshima na kuwauwa watu 140,000.

Siku tatu baadaye, iliangusha bomu nyengine kwenye mji wa Nagasaki na kuuwa wengine 70,000.

Matokeo yake, Japan ilisalimu amri tarehe 15 na kuhitimisha Vita vya Pili vya Dunia na uvamizi wake wa nusu karne barani Asia.
 
Back
Top Bottom