Hilo Kokolo kwa Kiswahili Linaitwaje?

Hilo Kokolo kwa Kiswahili Linaitwaje?

Zeni2017

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
1,247
Reaction score
534
a394d99373e780ea37b7f95d16154f69.jpg


Na kazi yake nini?
 
Hizo ni water points kwa ajili ya emergences kama majanga ya moto,usafi au hata maji kwa matumizi mengine.Huwa unachomekwa mpira hapo kwa kazi hiyo.Kama sijakosea mpira huo unaitwa Horse pipe
 
Linaitwa fire hydrant. Kiswahili naona hatujalipatia jina rasmi kwa sababu hatulihitaji.

Gari la zimamoto likiishiwa au likija bila ya maji linaunganisha mpira hapo. Ni bomba lenye msukumo wa maji wa nguvu sana ili kuweza kuzima moto haraka.

Kuna mengine yameunganishwa na mabomba ya maji ya mitaani na mengine yanatokea moja kwa moja kutoka kwenye vyanzo vya maji.
 
Yana rangi tofauti kulingana na nguvu ya maji. Na kuna yanayofanya kazi na yaliharibika.
 
Utayakuta katika kila barabara. Sio moja kwa barabara moja. Ni moja kila upande kiasi cha kila mita mia.
 
Hairuhusiwi kupaki ndani ya futi 15 kutoka kwenye fire hydrant.
48d9344af4c331a40e979c268932d9de.jpg
 
Sababu ni kuwa gari la zimamoto milango yake ya kuzimia moto ina upana huo kama inavyoonyeshwa kwenye picha.
a5cacc80f956300504caa64c0aafee1c.jpg
 
Huyu jamaa akikutwa hapo fine si chini ya 125.
3657495bf81b03c2ac9e39164c659ae9.jpg
 
Huyu jamaa alipewa tiketi ya fine kwa kukalia fire hydrant.
5dc31cf46bbb3ae743684ffe35ee6c48.jpg
 
Ngoma ni fire wako kazini halafu gari lako lizuie nafasi.
702abffd078e0e7743b6861a3a1309e8.jpg
 
Habari kutoka idara ya zimamoto Tanzania zinasema haya mabomba kwa Tanzania yalikuwepo mengi ila kwa sasa hivi hayafanyi kazi na mengine yamevunjwa na mafundi wa majiko na skrepa.
Kuna kipindi jiji zima la Dar lilibakiwa na matatu tu. Mungu anajua sasa hivi yamebaki mangapi.
 
Hii ni huduma muhimu kwa jamii. Tembea mtaani kwako, wilayani na mkoani usipoona fire hydrant mlalamikie mbunge wako na wakuu wa mikoa.

Hizi ndizo kazi zao walizochaguliwa kuwawakilisha wananchi.
 
Hii kokolo nilikua naigonga na gari sana enzi na cheza game ya gt4 .nikiigonga tu maji yana mwagika ila jina lake sikuwahi kulijua
 
Back
Top Bottom