Hillary Clinton kutembelea Kenya. Wakenya watupiga bao. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hillary Clinton kutembelea Kenya. Wakenya watupiga bao.

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by JokaKuu, Jul 28, 2009.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..wadau hili mnalionaje?

  ..hii ni ziara ya kikazi ambapo pamoja Mama Clinton na Mzee Vislack[waziri wa kilimo] pia atakuwepo.

  [​IMG]

  US Secretary of State Hilary Clinton is expected in Kenya to attend a major conference on the African Growth and Opportunities Act

   
  Last edited by a moderator: Aug 3, 2009
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kila kitu bao,muhimu nini benefits za hizo safari kama angekuja tanzania zaidi ya kuwanufaisha mafisadi.alikuja bush tayari sio kila siku waje tu kwetu kuna nchi nyingi africa moja wapo ni kenya.haya mambo wanatupiga bao ,mara wanatupiga bao mlima kilimanjaro ni pumba tu.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  WTF is up with this mentality ya "kupigwa bao" just because some Amerivcan official kawatembelea watu? Au hii ndiyo part ya mentality ya uombaomba?

  Kwa nini hatusemi wakenya mwaka huu wametupiga bao na GDP yao kubwa kulinganisha na yetu, bado tuna ukoko wa ukoloni wa kumsujudia mtu mweupe?
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Clinton alifika Tanzania na bintiye mumewe akiwa Raisi
   
 5. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Wakuu Arsene Wenger na Blueray

  Hata mimi sikutegemea Jokakuu, of all the people, atasema "tumepigwa bao" kwa vile foreign minister wa US haji hapa kwetu kaenda Kenya. Nilipoona kichwa cha thread, na author, nikashangaa na kusikitika kwa kweli...
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  mawazo ya ukoloni na uombaomba hayataisha mpaka mtu ufe make hata wakenya walianza fyoko baada ya Obama kumualika JK ikulu ya white house kama rais wa kwanza wa afrika kukutana naye.

  Miafrika ndivyo tulivyo.......
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..imeelezwa/nimeeleza ziara hiyo ni ya KIKAZI.

  ..mama Clinton anaandamana na Waziri wa Kilimo Tom Vilsack na US Trade Representative.

  ..ujumbe/theme ya ziara ya mama Clinton ni masuala ya AGOA, ambayo ndugu yetu Rev.Kishoka,Mkandara, etc walitumia weekend zao kuyajadili hapa jamii forums.

  ..kwangu mimi naona huu ni ujumbe mzito, uliona na mwelekeo, na unaoweza kuwa na manufaa kwa Wakenya.

  ..wakati Tanzania tunadai Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu, Raisi wetu alipokwenda White House hakuambatana na Waziri wa Kilimo.

  ..sidhani kama Mwai Kibaki amefanya ziara nyingi na zenye gharama kubwa kama za Raisi wetu kwenda USA.

  ..kama ni kuwekeza ktk Diplomasia inaelekea Kenya wanapata returns kubwa kuliko sisi Watanzania.

  ..sisi waTanzania tukitembelewa na ujumbe mzito kama huu unakuta serikali inazungumzia migogoro ya majirani zetu.

  ..Somalia ni jirani na Kenya, mbona Clinton haendi kuzungumzia masuala ya ugaidi na piracy badala yake anakwenda kushughulikia KILIMO na BIASHARA[agoa].

  ..wengine mnanilaumu kwa mentality ya "ombaomba" quite the opposite to my post. ziara ya mama Clinton Kenya itahusu KILIMO na BIASHARA, sasa ombaomba imetoka wapi hapo?

  ..Tanzania ina ardhi kubwa na yenye rutuba kuliko Kenya, tuna amani kuliko Kenya, tuna population/nguvu kazi na kwa maana nyingine soko kubwa kuliko Kenya, sasa inakuwaje ktk masuala ya kilimo na biashara mama Clinton anatembelea Kenya na siyo Tanzania?

  NB:

  ..ndiyo Raisi wetu alikuwa wa kwanza kualikwa White House.

  ..je ni kwanini tumeshindwa kuwa nchi ya kwanza kutembelewa na ujumbe mahsusi toka USA kujadili KILIMO[uti wa mgongo wa taifa letu] na BIASHARA?
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Jokakuu, pamoja na unayosema inabidi kufikiria mara mbili mbili kama kweli kilimo ni bado uti wa mgongo wa taifa letu ili tuone umuhimu wa Ziara hiyo ya mama Clinton au tujisikie vibaya kwa kupigwa 'bao'

  Bado kilimo ni uti wa mgongo?
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Jibu la haraka ni hapana. Nitakusimulia kisa kimoja. Alipokuja rais Kikwete NY 2006 kuna dada mmoja ambaye wazazi wake walimehamishwa ili Barrick ichimbe dhahabu huko Mara alisimama kuuliza swali. Alieleza kuwa wazazi wake wamekuwa na shamba hilo miaka nenda rudi na sasa wanahamishwa. Rais alimjibu kuwa afadhali dhahabu ichimbwe kuliko kilimo. Sasa unadhani huyu akisema kilimo ni uti wa mgongo anaaminika?
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Jokakuu acha mentality ya ubabaikaji wewe. So what kama Clinton na Vilsack watatembelea Kenya? Yaani ndio unazidi ku perpetuate falsafa yangu ya Miafrika Ndivyo Tulivyo.

  Yaani it's like we can't do anything on our own bila msaada wa wazungu. Upuuzi mtupu.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..80% ya waTanzania ni wakulima.

  ..inawezekana viongozi wana mtizamo tofauti, lakini bila ya hii 80% kushirikishwa, kushughulishwa, ili kuwa na mchango ktk taifa letu hii nchi itaendelea kuwa maskini.

  ..kwa msingi huo kilimo bado ni uti wa mgongo, hata kama viongozi wetu wanaamini vingine.

  Nyani Ngabu,

  ..mama Clinton anakwenda Kenya kwa shughuli za kikazi. ziara yenyewe itahusu KILIMO na BIASHARA.

  ..tatizo langu USA wakitu-engage inakuwa ni kwa masuala ya migogoro ya majirani zetu, terrorism, na masuala mengine ambayo hayana tija kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida.

  ..sasa ndiyo maana nasema tumepigwa bao. tunaingia gharama kubwa kwa viongozi wetu kwenda USA lakini matunda yake hayaonekani.

  ..we need to clean our house.

  Bluray,

  ..umezungumzia GDP.

  ..theme ya ziara ya mama Clinton na ujumbe wake ni KILIMO na BIASHARA.

  ..je huoni kwamba masuala hayo yana-relation na GDP?
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wewe unaongea kama vile yashapandisha GDP wakati mtu kaja ziara bwana, wapi na wapi?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Nakubalian ana wewe Dilunga. Tusitegemee kwamba siku zote kila kiongozi maarufu duniani atataka kuja Tanzania kwanza kabla ya nchi nyingine katika Afrika.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Aha! Mmesahau, wapo walioshangilia kwa Jk kuwa rais wa kwanza Afrika kukutana na Obama... ndio muendelezo huo sasa
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  Bluray,

  ..lakini ziara inayohusu KILIMO na BIASHARA is more likely kuwa na real effect kwenye GDP kuliko masuala ya terrorism na migogoro ya majirani zetu ambayo tumezoea kuizungumzia tunapokutana na US officials.

  Bubu-Utaka-Kusema,

  ..kauli yako hapo juu ni ya kujikatisha tamaa.  ..swali ni kwanini tusiwe nchi ya kwanza kutembelewa na uongozi mpya wa Marekani kujadili KILIMO na BIASHARA?

  ..umesahau kwamba Raisi wetu alikuwa kiongozi wa kwanza toka Afrika kualikwa White House?
   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  binafsi sikutegemea jokakuu afulie namna hii......hii thread nilijua author atakuwa Pdidy si great thinker joka
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jul 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  So what kama anaenda Kenya kikazi? Mwache aende na mpaka hapo sijaona bao tulilopigwa

  Jokakuu please...ni mentality tegemezi na ya kijinga kutaka USA watu engage ktk maswala yenye tija kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida. Kwa nini mambo yenye tija kwa Mtanzania wa kawaida tutegemee kutoka nchi nyingine? I'm dissapointed in you for thinking that way.

  Hapana hatujapigwa bao. Wakenya wangekuwa wamepiga hatua kubwa sana kiuchumi kwa kutumia rasilimali na ubunifu walionao hapo ingefaa kusema tumepigwa bao. Lakini ziara ya waziri wa mambo ya nchi za nje na waziri wa kilimo wa Marekani sio kupigwa bao.

  Sasa kama viongozi wetu wanajipendekeza pendekeza kwenda USA hilo ni tatizo lao na letu sisi wananchi.
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  Nyani Ngabu,

  ..hatuwezi kuishi in an "island" or issolation.

  ..sasa tunaposhirikiana na wengine ni bora iwe ktk mambo yenye tija ktk maisha yetu ya kila siku.

  ..my thinking is that, Kenyans made a good impression, ndiyo maana wanakuwa-engaged ktk masuala ya BIASHARA na KILIMO.

  ..wenzetu hawa hawatembezi bakuli. there is something to learn frm them.
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Jul 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Whatever the case I don't see the so called "bao tulilopigwa" with Clinton and Vilsack's visit to Kenya.

  Unanikumbusha rafiki yangu mmoja wa Ki Ghana aliyechukulia ziara ya Obama Ghana kama ujio wa Yesu Kristo....Lol...Waafrika kwa ujumla tuna safari ndeeeeeedu sana.
   
 20. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  They (US/Kenya) have their priorities.

  What's our (Tanzania) priorities?

  What's Kenya/US get in return as you know, there's no free lunch!
   
Loading...