Hillary Clinton atangaza kugombea urais

Hillary Clinton atangaza kugombea urais

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Bi Hillary Clinton ametangaza rasmi kuingia katika kinyang'anyiro cha urais wa nchi hiyo katika uchaguzi wa 2016 ambapo anataka kuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Marekani.

Alizindua ukurasa wake wa kampeni katika mtandao wa internet, Jumapili, akiwaambia Wamarekani kuwa anataka kuwa "kiongozi" wao.

Bibi Clinton aliingia katika mbio za kuomba kuteuliwa na chama cha Democratic kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008 lakini alishindwa kwa Bwana Barack Obama. Akiwa mgombea anayepewa nafasi na wanachama wa Democratic alitarajiwa kutangaza azma yake ya kugombea miezi kadhaa iliyopita.

Katika video kupitia ukurasa wake wa kampeni, Bibi Clinton alitangaza: "Nagombea urais". "Wamarekani wamepambana na nyakati ngumu za uchumi," amesema, "lakini hali imebaki kuwanufaisha walio juu.

Kila siku Wamarekani wanataka kiongozi na nataka kuwa kiongozi," amesema Bibi Clinton pia alikuwa mke wa rais wakati mumewe Bill Clinton alipokuwa rais wa Marekani.

Chanzo:
BBC Swahili.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli Jana nilitizama CNN alikuwa tayari anaonyesha hilo.

Bado ana nafasi kubwa ila siasa haitabiriki!!
 
Hivi sisi ni nani aliyeturoga? Mpaka sasa hatuijui hatma ya Tanzania. Vyama vya siasa acheni uoga waacheni watu wajitangaze ili tuwachuje mapema. Oktoba haiko mbali!!!!
 
Tukijulikana mapema mkuu tutalogwa........ha ha ha ha ha hii ndio tz.
 
Mimi pia nashangaa maana mwez wa 10 upo karibu na Tanzania ni Kubwa
 
Now the GOP knows their nightmare is real!. I can't wait...:smile-big:
 
Farrs-Hillary-2.jpg
 
No way, no how Hillary could win, hana UWEZO WA KUONGOZA....first, she is lucky to use her husband umbrella, and secondly gender issue, ana tegemea sympathy ya wanawake wengi USA...
I do wonder, yaani Democratic, wamekosa watu wenye uwezo wa akina John Kerry atleast, Bill Clinton, etc...
Hillary she has no personal capability to lead, she will be leading from BEHIND....which is not a sign of a good LEADER....
We need new faces in White House, USA sio ya Bushes and Clintons....USA isn't the monarchy...!!!
Hafai...!!
 
Kwani chama kimempitisha? Kama hawezi nani anaweza? Membe, Kigwangala au nani? Wenzetu wanatangaza nia mapema ili watu wapate nafasi nzuri ya kuwatathmini..sisi miezi almost mitano kabla ya uchaguzi hujui nani mgombea urais!
 
Now the GOP knows their nightmare is real!. I can't wait...:smile-big:

.....hehe!, umeona walivyo panic kwenye social media?!, Jeb Bush and Carly Fiorina jumped right in to say something after she came out!
 
Kibongo bongo pole pole ndo mwendo atii!,.....lol!

We have 6 months to go, hatuwafahamu wala kuwa jua wagombea!
 
.....hehe!, umeona walivyo panic kwenye social media?!, Jeb Bush and Carly Fiorina jumped right in to say something after she came out!

Hahaaa... Ngoja tusubiri nyimbo za Benghazi from The GOP!.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Back
Top Bottom